Drifter
JF-Expert Member
- Jan 4, 2010
- 5,122
- 5,104
Mkuu Tindo you better reconsider. Hakuna binadamu anayemiliki kanisa. Ni Kristo peke yake ndiye mwenye kanisa lake. Usitarajie watumishi kuwa watakatifu, wakweli au waelewa kuliko wewe. Hivyo nenda kanisani kwako kaabudu katika roho na kweli na kupuuza (ignore) uzushi (heresy). It’s for your own spiritual health. The Good Lord needs your attention and you have to have His blessings.Ndio maana mimi nimeacha kabisa kwenda kanisani.
Mimi kwa mfano, kuna baadhi ya taratibu na mahubiri nisiyokubaliana nayo katika “kanisa” langu fulani ndani ya KKKT. Huwa nikipata fursa nje ya ibada au katika jumuia naweka mijadala na baadhi ya washirika, wachungaji na wazee kuwaonyesha kwamba baadhi ya vitu wanavyofanya au kuruhusu viko nje ya Neno au misingi ya ibada; havina support ya Neno (Biblia) tena vingine vinakiuka Neno lenyewe. Nashukuru tunaelewana kiasi kikubwa katika facts ingawa inaelekea TATIZO kubwa sana ni madhehebu kuwa kwenye “mashindano ya kidunia” kutaka kujitanua kwa idadi ya washirika, mapato na influence hasa kwa watawala.