Uchaguzi 2020 SADC yaipongeza Tanzania kwa kuendesha Uchaguzi halali

Uchaguzi 2020 SADC yaipongeza Tanzania kwa kuendesha Uchaguzi halali

Joined
Sep 8, 2020
Posts
67
Reaction score
133
Jukwaa la Tume za Uchaguzi la SADC limeipongeza serikali ya Tanzania kwa kuendesha Uchaguzi halali.

Jukwaa hilo linaundwa na tume za uchaguzi za mataifa 14 ya SADC.

Tamko lililotolewa na jukwaa hilo kutoka makao makuu yake yaliyopo Botswana, linasema NEC na ZEC zimeendesha uchaguzi huru, wa haki, unaoaminika na uliogubikwa na uwazi wa hali ya juu.

Aidha, jukwaa hilo limezitaka nchi wanachama wa SADC kujifunza kiwango cha juu cha demokrasia kilichooneshwa na Tanzania na Zanzibar kwenye chaguzi kuu zake za mwaka 2020.
 
Hayo yalikua yanatarajiwa kwa sababu ni nchi wanachama, Serikali zinazounda hayo mataifa haziwezi kuwa zimetofautiana sana na tawala zinazounda hiyo jumuia ni lazima wajitetee kuwa uchaguzi ulikua huru na haki kwani hata serikali za maeneo yote ya jumuia hio mrengo wao ni ule ule.
 
Shughuli imeisha, JPM amekabidhiwa cheti cha ushindi muda si mrefu, vyama vyote vya upinzani kasoro CHADEMA, ACT na CUF ndio havikuwapo yaani vyama 12 vilikuwapo kushuhudia tukio...Q
IMEISHA HIYO....!
 
Mbona Watanzania wenyewe walikuwepo kwenye vituo vya kupigia kura? Wameona kura kwenye mabegi zikiletwa kwenye vituo, wameona mawakala wa vyama vya upinzani wakifukuzwa, wameona mawakala wa vyama vya upinzani wakinyimwa utambulisho, nk. Picha zimepigwa na video pia?

Hata kabla ya uchaguzi, Watanzania waliona vyombo vya habari zikitangaza habari za CCM na Magufuli tu, wagombea wa vyama vya upinzani wakienguliwa wengine kwa kutekwa ili muda wa kurudisha fomu upite, nk. Hawa SADC ndio nani na wakaa nchi gani? Kama ubeberu upo basi ndio huu wa SADC kuja kuwaambia Watanzania uchaguzi eti ulikuwaje. Ni kichekesho.
 
Habari mbaya sana hii kwa wale wasaliti
 
Back
Top Bottom