Safari ya kujitafuta 2025 inaanzia hapa! Hisa 129,700 za CRDB, NICOL 3864, UTT 400k safari inaendelea

Safari ya kujitafuta 2025 inaanzia hapa! Hisa 129,700 za CRDB, NICOL 3864, UTT 400k safari inaendelea

Wakuu,

Mwezi january ndo huo unapamba moto, baada ya mapambano makali ya mwaka jana na bata la desemba, sasa narudi ulimwengu wa vita ni vita Mura. Kifupi liwalo na liwe nikipata nipate, nikikosa nikose.

Kifupi mshahara wangu ni 1000k+ as take home. Kwanzia mwezi huu huwa nina tabia ya kusave 700k each month. Na kazini kwetu kuna marupurupu kidogo kwa mwezi hukosi 200k au 300k mbali na mipigo mingine.

Wife nimemfungulia biashara wa wakala wa pesa mitandao ie Mpesa, CRDB etc lengo ni kupunguza ugumu wa maisha huku tukiendelea kujitafuta na biashara inaenda vizuri hatukosi hela ya mboga na mahitaji madogo madogo.

Dhamira mwaka huu ni kukusanya 40ml mbali na savings zangu za awali nilizo zitaja.

Committiments ni kwamba;

-Nafunga kunywa bia from now to Nov mpaka kieleweke
  • Kuhusu misosi nitapendelea kula nyumbani na familia.
  • Sitoki out kula bata bora nipunguze marafiki coz familia ikinipenda inatosha
  • Kuendeleza miradi ya ufugaji hapa nyumbani kwangu ie kuku, bata etc kupunguza makali ya maisha. (Extra time after job hours)

Bata litafunguliwa Nov mwishoni baada ya malengo kukaa sawa😂😂😂
Tukutane DEC mwaka huu kwa mrejesho.
Keep it up bro,
You can make it happen....!!🔥🔥

No one can stop yr dream, unless you want to...
 
Kuendeleza miradi ya ufugaji hapa nyumbani kwangu ie kuku, bata etc kupunguza makali ya maisha. (Extra time after job hours)
Hongera mkuu! Kama uko Dar hii miradi yako utatusua! Dar wanakula vifaranga na wanavigombania!
 
Lakini amesema kazini kwake kuna marupurupu yanayofikia 200-300k kwa mwezi na mipango mingine. Sasa hapo kwenye mipango mingine ndipo penye kipato sasa!
Ni ngumu sana kisevu 700,000/- kwa kipato cha 1.2m
Fanya hivi
-nyumbani matumizi kwa mwezi 300,000/- chukua Laki3 toa ile 1.2m utabaki na laki9, hapo sijaweka Kula kazini (mchana na asubuhi), Nauli za kwenda kazini, Vocha, maji, umeme, gasi/mkaa, kuvaa, kin'gamuzi,
- Milioni40 kuipata labda ujiingize kwenye magendo kwa sababu kipato chako kwa mwaka ni hakizidi 15.6M
 
Lakini amesema kazini kwake kuna marupurupu yanayofikia 200-300k kwa mwezi na mipango mingine. Sasa hapo kwenye mipango mingine ndipo penye kipato sasa!
Labda pengine hayo madili ya magumashi, lakini posho za 300,000/ na salary ya 1M sio nyingi sana kiasi cha kuweza kusevu 700,000/-
 
Wakuu,

Mwezi january ndo huo unapamba moto, baada ya mapambano makali ya mwaka jana na bata la desemba, sasa narudi ulimwengu wa vita ni vita Mura. Kifupi liwalo na liwe nikipata nipate, nikikosa nikose.

Kifupi mshahara wangu ni 1000k+ as take home. Kwanzia mwezi huu huwa nina tabia ya kusave 700k each month. Na kazini kwetu kuna marupurupu kidogo kwa mwezi hukosi 200k au 300k mbali na mipigo mingine.

Wife nimemfungulia biashara wa wakala wa pesa mitandao ie Mpesa, CRDB etc lengo ni kupunguza ugumu wa maisha huku tukiendelea kujitafuta na biashara inaenda vizuri hatukosi hela ya mboga na mahitaji madogo madogo.

Dhamira mwaka huu ni kukusanya 40ml mbali na savings zangu za awali nilizo zitaja.

Committiments ni kwamba;

-Nafunga kunywa bia from now to Nov mpaka kieleweke
  • Kuhusu misosi nitapendelea kula nyumbani na familia.
  • Sitoki out kula bata bora nipunguze marafiki coz familia ikinipenda inatosha
  • Kuendeleza miradi ya ufugaji hapa nyumbani kwangu ie kuku, bata etc kupunguza makali ya maisha. (Extra time after job hours)

Bata litafunguliwa Nov mwishoni baada ya malengo kukaa sawa😂😂😂
Tukutane DEC mwaka huu kwa mrejesho.
Nipo kwenye Bus lako, tunatofautiana tu figure ulizoweka, na tunatofautiana miezi ya kula bata. Mimi nakula bata kuanzia 20th December hadi 30th December ya kila mwaka. Na lazima nitoke na familia yangu twende popote nje ya Dsm tukodishe eco homes kwa hizo siku, na ndo kipindi ninachofungulia koo, yaani bia na marafiki sijali hata itumike 500k au 1m kwa siku, hizo siku 10 nazitendea kazi kwakweli, 29th December tunarejea Dar na 30th December namalizia bia za mwisho na marafiki na majirani wa Dar,.kisha 31st December sinusi tena pombe, saa 2 usiku nazima simu na saa 3 kamili nalala, naamka saa 11 alfajiri na ratiba ya siku inaanza kwa jogging for 1hr.

Dear bia na marafiki tutakutana tena December 20th this year 2025
Usijitese sana, maisha ya mwanadamu yana mwanzo na yana mwisho. Kula ni muhimu, kuvaa ni muhimu, matibabu ni muhimu, pia kufurai/kula bata ni muhimu; cha kufanya ni kuimarisha vyanzo vyako vya kifedha viweze kukupatia hizo huduma.

Utajitesa leo, kesho unapinduka na gari; wakulungwa wanatumia hela zako bila huruma.

Muhimu tujue kuna kuishi pia, na tunaishi mara moja tu. Usiwalishe watoto mboga isiyokuwa na mafuta kwa sababu ya kujenga.​
Kuacha kunywa bia sio kujitesa ni kuimarisha afya yako ambayo ni muhimu kuliko bia, tafsili ya wengi yakutokula bata wanaona nikujitesa. Kula mboga zenye mafuta nikuutesa mwili, afya yako na ya familia yako ni muhimu kuliko kula vile mnavyoita vizuri au kunywa bia.
 
Back
Top Bottom