Saed Kubenea atiwa mbaroni. Afikishwa Mahakamani kwa kuingia nchini kinyume na Sheria, utakatishaji fedha na kupelekwa rumande

Sasa hapa Tunduma mbona tunatakiwa kukamatwa karibia wakazi wote wa hapa?
Kuingia na kutoka nchi jirani kwetu kawaida mno na hatujui sheria inatuchukuliaje?
Sehemu zote za mpakani kubinjuka kawaida
Wenyeji wa pande zote mbili wanazijua chocho

Ova
 

Wamemshika pabaya. Wakati wengine wakiendelea na kampeni, yeye atakuwa anapambana na kesi huku akiwa anasota rumande.
ACT iungane na vyama pinzani ili kumpigia kampeni mgombea mwingine maana huyu atapigwa tarehe za mwezi kwa mwezi hadi uchaguzi upite.
Wasipo kuwa makini hilo jimbo litachukuliwa na sisiem
 
We akili huna, hata kama wewe ni mtanzania kuna namna ya kuingia tanzania. Njia ya kuingia Tanzania ni kupotia mpaka rasmi. Sasa yeye kaingia kupitia isivyo halali, ni lazima akamatwe kwa kuwa hawajui kabeba nini
Muulize kwani yeye Kurudi kwake huwa anapitia Madirishani!?

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Kumbuka Kubenea ametoa maelezo Polisi. Hayo uyasemayo siyo maelezomaliyotoa Polisi. Don't make speculations
 
Hizo pesa si angetumiwa tu kwa account namba yake ya Benki ama hata ya MTU wake wa karibu, ni pesa ndogo sana
 
Akapanda basi kwa tiketi kwa jina la Saed Kubenea mpaka Namanga😂😂 Na apliyemletea MoU akavuka kwa njia za panya kukutana na Kubenea😂😂
 
Hajaonewa, tatizo ni mchoyo na mbinafsi.

Watu kama Kubenea hapendi hata kuona kuna kijana ana millioni mfukoni

Vitu kama hivyo unawatuma tu vijana wako kwenda kukuchukulia pesa sehemu.

Tuache uchoyo matokeo yake ndio haya.
Mkuu ungekuwa wewe ungemtuma kijana?hivi unawajua Watanzania linapokuja suala la uaminifu? mtume mtu hata laki mbili na ndio kwa heri. Nashindwa kwanini mtu kama Kubenea ameshindwa kufuata taratibu na akaingia kwenye mtego wa kitoto, kwani angefuata njia halali na kutaja /kujaza fomu kuhusu hizo pesa yasingemkuta hayo yote.
 
Hapa ndipo ninapokuona wewe ni wakili kanjanja, inawezekana vipi umkamate raia wa Tanzania ndani ya Tanzania na halafu umshtaki kwa kuingia Tanzania isivyo rasmi? Are you mad?

Hivi huko CCM huwa mnavutishwa bangi gani ya kuwatowa akili?
Sheria hujui nyamaza! Kuna utaratibu wa kutoka na kuingia nchini mwako!! Siyo unapitia njia za panya ni kosa la uhamiaji mkuu!
 
😂😂
 
Kushikwa kwa kubenea ni pigo kubwa kwa Lisu
Lissu anakusumbua akili sana ndugu yangu, nimekuja kugundua unampenda sana, ndio mana mda wote yuko kichwani kwako

Kwa siku jina la lissu unaandika zaidi ya mara 50, naamini hata bwana ako atakuwa anapata wivu sana sababu ni lazima keshaliona hili
 
 
Aliyekuwa mbunge wa Ubungo kijana Said Kubenea yuko Mahabusu kwa kosa la kuingiza kiasi kikubwa fedha bila kutoa Maelezo yake.Pia anatakiwa kujibu tuhuma ya kwenda nje ya nchi Na kurudi bila kufuata taratibu za mipaka.
Je hizo ndio fedha za kuchochea vurugu au za nini?
Kwani azifate Kenya?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…