Kwa kweli matrafiki ni wengi sana barabarani. Hawatoi elimu kuhusu matumizi ya barabara, lugha yao ni kupiga faini tu.
Inachosha kwa kweli.
Nimewahi kufanya safari ya usiku sikuona traffic hata mmoja. Lakini nilifika salama.
Lakini mchana ni balaa. Mfano wanasimama na camera yao kwenye kibao cha 50. Wanataka ukifika kibao hicho uwe 50 net.
Mfano nikiwa spidi 130 nikaona kibao cha 50 kweli inawezekana kushusha spidi kutoka 130 hadi 50 ndani ya mita 30 baada ya kuona kibao?
Si bora wakae mita 50 kutoka kwenye kibao ili kutoa nafasi kwa dreva ya kushusha spidi bila kushika breki kwa nguvu?
Inachosha sana.