Safari ya kuusafirisha mwili wa Mtanzania Nemes Tarimo kutoka Urusi hadi Tanzania inaanza 24 Januari, 2023

Safari ya kuusafirisha mwili wa Mtanzania Nemes Tarimo kutoka Urusi hadi Tanzania inaanza 24 Januari, 2023

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Taarifa za uhakika kutoka ndani ya Familia ya Mtanzania Nemes Raymond Tarimo (34) ambaye alifariki wakati akipigana upande wa Jeshi binafsi la Urusi la Wagner Group dhidi ya Ukraine, zinaeleza kuwa safari ya kuurejesha mwili wake Nchini Tanzania inatarajiwa kuanza kesho Jumanne Januari 24, 2023.

Muda wa kuwasili Tanzania bado haujawekwa wazi lakini taratibu za kuupokea zimeshafanyika ambapo ndugu, jamaa na marafiki wanasubiri ratiba kamili juu ya muda wa kuwasili kutoka Urusi.

Tarimo.jpg

Pia soma: Tarimo Nemes, anayedaiwa alifariki akiwa vitani Ukraine, aligombea Ubunge

Mtanzania Tarimo Nemes Raymond, afariki akiwapigania Wagner wa Urusi, kule Ukraine
 
Is there a direct communication between PMC Wagner Group and the family or Ubalozi?

Na kuhusu gharama za kusafirisha ni wao Wagner wametoa ama ni nani?

Na kuna "Fidia" yoyote familia itapata baada ya kifo cha askari?
 
Is there a direct communication between PMC Wagner Group and the family or Ubalozi ?
Na kuhusu gharama za kusafirisha ni wao Wagner wametoa ama ni nani ?
Na kuna "Fidia" yoyote familia itapata baada ya kifo cha askari ?

Serikali ya Urusi inalipa fidia inayokadiriwa dola 30000 hiyo ni mkono wa pole nje ya gharama zote za kusafirisha mwili na kuna mwakilishi atakuja na mwili
 
Tangulia mpambanaji....
Hata mm nitajilipua tu niupige vita umasikini. Umasikini ni mbaya aseee
Na asikwambie mtu hela ina attract hela
Unataka kwenda vitani nikuunganishe au unajiripua kwa njia tofauti?
 
Alikuwa well trained na kupitia mafunzo ya vyuo mbalimbali vya kijeshi hata south africa so usimchukulie poa
mzee hakuna cha treiningi wala nn hao walikua wanawekwa frontline afu mafunzo yenyew n ya week1 una tegemea nn ume sahau ya mobilization ambapo mpaka walev wa kirus walikua wana pewa mafunzo kwa week 1 kisha wana pelekwa frontline
 
Huyo ni mpambanaji na historia imeandikwa, hapa wanaoponda wengi wetu tunapata viazi nyumbani kwetu
Jamaa ana spirit kama ya wa West Africa. Alijua akifanikiwa akitoboa ndo basi mpunga wake angeish vizuri siku zake zilizobaki duniani sema ndo hvyo imekuwa bahati mbya. Alikufa kijeshi Na ndo maana wamemuaga kijeshi.
Hajafa kizembe....
Watanzania waoga sana.
 
Kwa akili yako unadhani miaka saba urusi alikua bado anasoma tu?
Hizo ni akili zako za kufikirika lakini uhalisia ni kwamba huwa wanapelekwa front line bila mafunzo yeyote mfano mzuri na wale mobilizations
 
Back
Top Bottom