Saed Kubenea atiwa mbaroni. Afikishwa Mahakamani kwa kuingia nchini kinyume na Sheria, utakatishaji fedha na kupelekwa rumande

Saed Kubenea atiwa mbaroni. Afikishwa Mahakamani kwa kuingia nchini kinyume na Sheria, utakatishaji fedha na kupelekwa rumande

Hapa ndipo ninapokuona wewe ni wakili kanjanja, inawezekana vipi umkamate raia wa Tanzania ndani ya Tanzania na halafu umshtaki kwa kuingia Tanzania isivyo rasmi? Are you mad?

Hivi huko ccm huwa mnavutishwa bangi gani ya kuwatowa akili?
Mkuu nenda taratibu. Mimi nahusikaje na suala hili na CCM? Hebu punguza mihemko isiyo na maana
 
Kwahiyo Watanzania wa Namanga hawaruhusiwi kupanda mabasi?

Hivi ukikutana na mtu boda akakulipa deni lako wewe ukageuza kurudi Arusha shida iko wapi?

Je Mtanzania haruhusiwi kuwa na dollar mfukoni?

Mkuu kwa sheria za sasa mpakani au hata hapa ndani ukikutwa na $ 1000 na kuendelea lazima uende kutoa maelezo polisi wakikukamata ,lazima uonyeshe risiti zake ,siyo mpakani tu hata kuvuka kutoka Zanzibar kuja bar ukikaguliwa ukakutwa na zaidi ya dolla 1000 maelezo ya msingi na risiti zake lazima ukamatwe ,hiyo ni baada ya kufunga bureau de change nyingi mjini
 
Watanzania lazima tujifunze sheria,makosa upelekea kuanzishwa sheria ndio maana naeleza kuwa kutokana na umaarufu wa kubenea kama kweli alikwenda Kenya bila kufuata sheria ya kuingia au kutoka nchini iyo kesi itamsumbua,mwanasheria ameeleza kuwa alikwenda huko na kuna ushahidi wa makubaliano Fulani ya kampuni Fulani ya Kenya kushirikiana na kampuni za kubenea sasa mnajua kuwa ni wazi alikwenda Kenya hatujui kama alipitia mlangoni au dirishani na kama alipitia mlangoni aonyenye vyombo vya usalama vinafuatilia sana watu kutokana na uhatari wa MTU mwenyewe,nchi zote duniani zinafuatilia mienendo ya watu wenye mashaka nao kuhusiana na kuhatarisha usalama wa taifa.
Kwahiyo unataka kutuambia muwakilishi wa kampuni ya Kenya hawezi kuja Namanga na wakasaini MoU na yule Mkenya kuvuka boda kurudi kwao?

Why Kubenea tu na siyo kwamba Mkenya alikuja yeye Namanga?
 
Kwa vyovyote itakavyokuwa, Kubenea anagombea ubunge, jimbo la Kinondoni kupitia ACT-Wazalendo hivyo anahitaji pesa kuendesha kampeini. Inawezekana walinasa mazungumzo yake kwenye simu wakamlia dip la static surveillance/connaissance, kisha wakamuingiza king.
Nimekuelewa sana ila nilitaka kufafanua zaidi kwa sababu hapa tayari kuna watu wanasema kuwa ni msaada wa fedha za kampeni kutoka mataifa mengine. Nina maana kuwa hajalipwa kwa ajili ya kampeni per se bali ni kwa kazi nyingine japo kuna uwezekano mkubwa akazitumbukiza kwenye kampeni
 
Kwahiyo unataka kutuambia muwakilishi wa kampuni ya Kenya hawezi kuja Namanga na wakasaini MoU na yule Mkenya kuvuka boda kurudi kwao?

Why Kubenea tu na siyo kwamba Mkenya alikuja yeye Namanga?
Watu wanadhani mahakani mambo yanaenda kwa hisia. Na hizo risiti za hotel na bus atasema huyo mwakalishi alikuwa ameninunulia akidhani nitaenda hivyo amekuja nazo ili gharama zake ziweze kuwa deducted
 
Kwahiyo unataka kutuambia muwakilishi wa kampuni ya Kenya hawezi kuja Namanga na wakasaini MoU na yule Mkenya kuvuka boda kurudi kwao?

Why Kubenea tu na siyo kwamba Mkenya alikuja yeye Namanga?
Kwa huyo mwanasiasa aliyekuwa anaipinga serika ya Magufuli ana Hali mbaya.

Unazungumzia Sheria?
Utawala wa 'hila' Kama atachomoka basi atakuwa na 'Allah' wake!
 
Roho ya usaliti huandamana na mhusika hadi kiyama, kalale panapokustahili kubenea!
sawa na yule aliyesaliti CHADEMA na kusababisha mrembo Acqulina kuuawa na wenzio kufungwa, dhambi zile zitamwandama hadi siku ya kufa atakufa huku ameachama mdomo kwa mateso!
 
Kwa huyo mwanasiasa aliyekuwa anaipinga serika ya Magufuli ana Hali mbaya.

Unazungumzia Sheria?
Utawala wa 'hila' Kama atachomoka basi atakuwa na 'Allah' wake!
Kwenye Court of law hatuongei kiholela, tunashindanisha hoja.

Ndio sababu Dpp anashindwa kesi nyingi.

Kesi hii haikuwa na uharaka huo wa kukimbilia mahakamani, walipaswa kutafuta ushahidi na uhakika wa kushinda kesi mahakamani, Dpp hawezi kushinda kesi hii.

Mimi sijadili kisiasa, najadili kwa fact and evidence.
 
Hivi huyu ndiyo alituunga juhudi kwa namna ya kipekerr? Naona Chadema huwa mnasali sana kuomba adhabu ya Mungu kwa wasaliti wenu maana naona wote wameangukia pua la mbwa koko la Baridiiii.
 
Kwahiyo unataka kutuambia muwakilishi wa kampuni ya Kenya hawezi kuja Namanga na wakasaini MoU na yule Mkenya kuvuka boda kurudi kwao?

Why Kubenea tu na siyo kwamba Mkenya alikuja yeye Namanga?
Umeelezwa mpaka hoteli aliyolala Kenya na risiti zake,pia tiketi za basi nazo zimetajwa kutokea Kenya sasa uelewi nini,ni bora ungesema tusubiri atakapojitetea mahakamani sema miaka hii serikali haishindwi kesi kwa sababu ushahidi haupotezwi kama zamani,yanakamatwa madawa ya kulevya kwenye kipimo unakuta unga wa ngano,kwahiyo uwezekano wa kupatikana na hatia ni mkubwa wasingempeleka mahakamani mapema hivi kama wangekuwa hawana ushahidi.
 
Kuna maalfu ya Watanzania wanaOver stay kwenye nchi za majirani kwa miaka ili kukwepa adhabu huwa wanarudi nchini kwa nchini kwa njia za panya

Huyu Kubenea alikuwa kwenye radar
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

YAH: KUFIKISHWA MAHAKAMANI KWA SAED AHMED KUBENEA

Mnamo tarehe 5/9/2020, Jeshi la Polisi Tanzania lilimkamata SAED AHMED KUBENEA akiwa katika gari la abiria lenye namba ya usajili T. 645 DKR akitokea kwenye mpaka wa Tanzania na Kenya, eneo la Namanga akielekea Arusha mjini.

Mara baada ya upekuzi, mtuhumiwa huyo alikutwa, pamoja na vitu vingine, Dola za Marekani Elfu Nane (USD 8000), Shilingi za Kenya Laki Nne Tisini na Moja Elfu Mia Saba (KES 491,700), Shilingi za Kitanzania Elfu Sabini na Moja (TZS 71,000/-), tiketi ya basi la Super Couch lenye namba ya usajili KCP 4230 ya tarehe 05/09/2020 kutoka Nairobi, Kenya kwenda Namanga, ‘Memorandum of Understanding’ kati ya Hali-Halisi (Tanzania) na Buni Media Limited (Kenya), Risiti ya malipo ya hoteli iitwayo After 40 Hotels Limited iliyopo Nairobi, Kenya yenye jina la Kubenea, Saed Ahmed kama mgeni kuanzia tarehe 3/9/2020 hadi 5/9/2020 na. Pasi yake ya kusafiria (Passport).

Mara baada ya kukamatwa, mtuhumiwa alieleza kuwa alifika mkoani Arusha tarehe 2/9/2020 akitokea Dar es Salaam na kufikia katika hoteli iliyopo Arusha mjini. Alieleza zaidi kuwa, tarehe 3/9/2020, alienda kulala kwa Kaka yake tarehe 3/9/2020, na tarehe 4/9/2020 alienda Namanga na kupokea fedha taslimu tajwa hapo juu kutoka kwa raia wa Kenya.
Hata hivyo, mara baada ya kupitia Ushahidi uliokusanywa nimebaini kuwa:-

1. Mtuhumiwa SAED AHMED KUBENEA hakufikia katika hoteli aliyoitaja Arusha mjini, wala kulala kwa Kaka yake kama alivyoeleza.

2. Mtuhumiwa tajwa alivuka Mpaka usio rasmi na kuelekea Nairobi nchini Kenya na kisha kurejea nchini Tanzania bila kutumia Mpaka rasmi mnamo tarehe 5/9/2020.

3. Mtuhumiwa tajwa aliingiza nchini Fedha za Kigeni (foreign currency) bila kutoa tamko rasmi la kisheria kinyume na masharti ya Kanuni za the Anti-Money Laundering (Cross - Border Declaration of Currency and Bearer Negotiable Instruments) Regulations, 2016 zikisomwa pamoja na Kifungu cha 28B(1)(a) cha Sheria ya Kuzuia Utakasishaji wa Fedha Haramu, Na. 12 ya Mwaka 2006.

Hivyo, leo tarehe 7/9/2020, mara baada ya kujiridhisha na uwepo wa ushahidi wa kutosha dhidi ya mtuhumiwa tajwa, sambamba na misingi ya kikatiba inayoniongoza kama ilivyoanishwa katika Ibara ya 59B(4)(a) hadi (c) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, nimeidhinisha mashtaka yafuatayo dhidi ya mtuhumiwa SAED AHMED KUBENEA:-

a. Kuingia nchini Tanzania kinyume na Sheria ya Uhamiaji, Sura ya 54 Marejeo ya mwaka 2016; na
b. Kuingiza nchini fedha za Kigeni bila kutoa tamko kinyume na Kanuni za Utoaji Tamko la Fedha Mpakani za mwaka 2016.

View attachment 1561443
View attachment 1561444
Nyumba yako mwenyewe lakini waingilia Dirishani, kunani Saed🙂
 
Kwenye Court of law hatuongei kiholela, tunashindanisha hoja.

Ndio sababu Dpp anashindwa kesi nyingi.

Kesi hii haikuwa na uharaka huo wa kukimbilia mahakamani, walipaswa kutafuta ushahidi na uhakika wa kushinda kesi mahakamani, Dpp hawezi kushinda kesi hii.

Mimi sijadili kisiasa, najadili kwa fact and evidence.
Sasa basi, naichukua hiyo sentensi ya

'Ndio sababu DPP anashindwa kesi nyingi.'

DPP anashindwa kesi nyingi sababu zipo 'associate'na matamko au maelekezo ya kisiasa! Hasa kwa upande kinzani na Serikali kuu ya mizuka!
 
Back
Top Bottom