Safari ya Lissu kuelekea Nairobi ilikuwa ni mateso na vilio, Spika Ndugai usitoneshe vidonda

Kuna watu humu nimeona nao wanachangia kwa upotoshaji,akiwemo mtu anaitwa Tume ya Katiba juu ya namna Lissu alivyotoka Tanzania kwenda Nairobi.

Kwanza naomba ku-declare kuwa nilishiriki "indirectly" kuona namna gani usafiri wa kwenda Nairobi unapatikana,japo nilikuwa mbali na nyumbani,lakini niliwasiliana na wadau ili kuona huyu mtu anapata usafiri kufika eneo la matibabu baada ya kusikia uhitaji mkubwa ni kufika Nairobi usiku uleule.

Suala la kwanza lilioafikiwa na Bunge ilikuwa ni kumleta Dsm-Muhimbili,ndege iliyokodiwa ilikuwa ni ya kampuni ya Safari Air Link na si ya NHIF kama anavyosema huyo Ndugai,ambayo ni MEDEVAC,ilikuwa ni Caravan usajili wa 5H-EWA,mali ya Peter Fox(mmiliki wa kampuni ya Safari Air Link),bahati mbaya ikatokea mabadiliko ya kwenda Nairobi,na ile ndege ikawa na rubani mmoja na haiwezi kwenda Nairobi usiku ikiwa na rubani mmoja ambaye hakuwa na masaa ya kuruka usiku.TCAA walikuwa tayari kutoa kibali cha ndege kuruka usiku hata kama ina injini moja kwa sharti la kuwa na marubani wawili,Ukawa ni mtihani mwingine wa kuanza kutafuta ndege nyingine usiku uleule.

Ndege nyingine ya Safari Air Link aina ya Citation(Jet Engines) siku hiyo ilikuwa imeenda Pemba ya Mozambique kama si Zambia,Fox akawa hana option,sbb pia hiyo ndege isingeweza kubeba abiria wengi ambao CHADEMA walikusudia wasafiri na Lissu.

Ndege kubwa ya kuwatosha mgojwa,daktari pamoja na wasindikizaji akiwemo mkewe, ikawa ni hiyo Citation ya Flight Link,5H-ETG.Ambayo ilipaswa kutoka Dsm kuja Dodoma usiku uleule,ili inyanyuke kwenda Nairobi.

Jambo hili likawezekana,lakini ilipaswa pesa iwe juu ya meza kwa mlipo ya dola,Dodoma hakukuwa na Mbunge wala waziri mwenye dhamana ya dola,Turky wa Mpendae akachukua dhamana hiyo ya mali kauli,sababu mmiliki wa kampuni ya Flight-Link(Mhindi) wana ushirika naye.Ndege ilinyanyuka Dsm-Dodoma na baadae Nairobi

Siri ya safari ile wakiwa angani,naamini ipo siku Mbowe na Msigwa wataiandikia kitabu(A Day to Remember in a Dark Political Arena),Ilikuwa ni safari ngumu iliyojaa machozi na uchungu mkubwa,walisafiri kwa shida sana,kitanda kilikuwa kinacheza na pia dripu ilibidi Dokta asafiri akiwa ameishika mkononi kaining'iniza juu sababu ya "height" ya ndege,ilikuwa ni safari ya mateso na experience mbaya sana kwa kina Msigwa na Mbowe pamoja na mke wa Lissu.Mungu aliyemponya Danieli katikati ya Simba wenye njaa,alitenda miujiza.

Sijaelewa huu upotoshaji wa huyu Ndugai ameutoa wapi,kwamba kuna ndege ilikodiwa toka Nairobi?Hiyo ndege ni ipi?kwamba aliomba itumie "airspace" ya Tanzania kinyume na sheria za nchi?Kwani sheria za nchi zinavunjwaje kwa ndege iliyoomba kibali kutua Tanzania na ikaruhusiwa?

Huu uwongo ni wa nini?hiyo ndege mliyokodi toka Kenya ni ipi?Maana kila mtu hata siyekuwa Dodoma aliona ndege iliyoondoka na Lissu ni 5H-ETG mali ya kampuni ya FlightLink.

Hii ni kampuni ya Tanzania,ndio maana usajili wa ndege umeanza na "5H",ndege zote zilizosajiliwa Tanzania huanza na "5H",zile za Kenya huanza na "5Y" na majirani Uganda ni "5X"...Wewe Ndugai hiyo ndege ya Kenya mliyoiombea kibali cha kutumia "airspace" yetu tena kinyume cha sheria ni ipi?Na sheria zipi mlizovunja?

Sasa unaona mtu anakuja humu anasema eti Lissu alitoka na ndege Dodoma hadi Dsm then ndio akaenda Nairobi.Huu uwongo mnauzalisha toka wapi??Wacheni upumbavu katika uhai na maisha ya watu sbb ya siasa!!Eboooo!!!!

Nimemsikiliza Ndugai hapa Jf kwenye video,ameongea kwa uchungu na huzuni,sababu maneno ya Lema yamemuingia sana,amefikia hatua ya kusema kama CHADEMA wanataka kumpeleka Lissu India,bunge lipo tayari endapo Waziri atakubali.Maneno ya Lema yamegusa mfupa,Job anajua aliondoka na hali gani hapa nyumbani kwenda India,amekaa miezi kibao akiugua.

Kila aliyekuwa anasimama bungeni,kabla ya kuchangia,alimuombea Spika afya njema na arudi mzima nyumbani.Watu walisali...Kuna siku Bulaya aliongoza sala ya kuomba afya ya spika katika Canteen ya Bunge.

Malumbano yanayoanzishwa na Spika ndani ya bunge juu ya afya ya Lissu si afya kwa ubinadamu na utu.Kuanzia lile la kutofautiana idadi ya risasi na Kubenea mpaka kamati ya maadili,na lile la kusema Turky ndio kachangia.Turky ni muislam safi,sadaka isiyo na mawaa na yenye thawabu haitangazwi.

Palipo na tendo jema,Mungu hufungua riziki...Kuitangaza sadaka ya Turky bungeni ni kumuondolea neema na thawabu kubwakubwa na ndogondogo mja wake aliyetoa sadaka.Mh.Spika,tumia busara kufunga malumbano ya afya ya Lissu Bungeni,wakati upo India,watu walijibiidisha kukuombea na si kujadili na kulumbana juu ya afya yako na matibabu yako.FUNGA MJADALA WA KUSIMANGANA BUNGENI KUHUSU AFYA NA HALI YA TUNDU LISSU...HUU SI UBINADAMU.

Kuna kijana sijui ni msemaji wa chama naye katoka kabisa na "Press Release" kupongeza hali ya Mbunge Turky,kutoa "mali kauli" ya safari ya ndege.Jamani mnaharibu sadaka za wenzenu.Turky mwenyewe amenukuliwa akisema;
" Mbowe akaniomba kwa kuwa nafahamiana nao (wenye ndege) niwadhamini wamuwahishe Lissu halafu wao watalipa. Na ndicho nilichofanya (kuwadhamini kwa mali kauli) na pesa hiyo imelipwa jana. Tunamshukuru Mungu nia njema hufungua milango yake” .Watu mnaharibu sadaka za watu bila kujua,nia njema ya Turky ipo katika hayo maneno yake ya mwisho yenye "bold".

Msaidieni Lissu kama nyie mlivyosaidiwa kwa kofia za ubunge na uspika wenu,wacheni masimango,tendeni kama vile mlivyotendewa,wengine mlikwenda India miguu haingii hata katika viatu,mlivaa suti na sandozi.Mungu amewaponya...Lipeni wema juu ya wema!!Mnaleta "urasimu" wa taratibu za matibabu nje ya nchi kwa mwili wa binadamu uliopigwa na kulowa risasi zaidi ya 10?Ebooo!!HIZO PESA ZA MAMA ZENU?

barafu wa JF

We Live Once,but Legacy Lives forever!!
View attachment 588456
Juu ni ndege ya kampuni ya FlightLink(Tanzania) iliyompeleka Lissu Nairobi

View attachment 588458
Hii ni ndege ya Safari Air Link iliyokusudiwa kumleta Dsm ikashindikana
Wewe ndiyo umeharibu kabisa na umeegemea upande mmoja umeshatoa hukumu unataka tujadili au tukuunge mkono?, Kwanza hujatueleza haya mateso makubwaa waliyoyapata wakiwa safarini kwenye ndege ni yapi, mgonjwa alisindikizwa na nurse pamoja na daktari toka Dodoma, ambao waliwajibika nw hayo mambo yote yanayohusiana na kucheza kwa kitanda na kushikilia hizo drip za damu, hao wengine wwlitesekaje?, lakini hataka kama walisaidia kuzuia kitanda, ndege inamtikisiko mkubwa kiasi gani cha kutaka kutuaminisha kwamba waliteseka sana kiasi hicho?

Kuhusu kauli ya Job Ndugai kusema kulikua na ndege ya NHIF, alimaanisha ndege iliyokodiwa na bima ya NHIF, ambayo ndiyo bima yenye jukumu la kuwatibia wabunge wote kisheria, hakumaanisha hiyo ndege ni ya NHIF, jaribu kutumia akili, mapenzi yakizidi sana hupoteza busara, punguza mapenzi.

Job Ndugai amelazimka kuyasema hayo baada ya Lema kutuma shutuma akiwa huko Nairobi akizielekeza kwa Ndugai kwamba hajafanya lolote katika kumsaidia Lisu, ilibidi aeleze yale yaliyofanyika ndipo amemtaja aliyetoa dhamana ya hiyo ndege, kama ni kulaumiwa ni Lema, hii habari ya kutomtaja Turky kwa sababu alitoa sadaka, sio kweli, hakutoa sadaka alidhamini na pesa yake imerudishwa

Wabunge wote wana bima ya afya, na kila bima ya afya inataratibu zake, wote waliokwenda kutibiwa walifuata hizo taratibu hatimaye wameenda kutibiwa India, akiwemo Mbatia, kwanini Lisu asitumie bima yake matokeo yake mnaanza kutupa lawama zisizokua na maana yoyote?, kwanini kule Nairobi wamebaki wasindikizaji wengi ambao wanaongeza gharama za matibabu, kama wanatumia pesa zao, kwanini wasirudi na hizo pesa wakamwachia mgonjwa?, ama kweli akili ni nywele.
 
Joto ya jiwe nawe unachemsha, km huwezi kuusoma uzi ni bora usipost chochote, NHIF ni wapi walileta ndege Dodoma? umeoneshwa ma picha kandege kalikuwa huko Dar na hakana marubani, pili huyo Turky hajarudishiwa yeye pesa kwani alitoa? hayoaluweluwe ya ndani ya ndege barafu hakuwepo wewe unachomuuliza atajibuje wakati ameelezea uzoefu wa angani na aliyoyanasa, kumlaumu Lema kuwa Agha Khan Nairobi ni hela yake hata Msigwa na Mbowe, kaa chini jiulize Tanzania tumefikia kutumia silaha za kijeshi kwenye siasa? na sio uendeleze malumbano

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shukrani mkuu barafu kwa maelezo yako yenye vithibitisho vya kutosha!

Nimekuwa nasema humu kwa muda sasa kuwa huyo Ndugai siamini kama yupo mzima maana tangu aumwe ubongo wake umezidi kwenda fyongo! Kwa jinsi alivyoumwa na kuteseka na ule ugonjwa nilitegemea angerudi akiwa mtu tofauti sana!...kumbe nilikosea. Lakini huyu Mungu wa Danieli na wenziwe akina Meshack & Abednego yu HAI..!! Hatoacha tenda makuu milele!
 
Boss barafu Bandiko lako nimenitoa machozi aisee. So sad. Karma is the BITCH !!!

Kuna watu humu nimeona nao wanachangia kwa upotoshaji,akiwemo mtu anaitwa Tume ya Katiba juu ya namna Lissu alivyotoka Tanzania kwenda Nairobi.

Kwanza naomba ku-declare kuwa nilishiriki "indirectly" kuona namna gani usafiri wa kwenda Nairobi unapatikana,japo nilikuwa mbali na nyumbani,lakini niliwasiliana na wadau ili kuona huyu mtu anapata usafiri kufika eneo la matibabu baada ya kusikia uhitaji mkubwa ni kufika Nairobi usiku uleule.

Suala la kwanza lilioafikiwa na Bunge ilikuwa ni kumleta Dsm-Muhimbili,ndege iliyokodiwa ilikuwa ni ya kampuni ya Safari Air Link na si ya NHIF kama anavyosema huyo Ndugai,ambayo ni MEDEVAC,ilikuwa ni Caravan usajili wa 5H-EWA,mali ya Peter Fox(mmiliki wa kampuni ya Safari Air Link),bahati mbaya ikatokea mabadiliko ya kwenda Nairobi,na ile ndege ikawa na rubani mmoja na haiwezi kwenda Nairobi usiku ikiwa na rubani mmoja ambaye hakuwa na masaa ya kuruka usiku.TCAA walikuwa tayari kutoa kibali cha ndege kuruka usiku hata kama ina injini moja kwa sharti la kuwa na marubani wawili,Ukawa ni mtihani mwingine wa kuanza kutafuta ndege nyingine usiku uleule.

Ndege nyingine ya Safari Air Link aina ya Citation(Jet Engines) siku hiyo ilikuwa imeenda Pemba ya Mozambique kama si Zambia,Fox akawa hana option,sbb pia hiyo ndege isingeweza kubeba abiria wengi ambao CHADEMA walikusudia wasafiri na Lissu.

Ndege kubwa ya kuwatosha mgojwa,daktari pamoja na wasindikizaji akiwemo mkewe, ikawa ni hiyo Citation ya Flight Link,5H-ETG.Ambayo ilipaswa kutoka Dsm kuja Dodoma usiku uleule,ili inyanyuke kwenda Nairobi.

Jambo hili likawezekana,lakini ilipaswa pesa iwe juu ya meza kwa mlipo ya dola,Dodoma hakukuwa na Mbunge wala waziri mwenye dhamana ya dola,Turky wa Mpendae akachukua dhamana hiyo ya mali kauli,sababu mmiliki wa kampuni ya Flight-Link(Mhindi) wana ushirika naye.Ndege ilinyanyuka Dsm-Dodoma na baadae Nairobi

Siri ya safari ile wakiwa angani,naamini ipo siku Mbowe na Msigwa wataiandikia kitabu(A Day to Remember in a Dark Political Arena),Ilikuwa ni safari ngumu iliyojaa machozi na uchungu mkubwa,walisafiri kwa shida sana,kitanda kilikuwa kinacheza na pia dripu ilibidi Dokta asafiri akiwa ameishika mkononi kaining'iniza juu sababu ya "height" ya ndege,ilikuwa ni safari ya mateso na experience mbaya sana kwa kina Msigwa na Mbowe pamoja na mke wa Lissu.Mungu aliyemponya Danieli katikati ya Simba wenye njaa,alitenda miujiza.

Sijaelewa huu upotoshaji wa huyu Ndugai ameutoa wapi,kwamba kuna ndege ilikodiwa toka Nairobi?Hiyo ndege ni ipi?kwamba aliomba itumie "airspace" ya Tanzania kinyume na sheria za nchi?Kwani sheria za nchi zinavunjwaje kwa ndege iliyoomba kibali kutua Tanzania na ikaruhusiwa?

Huu uwongo ni wa nini?hiyo ndege mliyokodi toka Kenya ni ipi?Maana kila mtu hata siyekuwa Dodoma aliona ndege iliyoondoka na Lissu ni 5H-ETG mali ya kampuni ya FlightLink.

Hii ni kampuni ya Tanzania,ndio maana usajili wa ndege umeanza na "5H",ndege zote zilizosajiliwa Tanzania huanza na "5H",zile za Kenya huanza na "5Y" na majirani Uganda ni "5X"...Wewe Ndugai hiyo ndege ya Kenya mliyoiombea kibali cha kutumia "airspace" yetu tena kinyume cha sheria ni ipi?Na sheria zipi mlizovunja?

Sasa unaona mtu anakuja humu anasema eti Lissu alitoka na ndege Dodoma hadi Dsm then ndio akaenda Nairobi.Huu uwongo mnauzalisha toka wapi??Wacheni upumbavu katika uhai na maisha ya watu sbb ya siasa!!Eboooo!!!!

Nimemsikiliza Ndugai hapa Jf kwenye video,ameongea kwa uchungu na huzuni,sababu maneno ya Lema yamemuingia sana,amefikia hatua ya kusema kama CHADEMA wanataka kumpeleka Lissu India,bunge lipo tayari endapo Waziri atakubali.Maneno ya Lema yamegusa mfupa,Job anajua aliondoka na hali gani hapa nyumbani kwenda India,amekaa miezi kibao akiugua.

Kila aliyekuwa anasimama bungeni,kabla ya kuchangia,alimuombea Spika afya njema na arudi mzima nyumbani.Watu walisali...Kuna siku Bulaya aliongoza sala ya kuomba afya ya spika katika Canteen ya Bunge.

Malumbano yanayoanzishwa na Spika ndani ya bunge juu ya afya ya Lissu si afya kwa ubinadamu na utu.Kuanzia lile la kutofautiana idadi ya risasi na Kubenea mpaka kamati ya maadili,na lile la kusema Turky ndio kachangia.Turky ni muislam safi,sadaka isiyo na mawaa na yenye thawabu haitangazwi.

Palipo na tendo jema,Mungu hufungua riziki...Kuitangaza sadaka ya Turky bungeni ni kumuondolea neema na thawabu kubwakubwa na ndogondogo mja wake aliyetoa sadaka.Mh.Spika,tumia busara kufunga malumbano ya afya ya Lissu Bungeni,wakati upo India,watu walijibiidisha kukuombea na si kujadili na kulumbana juu ya afya yako na matibabu yako.FUNGA MJADALA WA KUSIMANGANA BUNGENI KUHUSU AFYA NA HALI YA TUNDU LISSU...HUU SI UBINADAMU.

Kuna kijana sijui ni msemaji wa chama naye katoka kabisa na "Press Release" kupongeza hali ya Mbunge Turky,kutoa "mali kauli" ya safari ya ndege.Jamani mnaharibu sadaka za wenzenu.Turky mwenyewe amenukuliwa akisema;
" Mbowe akaniomba kwa kuwa nafahamiana nao (wenye ndege) niwadhamini wamuwahishe Lissu halafu wao watalipa. Na ndicho nilichofanya (kuwadhamini kwa mali kauli) na pesa hiyo imelipwa jana. Tunamshukuru Mungu nia njema hufungua milango yake” .Watu mnaharibu sadaka za watu bila kujua,nia njema ya Turky ipo katika hayo maneno yake ya mwisho yenye "bold".

Msaidieni Lissu kama nyie mlivyosaidiwa kwa kofia za ubunge na uspika wenu,wacheni masimango,tendeni kama vile mlivyotendewa,wengine mlikwenda India miguu haingii hata katika viatu,mlivaa suti na sandozi.Mungu amewaponya...Lipeni wema juu ya wema!!Mnaleta "urasimu" wa taratibu za matibabu nje ya nchi kwa mwili wa binadamu uliopigwa na kulowa risasi zaidi ya 10?Ebooo!!HIZO PESA ZA MAMA ZENU?

barafu wa JF

We Live Once,but Legacy Lives forever!!
View attachment 588456
Juu ni ndege ya kampuni ya FlightLink(Tanzania) iliyompeleka Lissu Nairobi

View attachment 588458
Hii ni ndege ya Safari Air Link iliyokusudiwa kumleta Dsm ikashindikana
 
Si sahihi kumkashifu kiongozi mkubwa kama Ndugai . Barafu uwe na hekima na busara, Tabia kama hizi ndio zimesababisha Lissu akakosa msaada wa pesa.
 
Malumbano wanaoanzisha ni chadema wenyewe..wakijibiwa wanaona wanaonewa..ndugai alielezea taifa wingi wa risasi alizopigwa lisu kwenye gari..kubenea akasema ndugai muongo..wakati kitendo tu cha kutaja wingi kule wa risasi ilibidi mumpongeze..maana angeweza pia kukaa kimya..kamsema zito bungeni..zito akagusia lisu..wakati lisu hausiki..Lema nae anamshutumu kuhusu lissu..
Sasa vitu mnaanzisha wenyewe..mkijibiwa mnasema malumbano..basi kaeni kimya uguzeni mgonjwa wenu..ila msidhani shughuli zitasimama kwa sababu ya ugonjwa au kifo cha lisu..hata vikao vya Acacia na timu ya magufuli havijasimama
Azungumze ukweli, siasa za chuki & dhihaka za nini kwa kiongozi kama yeye?!

Urasimu wa nini katika matibabu ya mtu aliyemiminiwa risasi kiasi kile?! Ukizingatia hadhi ya mgonjwa na mchango wake kwa taifa ?!. Hili liwe funzo la kwanini lazima iwe Apollo?! Kuna swala itikadi, uadui kama ilivyo tokea kwa Lissu , hawezi kulazimishwa tiba ktk hospital iliyojaa ajent wa maadui zake!!

MWISHO:
Hata msiposimamisha majadiliano na acaccia lakini hayana tija. Kama ulisikia vizuri ni majuzi tu, mkuu alilalamikia waliofunga mikataba ya kishenzi. hata ukiwazodoa cdm na mazungumzo ya acaccia lakini usitarajie makuu na kosa ni la serikali yenyewe na si chadema. Na shida ni mikataba.
 
Back
Top Bottom