Safari ya gari Cape Town, Afrika Kusini mpaka Dar es Salaam, Tanzania

Safari ya gari Cape Town, Afrika Kusini mpaka Dar es Salaam, Tanzania

Armani William

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2014
Posts
248
Reaction score
744
Wakuu, mwaka huu mwishoni nimepanga kufanya safari kuendesha hiyo ndinga kwenye picha kutoka Cape Town South Africa mpaka Dar es Salaam Tanzania karibia Kilomita 5,000.

Kuna yeyote yaliyewahi fanya safari ya namna hiyo, nipate mawili matatu ya barabara na usalama.
SAVE_20220816_202101.jpg
 
Wakuu, mwaka huu mwishoni nimepanga kufanya safari kuendesha hiyo ndinga kwenye picha kutoka Cape Town South Africa mpaka Dar Es Salaam Tanzania karibia Kilomita 5,000.

Kuna yeyote yaliyewahi fanya safari ya namna hiyo, nipate mawili matatu ya barabara na usalama.View attachment 2325827
Hii ni picha umedownload, ila hata ingekuwa ni bajaj haiongezi wala kupunguza millage.

Cape town mpaka Dar ni zaidi ya kilometer 5000 inategemea unapitia njia gani, kuna njia zaidi ya tatu.

Ukipitia Johannesburg maana yake mpaka Dar si chini ya kilometer 6000. Pili kuna vitu vya kuzingatia kibali cha interpol na border ya kuingia Tanzania ili gari iingie kwa kulipia transit tu ni lazima gari iingizwe na mgeni yani siyo Mtanzania kwamba anakuja kutembea, sidhani kama utaratibu umebadirika, ila kama upo vizuri ujiandae kulipa ushuru wa hiyo gari border kama unaingia nayo mwenyewe kwa passport ya Tanzania, kitu ambacho najuwa hiyo gari utaiacha tu border na kupanda basi kwenda Dar na huenda hiyo gari ukaiuzia hapohapo border. Unawajuwa TRA?

Nimekufumbuwa macho kidogo, wajuzi watakueleza zaidi.
 
Nimeendesha mara tatu kutokea Cape Stad huwa tunapita Namibia,Zambia,Tanzania ukipita kuitafuta Pretoria Kilomita ni nyingi sana kutoka Cape Town mpaka Johanesburg ni 1500Km kwa usafiri wa bus likitoka leo asubuhi linafika tena kesho asubuhi Johanesburg.

Kuingia Namibia utapitia mpaka wa Sesheke kuingia Zambia unakua umefika Living stone hapo mpaka Lusaka ni kama mia sita naa Km na Lusaka mpaka Nakonde ni 1100Km sema gari nyingi zipo Johannesburg kuliko huko Cape Town na pia kutoka Jozi sio mbali kuja Tanzania ila pia Cape pana gari nyingi bei nafuu kuliko Gauteng Province shida ni huo umbali.
 
Vipi usalama barabarani? Je Namibia na Zambia wanaruhusu kusafiri usiku?
Usalama Namibia na Zambia upo wa kutosha kwa Zambia jambazi wa magari au watekaji wanapotezwa na kikosi maalumu kipo kwa ajili hiyo miaka ya nyuma kidogo maeneo ya Mkushi palikua na utekaji nadhani walikua wanatokea Congo Drc wale walipotezwa wote..

SA ndio usalama wa mashaka na Zimbabwe usiku huwa wanachimba bara bara ili magari yapate ajali wao wachukue vitakavyokuwepo...
 
Mkuu vipi kuhusu malipo wakati unaingia Tz?
Nchi za Sadc kodi ipo nafuu kwa bidhaa zinatoka ukanda wao ila hiyo gari utakayonunua SA iwe made ya SA na unapata karatasi za export kutoka wizara yao ya Export and trade ipo Sunyside jengo la Mandela bure ila uwe na document zote za Interpol na wao ndio wanakuuliza utapitia mpaka upi ili likitoka hiyo namba inafutwa SA na hata Interpol wakija Tanzania hawawezi kukusumbua kwa sababu gari ishafutwa kwao muda mwingine wanakamata gari ambazo hazijafutwa SA ila sio za wizi..ukifata utaratibu hauwezi kusumbuliwa miaka nenda rudi...
 
Back
Top Bottom