Safari ya gari Cape Town, Afrika Kusini mpaka Dar es Salaam, Tanzania

Safari ya gari Cape Town, Afrika Kusini mpaka Dar es Salaam, Tanzania

Ahadi hii huwa hutimizi mkuu
Mkuu nachotaka kufanya hasa ya trekta niende ule mtaa wanaouza hayo hapo Pretoria ni kupata namba zao na Location sasa muda ndio inakua tatizo kidogo ila wengi nawapa location wakitaka kuja na wamefanikiwa bila hata ya kuonana na mimi..
 
Ilirudi SA maana hawawezi kuchukua na kuuza gari yenye umiliki wa mtu mwingine ilirudi SA naifahamu hiyo gari ni wasanii wawili imewatokea hiyo ishu..sema vijana ni kama waliwakopa wale wasanii kwa kuwapa gari ambazo ilikua ngumu kwa wasanii kuzilipia kodi wakijua zitarudi tuu nyumbani...
Mimi nimekupa utaratibu wa kisheria ila naona wewe umeleta mazoea ya miaka 20 kwaio siku jambo hilo likikukuta usishangae kabisa mzee...hayo magari yenye namba za kigeni yamekua yamoto DSM...
Watafute wa kuwafundisha sikumbuki idadi ya gari nilizoleta na pia mimi ni mhasibu sidhani kama pana kitu kipya ntapata kutoka kwako kwa ishu za sheria za kodi iwe Tanzania au SA...
Basi sawa hakiharibiki kitu...😀😀😀
 
Vipi usalama barabarani? Je Namibia na Zambia wanaruhusu kusafiri usiku?
Namibia unasafiri full time , na barabara zao zipo very well posted kupata maja ga ni ngumu sana
Sio kama barabara ya lindi masasi , mchana unapita safi kabisa usiku unakuta pamechimbwa msingi wa kukata barabara , kibao cha diversion kimechorwa na peni.
 
View attachment 2325911
View attachment 2325912
View attachment 2325913
Was among the best experience through Zambia,Zimbabwe then South kuwa makini ukivuka Britbridge usilale Mesina kuna wazimbabwe wakatili sana
Njia hiyo ya beitbridge niliacha kupita miaka mingi sana
Beitbridege ni boarder ambayo madawa ta kulevya yanapita sana , kuna check point nyingi sana hadi unafika polokwane unaweza pata usumbufu wa kusimamishwa simamishwa .
Mabasi ya abiria mengi yanapita hapo yakitokea harare lusaka na bulawayo,bulawayo kuna shida ya illigal immigrants na wengi wa uoande huo ndo wezi wezi , hivyo kuna checkpoints nyingi pia za watu wa uhamiaji
Ningekuwa mimi ningepita lusaka livingstone kazungura boarder francis town gabarone unakuja kutokea uwani mwa jo burg.. anyway good experience
 
Mkuu nachotaka kufanya hasa ya trekta niende ule mtaa wanaouza hayo hapo Pretoria ni kupata namba zao na Location sasa muda ndio inakua tatizo kidogo ila wengi nawapa location wakitaka kuja na wamefanikiwa bila hata ya kuonana na mimi..
Usikate tamaa mkuu nakumbuka hata mimi ulinipa maelekezo wapi na lini pa kununua Discovery 4.
Sasa anzisha uzi
 
Njia hiyo ya beitbridge niliacha kupita miaka mingi sana
Beitbridege ni boarder ambayo madawa ta kulevya yanapita sana , kuna check point nyingi sana hadi unafika polokwane unaweza pata usumbufu wa kusimamishwa simamishwa .
Mabasi ya abiria mengi yanapita hapo yakitokea harare lusaka na bulawayo,bulawayo kuna shida ya illigal immigrants na wengi wa uoande huo ndo wezi wezi , hivyo kuna checkpoints nyingi pia za watu wa uhamiaji
Ningekuwa mimi ningepita lusaka livingstone kazungura boarder francis town gabarone unakuja kutokea uwani mwa jo burg.. anyway good experience
Umesafiri siku ngapi kati ya Cape town to Dar kupitia Gaborone?
Bei ya gari kama Ist (old model) huko Cape town bei gani show room?
 
Wakuu vp experience ya basi ya abiria kutoka Cape town kuja Tanzania, nauli imekaaje na uchukuwa siku ngap

na kama kuna details zinazohitajika zaid ya Passport, ningependa ufafanuzi kwa anayefaham
Cape Town ni hakuna gari ya moja kwa moja kutoka TZ, utachua bas kutoka TZ mpaka Zambia, kisha Basi lingine kutoka Zambia mpaka Pretoria au Joburg kupitia Zimbabwe ni rahisi kidogo, then ukifika hapo ndipo utanyanyuka na Basi nyingine kwenda Cape town.

Ningekushauri upande treni kwa unafuu ingawa utachelewa kuliko Basi. Cape town ni mbali sana ukitokea hapa tz nahisi ni 5000+ km.

Nauli kutoka TZ hadi Joburg haizidi 230000 ila jitahidi kuweka akiba ya pesa maana safari ni safari, na safarini kuna mengi mno.
 
Ukifika MPIKA, kunja kushoto, moja kwa moja hadi Mbala, vukia border ya Zombe / Kisesya Utatokea SUMBAWANGA.

Utakuja kunishukuru.
Yes ni njia imetulia na haina usumbufu sana hasa pale border, wazo zuri sana hili kuliko pale Mpika unaonyosha hadi chinsali, tunduma border kuna urasimu sana pale wa kukatisha tamaa kabisa
 
Wakuu, mwaka huu mwishoni nimepanga kufanya safari kuendesha hiyo ndinga kwenye picha kutoka Cape Town South Africa mpaka Dar es Salaam Tanzania karibia Kilomita 5,000.

Kuna yeyote yaliyewahi fanya safari ya namna hiyo, nipate mawili matatu ya barabara na usalama.
View attachment 2325827
anyways ni kama kwenda Dar-mwanza mara tano. 😁, kwahiyo jipange na kila na kheli blaza
 
Wakuu vp experience ya basi ya abiria kutoka Cape town kuja Tanzania, nauli imekaaje na uchukuwa siku ngap

na kama kuna details zinazohitajika zaid ya Passport, ningependa ufafanuzi kwa anayefaham
Kuna trans lux na Greyhound, check online au nenda ofisi zao Mother City.
 
Ilirudi SA maana hawawezi kuchukua na kuuza gari yenye umiliki wa mtu mwingine ilirudi SA naifahamu hiyo gari ni wasanii wawili imewatokea hiyo ishu..sema vijana ni kama waliwakopa wale wasanii kwa kuwapa gari ambazo ilikua ngumu kwa wasanii kuzilipia kodi wakijua zitarudi tuu nyumbani...
Nimeona Kajala naye amehongwa Range ina namba za Gauteng Province, nadhani ndio walewale.
 
Umesafiri siku ngapi kati ya Cape town to Dar kupitia Gaborone?
Bei ya gari kama Ist (old model) huko Cape town bei gani show room?
Kwanza unapaswa kujuwa South Africa system yao magari ya kutoka Japan wanayapiga ushuru kisawasawa, sababu wao wanatengeneza magari, unafuu wa magari South Africa ni kwa magari wanayotengeza wao.
 
Back
Top Bottom