Saed Ramovic: Ligi ya Algeria ina Ushindani mkali kuliko Tanzania, ambapo kuna timu Tatu tu!

Hamna kocha hapo
 
huyo hakuwa kocha. sababu kibao. ukisikia kuna wazungu matapeli, sidhani kama huyo atakosa. anasema ameshindwa kuwavusha yanga kwa sababu ligi ni laini, wakati huo huo wenzake simba wamefanya vizuri, na gamond alikuwa bora kuliko yeye, kama sio tapeli ni nini sasa huyu. kwa hiyo simba wanatoka ligi ipi, si hii hii?
 
Kwani Algeria mbona timu ni zile zile miaka yote. Hizo timu nyingine mbona kimataifa huwa hatuzioni.
 
Ndiyo ukweli wenyewe hata kama ni mchungu.ukiondoa yanga(wanaume),Simba(wa mama) na azamu kunakuwa hakuna ligi
 
Ujeeremani kuna timu ngapi huyu fundi Bomba asituzingue.
 
Simba wanacheza mechi halisi, yanga ananunua timu pinzani anajizolea migoli tuu
 
Yuko sahihi kabisa Kwa asilimia zote. Ligi yetu timu ni mbili. Simba na Yanga, Azam kidogo zilizobaki zinasindikiza tu, yaani alichomaanisha udhaifu uliopo ni collectively. Ligi ya Algeria unaweza usikute timu itakayofika Nusu fainali CAF champs, lakini as collectively timu zake ziko na weights za maana sana.

Kuna MC Alger, USM Algiers, CS Constantine, CR belouzdad, JS kabylie, JS Soura, ES setif, hizi timu Saba nilizozitaja hapo juu zikiamua msimu huu tunataka matokeo na tunataka kushindana wanao uwezo wa kuja kuchukua key player yyte hapa TZ hata Kwa bilioni moja ya kitanzania, hakuna mchezaji anayejitambua tena umri mdogo mwenye malengo anayependa kukua kimpira na kiushindani asivutiwe na kucheza Ligi kuu za Egypt, morroco, Algeria na Tunisia Kwa case ya hapa kwetu Afrika
 
Kaanza na kushindwa mechi ni mkosi mkubwa na labda ataendelea kushindwa huko, mtu akiondoka mahali husema ahsante sio kuponda. Yanga ni platform ambayo pia imemsogeza mbele aache kuropoka
 
Huyu mropofu bora tu aliondoka. Kwanza mashabiki wengi wa Yanga tulikuwa hata hatumkubali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…