Uchaguzi 2020 SADC yaipongeza Tanzania kwa kuendesha Uchaguzi halali

mambo ya kushangaza yanayoendelea TZ.
 
Angalia kauli ya waangalizi wa nje walicho kisema
 
Sasa jamani izonchi zinazounda hilo genge chaguzi zao uwazipo huru ?ilitujuwe maoni yao nikweli mfano kamavile china akosoe au Asifie mimi sishikichochote hapo labda ningesikia marekani tu
 
Usipende kutusemea wa Tanzania eti sisi wa Tanzania!!! Au wewe dada yako na mumewe ndio wa Tanzania wote?
Kwahiyo wafuasi, wapenzi, wafurukutwa na wanachama wa chadema na ACT ni warundi?
 
Kwa nini wakati mwingine unajitoa ufahamu, mbona hapa upo vizuri?

CHADEMA na ACT-Wazalendo walikuwa na nafasi nzuri sana ya kuzuia uchaguzi wakati haya uliyoorodhesha hapa yanatokea,; na sio wakati huu baada ya kuruhusu UCHAFUZI kufanyika.

Ilikuwa ni rahisi zaidi kudhibiti uchafuzi huo katika vituo vyote vya kupigia kura na kusimamisha uchaguzi kila mahali, badala ya kusubiri kura zihesabiwe na matokeo haramu kutangazwa ndipo maandamano yafanyike.

Maandamano haya hayatabadili chochote, sana sana yatakuwa ya kuwaumiza tu baadhi ya majasiri watakaojitoa mhanga kuitetea nchi hii.
 
SADC ni muungano wa madikteta tupu ukitoa Kenya na S. Africa
Aiseee!
Kenya nao wamo?

Unawaweka wapi Botswana, Namibia, na hata Malawi kwa sasa hivi?

Ila inashangaza kwa SADC kutoa taarifa ya namna hii. Hawa ni Secretariat waliotoa taarifa, na hata taarifa yenyewe naona ni ya kujiumauma na aibu nyingi.
 
Ingekuwa vyema zaidi kama ungesema " baadhi ya watanzania"!!!!
Umeona ripoti ya wazungu??? Yaani hata wazungu wameona ubatili, wewe hujauona?? Jiwe alikataliwa kwa kiwango kikubwa Sana.
 
Umeona ripoti ya wazungu??? Yaani hata wazungu wameona ubatili, wewe hujauona?? Jiwe alikataliwa kwa kiwango kikubwa Sana.
Shida Wazungu hawaishi Tanzania, kuna watu kibao wanaomkubali Magufuli wengine hawako hata mitandaoni ukipata bahati ya kukutana na watu mbalimbali/tofautitofauti unaweza ukashangaa idadi ya watu wanaomkubali!! Ndo maana nikasema ni heri kusema baadhi ya Watanzania
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…