Hii ni picha umedownload, ila hata ingekuwa ni bajaj haiongezi wala kupunguza millage.
Cape town mpaka Dar ni zaidi ya kilometer 5000 inategemea unapitia njia gani, kuna njia zaidi ya tatu.
Ukipitia Johannesburg maana yake mpaka Dar si chini ya kilometer 6000. Pili kuna vitu vya kuzingatia kibali cha interpol na border ya kuingia Tanzania ili gari iingie kwa kulipia transit tu ni lazima gari iingizwe na mgeni yani siyo Mtanzania kwamba anakuja kutembea, sidhani kama utaratibu umebadirika, ila kama upo vizuri ujiandae kulipa ushuru wa hiyo gari border kama unaingia nayo mwenyewe kwa passport ya Tanzania, kitu ambacho najuwa hiyo gari utaiacha tu border na kupanda basi kwenda Dar na huenda hiyo gari ukaiuzia hapohapo border. Unawajuwa TRA?
Nimekufumbuwa macho kidogo, wajuzi watakueleza zaidi.