Mbona Watanzania wenyewe walikuwepo kwenye vituo vya kupigia kura? Wameona kura kwenye mabegi zikiletwa kwenye vituo, wameona mawakala wa vyama vya upinzani wakifukuzwa, wameona mawakala wa vyama vya upinzani wakinyimwa utambulisho, nk. Picha zimepigwa na video pia?
Hata kabla ya uchaguzi, Watanzania waliona vyombo vya habari zikitangaza habari za CCM na Magufuli tu, wagombea wa vyama vya upinzani wakienguliwa wengine kwa kutekwa ili muda wa kurudisha fomu upite, nk. Hawa SADC ndio nani na wakaa nchi gani? Kama ubeberu upo basi ndio huu wa SADC kuja kuwaambia Watanzania uchaguzi eti ulikuwaje. Ni kichekesho.