Saed Kubenea atiwa mbaroni. Afikishwa Mahakamani kwa kuingia nchini kinyume na Sheria, utakatishaji fedha na kupelekwa rumande

Kama Wahusika wameamua kuwa na Umakini huu basi usiwe unaishia tu kwa Wanasiasa tena wa Upinzani kwani unafanywa na wengine wengi tu.
Kwa sababu Kubenea ni mwanahabari hivyo kukamatwa kwake ni habari. Isiwe tena kuanzisha lawama zisizo na ukweli bali uzushi tu. Wako wengi mahabusi/gerezani wakisubiri/kukabiliwa na kesi za aina hiyo.
 
Mtanzania ameingia Tanzania sio kihalali? Sijae
Kumbe interest yao ni mambo mengine !
Mimi nilikuwa nasema hilo la kutoka kwenda nchi jirani na kurudi!Huku kwetu ni maisha ya kawaida kabisa na tunaenda kama tunavyoenda chooni!Wengine hadi kuhemea tunahemea nchi jirani!
Ndio mkuu, jamaa alikuwa anatoka "kuuza nchi kwa vipande ishirini vya fedha!"
 
Vitu vingi vinakua haviingii kabisa kichwani, yaani moja haikai mbili nayo tia maji. Katika kipindi kama hiki kwa nini mtu anakuwa anakosa umakini na kuacha nafasi za kutunguliwa, ni kama kumpa adui yako risasi ilhali unajua kwamba given a chance anakumaliza.
 
Hizo receipt za hotel ya Nairobi zenye jina lake na mkataba uliosainiwa Nairobi ni vimeo kwa Kubenea. Ndio maana walitaka aseme alikuwa wapi hizo tarehe na hilo kama hotel aliyotaja Arusha imemruka na kaka/Familia wamesema hakulala kwao ( wanaweza kuhoji hadi watoto) ni msala.

Kama atashindwa kudhibitisha kwa ushahidi alikuwa wapi hizo tarehe inakula kwake mazima wala msijidanganye. Atafute law firm kali imsimamie
 
Kesi dhaifu sana hii, hizi ndio kesi za kuwapa ujiko mawakili

Nitashangaa sana kama wengi hamuoni udhaifu wa mashtaka haya.
Lengo sio kumfunga hapo lengo lao ni kumkomoa kwa kumpotezea muda tu.
 
Urefu wa barua ya mwendesha mashataka "unasema" mengi sana tena kwa sauti! Tunajua.
 
Hiyo kampuni aliyosaini nao MOU labda waje kutetea huko mkataba haukusainiwa Nairobi kitu ambacho si rahisi kujiingiza kwenye hizo risk za udanganyifu.

Kuvuka mpaka na kurudi kwa njia za panya ni kosa na hizo documents plus Kubenea kushindwa kudhibitisha alipokuwa hizo siku ndio msala wenyewe.
 
Kubenea alikua anagombea Kinondoni nasio ubungo, alihama jimbo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…