Uchaguzi 2020 Saed Ahmed Kubenea: Sijachukua fomu za Kugombea Ubunge CHADEMA Jimbo la Ubungo

Uchaguzi 2020 Saed Ahmed Kubenea: Sijachukua fomu za Kugombea Ubunge CHADEMA Jimbo la Ubungo

Bon kwa mgawanyiko huo kamwe hatashinda jimbo la Ubungo na Kubenea rasmi anaenda kugawa kura za jimbo lile na CCM watashinda jimbo lile kwa urahisi mno!
 
Kwenye siasa ukiwa na roho ndogo kama ya korosho, unakufa kibudu bulee

Uadui kwenye siasa ni ujinga na upumbavu
 
Ukimaliza thread hii kuisoma ingia play store download Chadema digital kisha jiunge na chama kwa njia ya kisasa kabisa.
Kudadeki! Kama uko majuu tuu. Hawa jamaa wako kisasa pengine kuliko chama chochote cha siasa EAC hadi SADC
IMG_20200714_222459.jpg
 
Hamna hata anayemtaka huko cdm, hivyo yeye ni kuvuja kwa pakacha.
Siasa za kubadili gia angani ndio zilizoharibu kina kubenea na wanasiasa wengine vijana aina ya kina Manyika.

Nakumbuka Kubenea alikuwa mwiba mkali sana kwa ccm na selikali kupitia gazeti lake la mwanahalisi.

Baada ya mwenyekti kuchange gia angani na Lowasa kutinga chadema, wanaharakati wengi walikuwa kama wamepigwa ganzi na ganzi hiyo imeendelea mpaka leo.
 
Atapitia ACT , nimeona malalamiko ya viongozi wa Chadema Ubungo jinsi walivyotimuliwa.

Naona yale yale ya NCCR ya akina Marando, Mbatia, Lissu n.k ndio inaifyeka Chadema. Bahati mbaya hawawezi kujirekebisha! Tunaanza upya kujenga upinzani.
 
Siasa za kubadili gia angani ndio zilizoharibu kina kubenea na wanasiasa wengine vijana aina ya kina Manyika.

Nakumbuka Kubenea alikuwa mwiba mkali sana kwa ccm na selikali kupitia gazeti lake la mwanahalisi.

Baada ya mwenyekti kuchange gia angani na Lowasa kutinga chadema, wanaharakati wengi walikuwa kama wamepigwa ganzi na ganzi hiyo imeendelea mpaka leo.

Sio kweli, siasa za Magufuli ndio zilizochangia.
 
" Ni kweli sikuchukua fomu ya kuwania Ubunge wa Jimbo la Ubunge kupitia CHADEMA na kwamba mimi si miongoni mwa wagombea wa CHADEMA watakaopigiwa kura leo kwenye mkutano mkuu wa kura za maoni kwa ajili ya kumpata mgombea wa Ubungo, lakini hiyo hainizuii mimi kugombea kupitia chama kingine, na sababu ni nyingi ikiwemo migawanyiko ndani ya chama na kusakamwa"

amesema Kubenea.

Chanzo: EATV
 
" Ni kweli sikuchukua fomu ya kuwania Ubunge wa Jimbo la Ubunge kupitia CHADEMA na kwamba mimi si miongoni mwa wagombea wa CHADEMA watakaopigiwa kura leo kwenye mkutano mkuu wa kura za maoni kwa ajili ya kumpata mgombea wa Ubungo, lakini hiyo hainizuii mimi kugombea kupitia chama kingine, na sababu ni nyingi ikiwemo migawanyiko ndani ya chama na kusakamwa" amesema Kubenea.
Polepole where are you Kuna fisi kateleza mlimani mvua ilikuwa kubwa changamka Hamfrey kumdaka huyo fisi [emoji3]
 
Huyo na mwenzie si walivunjishwa wakimteta Mwamba!

Ukishapoteza uaminifu kwa Mwenyekiti huwa ndo imeisha hiyo.

Heri Waitara alijiongeza mapema baada ya kuambiwa hana chake 2020.
 
Back
Top Bottom