mapipando
JF-Expert Member
- Jun 8, 2015
- 2,922
- 3,559
Nimezaliwa mwanzoni mwa miaka ya themanini katika hospitali ya Mwananyala iliyopo wilayani Kinondoni mkoani Dar es Salam.Mimi ni mtoto wa kwanza na pekee wa kiume kwa mama mwenye watoto 3.
Baada ya wazazi wangu kutofautiana waliachana na mama akaanzisha maisha yake Kurasini na baba akabaki Tandale (kwa Mtogole). Na wakati huo baba alikuwa anafanya kazi kituo cha mafuta pale karibu na kituo cha Polisi cha Msimbazi na mama yeye akaanza kuchoma vitumbua kwaajili ya kupata pesa za matumizi.
Mwishoni mwa mwaka 1991 mimi na mama tulienda kijijini (Singida) kusalimia na ulipofika wakati wa kurudi Dar mimi nilikataa kwakuwa nilivutiwa na mazingira ya kule hivyo mama akaniacha na 1992 nilianzishwa darasa la kwanza katika shule ya msingi Sekou-Toure na kuhitimu darasa la saba 1998.
Mwaka 1999 nilirudi Dar,kwani sikubahatika kuchaguliwa kwenda sekondari maana kipindi kile shule zilikuwa chache so katika darasa moja unakuta wanachaguliwa wanafunzi watatu ikizidi sana watano...katika darasa letu walichaguliwa watatu tu. Kutokana na mama kutokuwa na uwezo wa kunisomesha alinipeleka kwa baba,lakini mzee hakuthubutu kabisa kujali ama kuhangaika na 'future' yangu..na hata hivyo sikupata mapokezi mazuri ukizingatia nimetoka kijijini na wao walikuwa na maisha flani hivi ya kishua...baada ya muda mzee alinitimua nikarudi kwa mama.
Mwaka 2000 nikatengeneza toroli nikaanza kubeba mizigo kwani alipokuwa amepanga mama kulikuwa kuna biashara ya mbao,kuni,mabati madirisha (used) hivyo nikawa napata tenda za kusafirisha mizigo maeneo ya karibu na hata mbali kidogo mfano Temeke,Mtoni,Keko nk. Mambo hayakuwa mabaya kwani nilikuwa napata pesa za kusaidia familia na kiasi kingine nilihifadhi. Mwaka 2003 mwishoni nilienda Iringa nikiwa shilingi laki moja, na msimu wa 2004 nililima karanga,maharage na alizeti lakini matokeo hayakuwa mazuri hivyo sikuendelea na nikarudi tena Dar.
Mwaka 2005 mama aliwasiliana na mjomba wangu (sio wa kuzaliwa tumbo moja na mama,ila undugu wao ni wa ukoo) ambaye kwa kipindi hicho alikuwa ni meneja katika bandari kavu (KICD) iliyoko chini ya TICTS na mjomba akamwambia kwakuwa sina elimu ya sekondari ni ngumu kupata kazi nzuri na kazi iliyopo ni ya kubeba mizigo so kama nitaweza nimwambie ili aniombee nafasi..mama akanieleza nikamjibu sawa naweza...mwezi wa 5 nikaanza kazi pale kweli ilikuwa kazi ngumu ila kwakuwa niliipenda niliifanya kwa moyo mmoja na mpaka nikapata marafiki wa kizambia na Kongo. Kazi kubwa ilikuwa ni kutoa mizigo kwenye kontena na kupakia kwenye malori na kusafirishwa kwenda aidha Kongo,Zambia ama Malawi. Mizigo ilikuwa ni tofauti tofauti wengine funiture,nguo,betri,nondo,saruji,mafuta ya kula,mpaka sumu. Tulikuwa tunalipwa kwa kontena na ni kwa kila wiki,hivyo ukifanya kontena chache malipo ni machache.
Kuna siku nikiwa kazini nilijiuliza nitafanya kazi hii mpaka lini? Wakuu,hili ni swali ambalo liliyabadilisha sana maisha yangu.Wakati najiuliza hili swali ilikuwa ni mwaka 2007,miaka 2 tangu nianze hii kazi, nikasema ningekuwa na elimu nzuri mjomba angenitafutia kazi nzuri...nikajiwekea mikakati ifuatayo
1.Nisome English Course
2.Nisome Computer Course
3.Nisome sekondari ya miaka 2
Sikupoteza muda,nilienda mtongani kuna chuo kilinivutia kinaitwa The Genesis (mpaka leo kipo) nikauliazia wakaniambia wako levels tatu katika kiingereza na kila level ni elfu 20,na kila level inachukua miezi 2 kukamilika..Nililipa pesa ya levels zote,nilifanya hivi makusudi kabisa ili nikikumbuka kuwa nimelipa kiasi kikubwa cha pesa napata nguvu ya kuhudhuria vipindi..nilikuwa tayari kukosa kazi lakini sio kipindi..niliona bora nipate kipato kidogo kwa wiki kwa miezi sita lakini niandae maisha mazuri zaidi hapo baadae.Kwakuwa akili yangu kubwa ilikuwa darasani niliweza kufanya vizuri mpaka nikwashangaza walimu na wanafunzi maana nilikutana na wanafunzi ambao wako sekondari,wengine wamemaliza lakini nilikuwa nawaburuza. Nilipoanza kusoma nilibezwa sana na jamaa zangu kwamba ooh mizigo na kusoma wapi na wapi,kusoma utasoma wewe? watu wanasoma bila kufanya kazi na wanafeli itakuwa wewe? lakini nashukuru maneno yao hayakunivunja moyo bali yalinipa nguvu zaidi na nilisoma zaidi kuwadhihirishia kwamba inawezekana na kweli iliwezekana.
Tulipofika level three,mwalimu wetu aliondoka na aliyebaki hakuwa vizuri so nikaona kwakuwa sasa najua kuandika na kuzungumza haina haja ya kupoteza muda,nikaanza kozi ya kompyta hapo hapo.Namshukuru Mungu kwani pia nilifanya poa nikapata cheti 2008 mwishoni.Baada ya kupata cheti nikaenda kwa mjomba nikamwambia sasa najua kiingereza na kompyuta hivyo naomba unitafutie kazi nyingine.Lengo langu lilikuwa nipate kazi ya uhakika then ndio niendelee na masomo ya sekondari.
Mwaka 2009 mjomba aliniunganishia kwenye kampuni ya ukarani hapo hapo KICD,nikabadili status sasa kutoka mbeba mizigo mpaka karani,mbali na mshara nilipiga sana hela kwenye hiyo kampuni kwani kulikuwa na mifereji mingi sana mpaka nikawa nasahau pesa zingine kwenye nguo wife akifua anakutana nazo, nikaanza kujenga huku nasoma..baada ya kupita Qt nikasoma O'level miaka 2 then A'level mwaka 1 (HGL), then nikajiunga na chuo kikuu huria (Open University) na kusomea BEDPM.
Sasa hivi nipo kwenye kampuni nyingine japo sifanyii nilichosomea (nipo kitengo cha data entry) lakini elimu niliyonayo ndiyo iliyonifanya niwe hapa na hapa nilipo sio mbali sana na nilipokuwa zamani so huwa naonana na baadhi ya wale jamaa zangu tuliokuwa tunabeba wote wakiwa bado wanabeba.
I do believe that we are what we think.
Mwisho kabisa nipende kuwashauri vijana kwamba tukifikiri vizuri na tukaziamini fikra zetu pasipokujali wanaotuzunguka wanasema nini ni muhimu na ni silaha pekee ya kutupeleka tunapoamini kufika.
Naomba kura zenu wakuu..shukrani.

Upvote
12