Saed Kubenea atiwa mbaroni. Afikishwa Mahakamani kwa kuingia nchini kinyume na Sheria, utakatishaji fedha na kupelekwa rumande

Saed Kubenea atiwa mbaroni. Afikishwa Mahakamani kwa kuingia nchini kinyume na Sheria, utakatishaji fedha na kupelekwa rumande

Kama Wahusika wameamua kuwa na Umakini huu basi usiwe unaishia tu kwa Wanasiasa tena wa Upinzani kwani unafanywa na wengine wengi tu.
Kwa sababu Kubenea ni mwanahabari hivyo kukamatwa kwake ni habari. Isiwe tena kuanzisha lawama zisizo na ukweli bali uzushi tu. Wako wengi mahabusi/gerezani wakisubiri/kukabiliwa na kesi za aina hiyo.
 
Mtanzania ameingia Tanzania sio kihalali? Sijae
Kumbe interest yao ni mambo mengine !
Mimi nilikuwa nasema hilo la kutoka kwenda nchi jirani na kurudi!Huku kwetu ni maisha ya kawaida kabisa na tunaenda kama tunavyoenda chooni!Wengine hadi kuhemea tunahemea nchi jirani!
Ndio mkuu, jamaa alikuwa anatoka "kuuza nchi kwa vipande ishirini vya fedha!"
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

YAH: KUFIKISHWA MAHAKAMANI KWA SAED AHMED KUBENEA

Mnamo tarehe 5/9/2020, Jeshi la Polisi Tanzania lilimkamata SAED AHMED KUBENEA akiwa katika gari la abiria lenye namba ya usajili T. 645 DKR akitokea kwenye mpaka wa Tanzania na Kenya, eneo la Namanga akielekea Arusha mjini.

Mara baada ya upekuzi, mtuhumiwa huyo alikutwa, pamoja na vitu vingine, Dola za Marekani Elfu Nane (USD 8000), Shilingi za Kenya Laki Nne Tisini na Moja Elfu Mia Saba (KES 491,700), Shilingi za Kitanzania Elfu Sabini na Moja (TZS 71,000/-), tiketi ya basi la Super Couch lenye namba ya usajili KCP 4230 ya tarehe 05/09/2020 kutoka Nairobi, Kenya kwenda Namanga, ‘Memorandum of Understanding’ kati ya Hali-Halisi (Tanzania) na Buni Media Limited (Kenya), Risiti ya malipo ya hoteli iitwayo After 40 Hotels Limited iliyopo Nairobi, Kenya yenye jina la Kubenea, Saed Ahmed kama mgeni kuanzia tarehe 3/9/2020 hadi 5/9/2020 na. Pasi yake ya kusafiria (Passport).

Mara baada ya kukamatwa, mtuhumiwa alieleza kuwa alifika mkoani Arusha tarehe 2/9/2020 akitokea Dar es Salaam na kufikia katika hoteli iliyopo Arusha mjini. Alieleza zaidi kuwa, tarehe 3/9/2020, alienda kulala kwa Kaka yake tarehe 3/9/2020, na tarehe 4/9/2020 alienda Namanga na kupokea fedha taslimu tajwa hapo juu kutoka kwa raia wa Kenya.
Hata hivyo, mara baada ya kupitia Ushahidi uliokusanywa nimebaini kuwa:-

1. Mtuhumiwa SAED AHMED KUBENEA hakufikia katika hoteli aliyoitaja Arusha mjini, wala kulala kwa Kaka yake kama alivyoeleza.

2. Mtuhumiwa tajwa alivuka Mpaka usio rasmi na kuelekea Nairobi nchini Kenya na kisha kurejea nchini Tanzania bila kutumia Mpaka rasmi mnamo tarehe 5/9/2020.

3. Mtuhumiwa tajwa aliingiza nchini Fedha za Kigeni (foreign currency) bila kutoa tamko rasmi la kisheria kinyume na masharti ya Kanuni za the Anti-Money Laundering (Cross - Border Declaration of Currency and Bearer Negotiable Instruments) Regulations, 2016 zikisomwa pamoja na Kifungu cha 28B(1)(a) cha Sheria ya Kuzuia Utakasishaji wa Fedha Haramu, Na. 12 ya Mwaka 2006.

Hivyo, leo tarehe 7/9/2020, mara baada ya kujiridhisha na uwepo wa ushahidi wa kutosha dhidi ya mtuhumiwa tajwa, sambamba na misingi ya kikatiba inayoniongoza kama ilivyoanishwa katika Ibara ya 59B(4)(a) hadi (c) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, nimeidhinisha mashtaka yafuatayo dhidi ya mtuhumiwa SAED AHMED KUBENEA:-

a. Kuingia nchini Tanzania kinyume na Sheria ya Uhamiaji, Sura ya 54 Marejeo ya mwaka 2016; na
b. Kuingiza nchini fedha za Kigeni bila kutoa tamko kinyume na Kanuni za Utoaji Tamko la Fedha Mpakani za mwaka 2016.

View attachment 1561443
View attachment 1561444
Vitu vingi vinakua haviingii kabisa kichwani, yaani moja haikai mbili nayo tia maji. Katika kipindi kama hiki kwa nini mtu anakuwa anakosa umakini na kuacha nafasi za kutunguliwa, ni kama kumpa adui yako risasi ilhali unajua kwamba given a chance anakumaliza.
 
Hizo receipt za hotel ya Nairobi zenye jina lake na mkataba uliosainiwa Nairobi ni vimeo kwa Kubenea. Ndio maana walitaka aseme alikuwa wapi hizo tarehe na hilo kama hotel aliyotaja Arusha imemruka na kaka/Familia wamesema hakulala kwao ( wanaweza kuhoji hadi watoto) ni msala.

Kama atashindwa kudhibitisha kwa ushahidi alikuwa wapi hizo tarehe inakula kwake mazima wala msijidanganye. Atafute law firm kali imsimamie
 
Urefu wa barua ya mwendesha mashataka "unasema" mengi sana tena kwa sauti! Tunajua.
 
Hiyo kampuni aliyosaini nao MOU labda waje kutetea huko mkataba haukusainiwa Nairobi kitu ambacho si rahisi kujiingiza kwenye hizo risk za udanganyifu.

Kuvuka mpaka na kurudi kwa njia za panya ni kosa na hizo documents plus Kubenea kushindwa kudhibitisha alipokuwa hizo siku ndio msala wenyewe.
 
Kubenea amehama Chadema na kuhamia ACT, na kwa uhasama pale Ubungo.

Chadema Ubungo imepasuka sababu ya ishu yake na Boni (mtu wa Mbowe).

ACT Ubungo ndo chama pekee kilichomuwekea Boni pingamizi pamoja na wagombea wote udiwani wa CHADEMA UBUNGO. Hili pingamizi la ACT ndo limemuengua Boni kugombea ubunge Ubungo. Kitu ambacho hakiwezi kufurahisha akina Mbowe.

Kwahiyo sidhani kama Kubenea anashirikiana na Lissu, ili hali akina Mbowe na wenzake wanammind.
Kubenea alikua anagombea Kinondoni nasio ubungo, alihama jimbo.
 
Back
Top Bottom