Saed Kubenea atiwa mbaroni. Afikishwa Mahakamani kwa kuingia nchini kinyume na Sheria, utakatishaji fedha na kupelekwa rumande

Saed Kubenea atiwa mbaroni. Afikishwa Mahakamani kwa kuingia nchini kinyume na Sheria, utakatishaji fedha na kupelekwa rumande

Hapa ndipo ninapokuona wewe ni wakili kanjanja, inawezekana vipi umkamate raia wa Tanzania ndani ya Tanzania na halafu umshtaki kwa kuingia Tanzania isivyo rasmi? Are you mad?

Hivi huko CCM huwa mnavutishwa bangi gani ya kuwatowa akili?
Hivi kweli hata kusoma tu ukaelewa habari NI ngumu hivi? Hujasoma kwamba amekwenda Kenya bila kupitia mpakani rasmi inamaana amepita njia za chochoroni au hujawahi kusafiru kutoka nchi Moja kwenda nchi nyingine na ukajua taratibu za kuvuka mpaka wannchi Moja kwenda nchi nyingine?

Halafu unamwambia mwenzako kanjanja.

Jamaniiii
 
Kama Wahusika wameamua kuwa na Umakini huu basi usiwe unaishia tu kwa Wanasiasa tena wa Upinzani kwani unafanywa na wengine wengi tu.
muhimu ni information tu
huyo kachomwa,inawezekana hata hiyo pesa na hao waliomwita ni wakala wa JMT walimtaka tu mtu wao
 
muhimu ni information tu
huyo kachomwa,inawezekana hata hiyo pesa na hao waliomwita ni wakala wa JMT walimtaka tu mtu wao

Nakubaliana nawe hapa tena kwa 100% kuwa hapa ni lazima tu 'Chezo' limechezwa vyema na SSIT halafu Kubenea nalo 'Kalivagaa' na amedakwa.
 
Kaa kimya, kina Tito Magoti wanaozea sello kwa kutakatisha laki saba tu!
Kwanini nikae kimya mkuu wakati nashangaa kwanini watanzania wawe charged kwa viwango kama hivyo vya pesa? There's must be something else out of money loundering.

Siasa hizi zinaletwa na chama kinachotumia dola kudhoofisha nguvu za upinzani ili wawajaze uoga wananchi na kupata kibali cha kuendelea kutawala miaka mingi ijayo.
 
Kwanza Mleta mada amefanya exaggeration ya hali ya juu kwenye heading yake anaposema suala la "utakatishaji fedha"!

Na ingawaje Wachangiaji wengi wamezungumzia suala la utakatishaji pesa lakini hakuna cha utakatishaji fedha hapo! Labda hawa nao wamekuwa misled na Mleta Mada!

Na ukiangalia hiyo press release, utaona kosa kubwa la Kubenea hapo ni kuikwepa custom/entry point. Hilo suala la kuikwepa custom ndicho DPP ameita kuingia nchini kinyume cha sheria!

Kwavile aliikwepa custom, automatically akawa amevunja Sheria ya Kuzuia Utakatishaji Fedha iliyotajwa hapo juu, Ibara ya 5(1) ambayo inatamka wazi kwamba mtu hataondoka au kuingia Tz bila kufanya declaration ya foreign currency kwa kiwango tajwa.

Suala la kuto-declare peke yake halihitimishwi kwa kusema eti amefanya money laundering kwa sababu undeclaration or false declaration of currency ni kosa linalojitegemea na money laundering ni kosa lingine kabisa!

As said, ukiangalia mtiririko wa hiyo PR, inaonesha Kubenea alitoka Nairobi na Super Coach, lakini alipofika karibu na mpaka, akateremka "akala chochoro" ili kukwepa custom hadi upande wa TZ ndipo akapanda basi lingine ambalo walimdaka!!

Wakati anafanya hayo, it's obvious kuna mtu akamchoma!!

Kama asingefanya hayo na kupita custom lakini akaacha ku-declare au kufanya false declaration, basi hata baada ya kukamatwa issue huenda isingekuwa kubwa kiasi hicho kwa sababu angeingia kwenye matata makubwa endapo tu ingeonekana hizo pesa ni kwa ajili ya ku-finance terrorism, au alikuwa na nia ya kufanya money laundering or any other offense.

Lakini kwavile DPP amejinadai kufanya uchunguzi lakini hatimae walihitimisha kutomuona na tuhuma yoyote kati ya hizo tatu hapo juu na kwahiyo issue inabaki kwa kuto-declare na kula chochoro.

Kwa maana nyingine, tayari DPP amejiridhisha hizo USD 8000, na KES 491,700 ni pesa halali na kwa matumizi halali.

Na kama hivyo ndivyo, basi lau kama asingekula chochoro, kosa kwake lingekuwa hilo la kuto-declare ambalo si ajabu angepigwa tu penalty na yakaisha!

Na hata ikithibitika "alikula chochoro", bado sioni kama ni serious offense kama inavyojaribu kuzungumzwa hapa na wengine.
 
Hili ndilo swali nililokuwa najiuliza. Hapo polisi walipaswa wajiridhishe tu kama huko Kenya alienda kihalali kwa kukagua passport yake bass. Ila kwa upande wa uvushaji pesa hapo jamaa wamepata sababu though ni kiwango cha kawaida sana kusema ni ishu ya money loundering
Man,

Hiyo sheria ipo karibu duniani kote na kiwango ndo hicho cha USD 10K, na sio Tanzania tu. Hata US ambako unaweza kusema USD 10K ni kiwango cha kawaida bado kama unataka kusafiri nje ya US na kiwango equal or greater than 10K ni LAZIMA ufanye declaration.

Aidha, issue hapa sio "kuvusha" pesa bali ku-declare kiwango cha pesa... simple like that! Kwanza hata hiyo fomu yenyewe unayotakiwa kujaza ni ya kawaida tu... swali pekee ambalo unaweza kusema ni "gumu" ni matumizi ya pesa husika!!

So, unless iwe hizo pesa hakukutwa nazo na amebambikiwa lakini kama amekutwa nazo, hapo kuna uvunjaji wa sheria ingawaje sio serious issue namna hiyo kama inaonekana pesa ni halali na ni kwa matumizi halali!!
 
Pamoja na kuwa alijitoa CHADEMA na kujiunga ACT-Wazalendo, hii isiwe sababu ya sisi wa upande wa upinzani kufurahia yaliyomkuta kwani safari ya kuelekea Oktoba 28 bado inaendelea...
YOU'RE RIGHT... Waswahili wanasema "tunajenga nyumba moja, yanini kugombea fito"! Tena watu wasisahau Kubenea alichangia kwa kiasi kikubwa sana kuibomoa serikali ya CCM ya JK!
 
Wakati mwingine mnajitoa ufahamu. Mtuhumiwa ameingia na kutoka nchini Kenya bila taarifa zake kuwapo mpakani. Ushahidi ni risiti ya Hotel aliyolala Nairobi, Memorandum of Understanding iliyosainiwa Nairobi na tiketi ya basi alilopanda toka Nairobi kwenda Namanga, unashangaa nini? maana yake Usafiri wake wa kwenda na kurudi ulikuwa ni wakuishia Namanga na kisha kuvuka kutumia njia za Panya, njia haramu.
Like serious?! Yaani tiketi, MoU na risiti ndio ushahidi wa kuthibitisha aliingia na kutoka Kenya bila kufuata sheria?!

What kama Kubenea kilichomtoa Dar ni safari ya kikazi/kibiashara kati ya Hali-Halisi na Buni Media ya Kenya lakini kwavile Halisi ni kampuni akaamua kutaka kuwadanganya wabia wenzake wa Halisi kwamba alienda Nairobi na akalala hotel ili hatimae achikichie pesa ya nauli na ya hotel?!

Lakini badala ya kwenda hadi Nairobi, partners wa Kenya (Buni Media) wakamaliza kila kitu kwa upande wao, including MoU signing kisha wakampa mtu ambae alileta hiyo MoU including anything else hadi mpakani upande wa KE na ndipo Kubenea nae akaifuata akiwa upande wa TZ kisha akarudi na kupanda basi ambako ndimo walimkuta na kumkamata?!

Hivi yule mtu aliyekuwa mpakani upande wa KE, akifunga mizigo labda kwenye mfuko kisha akaurushia upande wa Tanzania na hatimae Kubenea kuchukua mzigo husika ina maana hapo itakuwa aliingia Kenya na hatimae kurudi TZ kwa njia isiyo halali?!
 
Pamoja na kuwa alijitoa CHADEMA na kujiunga ACT-Wazalendo, hii isiwe sababu ya sisi wa upande wa upinzani kufurahia yaliyomkuta kwani safari ya kuelekea Oktoba 28 bado inaendelea.

La msingi kuliko yote ni kuwa,tusimuhumu ili hali hatujasikia chochote kutoka Kwake na tusiwe kama ni wageni katika nchi hii.

Subirini kuona hiyo kesi itavyoendeshwaa na zaidi hatima ya kesi yenyewe.

Tujipe muda
Kwamba hamjui kama mlimtuma enh!!!???
 
Sasa hapa Tunduma mbona tunatakiwa kukamatwa karibia wakazi wote wa hapa?
Kuingia na kutoka nchi jirani kwetu kawaida mno na hatujui sheria inatuchukuliaje?
 
Atakuwa alienda kutafuta pesa za kufanyia kampeni, huu mchoro inawezekana atakuwa amechomwa na mtu wake wa karibu, kosa limefanywa kuwa kubwa kwasababu ya nafasi yake aliyokuwa nayo kisiasa, hapo hakuna dhamana na ndoto za ubunge ndio zimekwisha.
Hivi lisu yeye pess zake za kampeni analetewa na nani kutoka kule kwa Amsterdam maan nasikia hadi anakodisha ndege
 
Wakati mwingine mnajitoa ufahamu. Mtuhumiwa ameingia na kutoka nchini Kenya bila taarifa zake kuwapo mpakani. Ushahidi ni risiti ya Hotel aliyolala Nairobi, Memorandum of Understanding iliyosainiwa Nairobi na tiketi ya basi alilopanda toka Nairobi kwenda Namanga, unashangaa nini? maana yake Usafiri wake wa kwenda na kurudi ulikuwa ni wakuishia Namanga na kisha kuvuka kutumia njia za Panya, njia haramu.
Kwanini unaamini risiti ni proof kuwa alikuwa Nairobi?
1. Risiti ya Hotel: Alikuwa ana mpango wa kwenda kulala Nairobi akamwomba mwenyeji wake amchukulie chumba cha kulala halafu atakuja kumrudishia fedha zake. Lakini kwa bahati mbaya hakwenda hivyo mwenyeji akamletea mpaka pale mpakani ili amrudishie fedha zake. Pia tiketi ya basi alikuja nayo mwenyeji wake mpaka Namanga. ambako walisaini hiyo MoA.
 
å Sometimes sisi wanadamu ni ngumu sana kuacha mazoea yetu hasa ya kuumiza na kubagaza watu wengine....

å Aidha ukiangalia namna mambo yalivyo kwa jicho la kibinadamu, kwa mazoea ya kibinadamu na kwa kusikia kwa sikio la kibinadamu, ni ngumu sana mtu kuamini kuwa mambo yanaweza kubadilika kwa kufumba na kufumbua tu macho...

å Tundu Lissu wiki tatu au nne zilizopita alilisema juu ya hali ya utawala huu chini ya CCM ya Magufuli, kwamba kupitia sanduku la kura kamwe hawawezi kushinda hapo Oktoba 28, 2020....!!

å Alionya kuwa, wao CCM na MAGUFULI wanalijua na kulitambua hili vilivyo, lakini wana advantage moja tu.....wanaongoza serikali na wanaweza kutumia faida hii kujipatia ushindi wa mezani kirahisi kabisa ktk uchaguzi ili kuendeleza mateso ya wananchi....

å Aliendelea kusema, njia rahisi na ya kipekee ni kufanya "systematic pull out" ya wagombea wa vyama vingine kwa njia za kisheria na uhuni mwingine wowote unaowezekana. Naona watu kama Saed Ahmed Kubenea hawakumwelewa Tundu Lissu na sasa yanawatokea...

å Tazama na sikiliza tahadhari ya TL ktk video hii [emoji116] [emoji116][emoji116]
View attachment 1561499
Do nyie watu bana kila Siku nfonjera zile zile ..mada ilyopo mezani ni kubenea kukamatwa na tsh 28m akitokea Kenya..
 
Back
Top Bottom