SoC01 Safari ya miaka 7 katika uraibu wa filamu za ngono

SoC01 Safari ya miaka 7 katika uraibu wa filamu za ngono

Stories of Change - 2021 Competition

longi mapexa

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2015
Posts
3,265
Reaction score
4,250
Habari Natumaini upo na Uzima.

Basi tumshukuru Mungu kwa hilo. Lakini kama Pia haupo sawa amini kwamba wakati wako Utafika tu.

Bila kupoteza wakati acha nikushirikishe mkasa huu ulionipata na namna nilifanikiwa kujitoa Katika Uraibu wa Machapisho, Picha na Video za Ngono kwa Miaka 7.

Nikiwa na umri mdogo tu wa kati ya 14 au 15 nilijikuta kwa mara ya kwanza natazama picha ya mwanamke akiwa Uchi kabisa. Hii ni baada kupekua simu ya Kaka yangu aliyokuwa kaiweka katika chaji japo Akili yangu ilibadilika nikapatwa na mshangao uliochanganyikana na uwoga kwa haraka nilirudisha simu kisha nikaendelea na mambo mengine.

Ajabu ni kuwa picha ile ilizidi kujirudia kichwani mwangu zaidi na zaidi. Hali hii ilinipelekea kutamani kuziona tena.
Wakati mwingine ulipofika nikajaribu bahati yangu Na kwa hakika nilifanikiwa. Tofauti na wakati uliopita, sikutazama moja tu bali nilikutana na nyingine nyingi sana. Huu ukawa mwanzo wa mimi kupenda picha za wanawake walio uchi kila wakati nikipata nafasi nikawa nazitazama.

Miezi michache mbele nilifanikiwa kumiliki simu najua utashanga. Sikununua nilipewa palepale nyumbani nadiriki kusema kwamba kwa hili familia ilikosea sana. Japo Simu haikua simu janja ila ilikuwa na sehemu ya Intaneti nafkiri kasi ya mtandao ilikuwa ni 2G Hapa nilianza kutumia Google kusearch maneno yoyote yenye kuashiria habari za ngono.

Nayo Google ikanipatia kila nililolitafuta Ikiwa ni pamoja na Simulizi za ngono, Picha na sasa nikaanza hata kupakua video japo ilichukuwa muda mrefu kulingana na kasi ya mtandao.

Wakati wa usiku ndio niliutumia kwani hakukuwa na yeyote wakunishika wala kuniona. Sikupenda usingizi tena nilipenda kutazama ngono kila wakati.

Hii ilifanya wakati mwingine hata mama kukaribia kunikamata. Nakumbuka Mama yangu aliwahi kukuta picha niliyochora kwa penseli japo picha ile ilikuwa ni Ya Ngono kwa asilimia zote. Nilizikana sana ila nafahamu mama alijua tu mwanae nshaharibikiwa.

Shuleni matokeo yakaanza kuporomoka. Nilazima ingekuwa hivyo kwani usiku wote nilikesha mitandaoni. Wakati wa kuamka mimi ndo naanza kulala.

Najivunia kwamba Nikipindi hicho hicho ndicho ambacho nilibahatika kujiunga pia na JamiiForums.

Nilifanya mtihani wa kidato cha nne kinyume na matarajio ya familia nilifanya vibaya sana japo nilifanikiwa pia kwenda kidato cha tano. Lakini nililaumiwa sana kwa kufanya uzembe nilifahamu wapi chanzo cha tatizo lilipo hivyo nilijiapiza kubadilika.

Maisha ya High school Yalinisaidia kupunguza uraibu kwani sikuweza tena kupata simu... Tatizo ni kwamba zile picha nilizozitazama bado zilikuwa zimehifadhiwa kichwani zikijirudia hata kwa njia ya ndoto.

Mfumo wa maisha yangu Ya uraibu ulikuwa ukiendelea pindi napokuwa likizo kwa kuhakikisha kuwa nakata kiu ya uteja wangu.

Miaka ikasogea nikamaliza Kidato cha sita Namshkuru Mungu matokeo yalikuwa mazuri hii ikafanya hata nyumbani wanipumzishe kunisemaa.

Nilipata nafasi ya kujiunga na chuo fulani maarufu hapa Dar es Salaam kwa Kozi ya miaka mitatu. Nikamiliki simu janja Yenye kasi ya 4G Hapa nilibadilika nakujikita rasmi kwenye Uraibu nikawa Porn hunter natazama napakua nahifadhi hata nikaamua kujiunga kwenye porn sites mbalimbali Nilifahamu Porn Stars wengi Hata wakitumika kwenye Memes ilikua rahisi kwangu kuwafahamu.

Sio Tanzania tu bali duniani Kote.
Nilianza kuchagua mpaka aina ya video hatari kubwa ni kuwa kila siku nilikesha kutafuta video za kusisimua zaidi kwani ilifika hatua nikawa sisisimuki kwa baadhi ya video. Mpaka muda huo sikuwa nimewahi kushiriki tendo lenyewe kwa uhalisia.

Maisha ya uhuru chuoni nilijikuta katika uhusiano na binti fulani. Lakini kwa bahati mbaya haukudumu. Sikuwa na tabia za kupendeza nilitaka kuishi na binti yule kama Pornstars wafanyavyo katika videos nilichojali ni ngono hakuna mazungumzo hakuna kubembeleza nilichotaka ni kufanya ngono kadri muda unavyoruhusu Hostel Chuo Barabarani popote kila nikimtazama naona ngono tu. Maskini binti yule hakuyaweza hayo.

Sikujali sana kuhusu mahusiano kwani wapenzi wangu wako kwenye simu nawaona mda wowote nikiwahitaji na wanafanya kile nachotegemea kuona wakifanya. Sikufahamu kwamba nimepoteza Ufahamu wa kawaida.

Miezi ikazidi kusonga lakini tofauti na vijana wengine mimi sikuwa natesekea mahusiano, Sikupenda habari za mapenzi nilikuwa bingwa wa majibu machafu. Kwanini nikasumbuane na wasichana ambao hawafanani na wanawake waliopo kwatika simu yangu.

Kiukweli sikuwa na heshima kwa wadada niliwafokea sikutaka wanizoee wengine niliwaona kabisa wakiumia lakini ningefanyaje?

Kuna wakati Ndani yangu nilihisi nina hatia. Ukweli sikuwa najiamini hivyo nilifanya yote hayo kukinga ukosoaji ni vipi wakigundua tabia yangu ya sirini?

Kila nikiwa kanisani mahubiri yalinichoma. Ajabu wakati wote baada ya kutazama videos nilijiapiza kutokuziangalia tena nikaweka mpaka nadhiri mbele za Bwana Nikaandika tarehe na kuzisaini kabisa kwa vitabu nikajaribu mpaka kufunga na maombi lakini wapi. Niliishia kuteleza na kurudia uteja wangu tena kwa kasi zaidi Kwanini?

Kwa sababu Video na picha za ngono ni tofauti na vilevi ama madwa ya kulevya ambavyo vinahitaji Fedha pia Upatkanaji wake ni mgumu pamoja na Usiri. Ukilewa kila mtu atafahamu. Ila kwa upande wa Porn materials unazipata kwa urahisi bila mtu kufahamu tena kwa uhakika kabisaa. Mtandao unaweza kuwa chini lakini kwenye Pornsites unaperuzi bila shida kabisa.

Namshukuru Mungu mimi ninapenda kujisomea vitabu kupitia hapa nilianza kusoma namna ya kujikwamua kwani Hatia ilinizidia. Njia nilizozipata kupitia vitabu nilianza kuzitumia japo kila wakati nilianguka, Sikukata tamaa kwani niliona nikiwa napunguza kasi ya kutazama mitandao hiyo.

Baada ya muda niliingia katika uhusiano mwingine sijui ilikuaje lakini moyo ulikuwa dhaifu kwa binti yule nilimpenda. Muda mwingi nikatumia kumuona kama malaika wakuniondoa katika janga lile aliweza vumilia ujinga wangu wote hata nikaona napaswa kubadilika.

Ni kweli nilijikuta napunguza muda wa kupita kwenye Porn webs mpaka atleast mara moja kwa Wiki hapa ilikua ni kipindi ambacho yeye anakuwa hayupo na mimi.

Taratiibu nikawa na imarika nikiteleza basi inakuwa ni bahati mbaya tu umepita mtandaoni unakutana nazo(Hii mpaka sasa ni changamoto)

Nilimaliza Chuo lakini uhusiano ukiwa imara sana nampenda Sana binti huyu Siwafikirii tena Pornstars. Kwa sasa Nafikiria namna gani nitaokoa vijana wenzangu.

Ikiwezekana Siku moja nitoke hadharani nishuhudie ili walio dhaifu wapate nguvu kupitia mimi.

Kiukweli madhara ya machapisho Video na picha za ngono naziona mpaka sasa japo nimestaafu kabisa lakini picha zile bado zipo kichwani hata baadhi ya mambo nayoyapenda kitandani ni matokeo ya janga lile.

Kwa sasa nimejitengenezea mpango wa kusafisha mawazo yangu kama ikiwezekana nizisahau kabisa.

Nimalize kwa kusema Kuwa huru kutoka kwenye uraibu wa picha video na machapisho ya Ngono inawezekana.

Chukua hatua madhubuti kwani Ubongo wako ni muhimu sana kwa kuwa huo ndio unaokufanya uwe Wewe. Wewe ni matokeo ya ubongo wako.

Kuna msemo unasema " Kila mtu ana majitu makubwa mawili moja baya moja zuri na siku zote huwa yana pigana Je! wewe unadhani ni yupi atakayeshinda? Atakayeshinda ni yule unaye mlisha" Mungu akubariki!

Njia Nilizotumia.
♡ Nimekuwa nikitafuta maarifa zaidi kuhusu imani yangu na uhusiano na Mungu.
♡ Nimetoa kipaumbele sana kwenye mambo mengine nayopenda tofauti na kazi Kama kupiga Gitaa na Kuchora.
♡ Kwa namna yoyote nimekuwa nikikwepa kukaa mwenyewe kwa muda mrefu.
♡ Kila mara nina utaratibu wa kupitia mabandiko yanayohusu madhara ya Video picha na mabandiko ya ngono ( ukitaka kuua mbwa mpe jina baya ).
♡ Nimemshirikisha mwenza wangu changamoto hii hivyo amekuwa masaada kwangu.
♡ Nimetengeneza ratiba inayoeleweka isiyotoa nafasi ya kuingiza wazo la kutazama Porn sites
kila napofikiria kufanya hivyo nabadili haraka wazo hilo.
♡ Mwisho nilipakuwa App fulani inayofungia picha video ama tangazo lolote la ngono kunifikia.
♡ Simu siweki password ama pattern yeyote akiingia kwa simu yuko huru hii inakuwa kama ulinzi kwamba ukikutwa na porn video ni aibu na sipo tayari kuaibika.

Kila la Kheri.
 
Upvote 52
Hope umeelewa nilichoandika ndio maana hujauliza juu ya maelezo yangu kwako yaliyohusu mada husika, habari ya msamaha wako kwangu kama ulidhani sitakuelewesha zaidi ili uelewe vizuri pole, am much more wider in context than you.

Unachotaka kuhusu mstari fungulia thread yake tusiharibu mantiki ya huu uzi, halafu huyo roho wako anaonekana anapenda taarabu!. Mtumaini Mungu vyema uache mipasho, sio kubeba jina tu.

Hav a gud evening.
Hahahaha.

Sijataka kuuliza kwasababu nafahamu unadandia kitu usichokifahamu, kiufupi wewe ni mdananda wa imani, kaa chini ujifunze taratibu na kanuni mbalimbali za mambo ya imani (Sio mambo ya dini, maana wengi mnadhani kuwahi kanisani au kuswali swala tano ndo kuiva kiimani).
 
Angalia tena, hunifahamu huyo "roho wako" anazidi kukudanganya kuhusu mimi, hilo kanisa ninalosali kama unalifahamu linaitwaje? stop guessing, be real and critical. Kwa jinsi ulivyo uone udhaifu kwenye hoja yangu usiutumie ulivyo na kisebengo cha roho wako!.

Comment # 7 niliyokupa hapo juu ndio imekufunga mdomo, usilete mipasho yako hapa kwa home of great thinkerz.

Kuhusu mambo ya imani na dini (kwenda kanisani in particular) napo nikwambie ukweli hunifundishi chochote, sikutanii, au nakujibu tu for that sake, naaminisha, hunifundishi kitu.

Hizo taratibu napewa na roho wangu sizitafuti kwenye maandiko yaliyochapishwa kwa kutumia roho za wengine kama wewe, hop u see the difference btn us.

Nimeshajadili hilo suala na watu wangu inside out several times, even jana jioni I was thinking about it nikajiuliza hivi siku watu wakiamka wakute majengo ya makanisa hayapo hawataabudu? (hapa sihitaji jibu lako, nakuonesha my practical side of view).
 
Hahahah

"Napewa na roho wangu"

Duh.. udananda huu utatuua, kumbe ukisia Roho wa Bwana ndio na wewe unatafsiri kuwa una Roho wako? Wewe unayo roho (Pumzi takatifu ya uhai itokayo kwa Mungu).. Hakuna mwenye roho wake ambae anaweza akamfunulia spiritual secret, ila Roho wa Bwana peke yake.

Kaka Mimi sikudharau, lakini your too bodily creature.. Mambo ya kimungu hayako kuwaza eti sijui makanisa yasipo kuwepo sijui nini.. (Huo ni utoto na kudhani kuwa wanaondea kanisani hawana/hawajui kuabudu bila hayo majengo), nikushauri... Anza na Toba, Kisha mtafute Mungu katika roho na kweli.
 
Naona unajiamulia tu kujijibia vitu usivyoulizwa, sijakuuliza habari ya "Roho wa Bwana" ni kitu gani, na nikisema "roho wangu" najua nachomaanisha na Mungu wangu, wacha kupenda kukurupuka.

Kama hujaelewa nilichoandika uliza, usikurupuke kujijibu ili ujichekeleshe kama mtoto.

Hakuna popote niliposema nawadharau wanaoenda makanisani, unajiokotea maneno yako unaweka hapa ujichekeleshe, just that.

Again, sijakwambia whether you hate me or whatever, unajishuku tu na huyo roho wako anayekupa ujuaji, hayo uliyoandika sijui umeyatoa wapi?

Like you know me, ulianza na mambo ya muddy, ukaja na kusali kanisa gani sijui, now am too bodily creature, huko kote umekosea, stop guessing kama mganga wa kienyeji.

Am finished with you very long time ago, unataka ubishani tu, hoja huna, ndio maana unajiokotea maneno yako na kujijibu ujichekeleshe.
 
Hahahahahah kwani uongo Wewe muddy na mwamwedy mnatofauti gani?

"Roho wa Bwana" anajulikana hasa kwa wenye "misuli ya imani" na hata wale legelege wa imani kama wewe mtamjua tu kupitia sisi kaka zenu.. Mimi sikuchukii, lakini nakupa ule ukweli fresh toka kwa Roho wa Bwana.. "Pure Spiritual Truth" Hakuna kukupa "uji wa Kiimani" wakati unataka "dona la kiimani".

Mimi nataka ukue kiroho, sio tu kukariri Mungu yupo, shetani yupo, imani ina ngazi basi ndo mwisho.. Mkristo wa kweli, uliyeko katika daraja fulani la kiimani nilitaraji Neno la Bwana liwe msaada wako katika maelezo na mafundisho (sio mabishano) yako, lakini badala yake umejawa na blah blah nyingiiii kwasababu ndani yako Huna Neno la Mungu...

Mungu Akubariki son
 
Angalia tena, hunifahamu huyo "roho wako" anazidi kukudanganya kuhusu mimi, hilo kanisa ninalosali kama unalifahamu linaitwaje? stop guessing, be real and critical. Kwa jinsi ulivyo uone udhaifu kwenye hoja yangu usiutumie ulivyo na kisebengo cha roho wako!.

Comment # 7 niliyokupa hapo juu ndio imekufunga mdomo, usilete mipasho yako hapa kwa home of great thinkerz.

Kuhusu mambo ya imani na dini (kwenda kanisani in particular) napo nikwambie ukweli hunifundishi chochote, sikutanii, au nakujibu tu for that sake, naaminisha, hunifundishi kitu.

Hizo taratibu napewa na roho wangu sizitafuti kwenye maandiko yaliyochapishwa kwa kutumia roho za wengine kama wewe, hop u see the difference btn us.

Nimeshajadili hilo suala na watu wangu inside out several times, even jana jioni I was thinking about it nikajiuliza hivi siku watu wakiamka wakute majengo ya makanisa hayapo hawataabudu? (hapa sihitaji jibu lako, nakuonesha my practical side of view).
Duh walokole hadi kisebengo mnakijua?
 
Hahahahahah kwani uongo Wewe muddy na mwamwedy mnatofauti gani?

"Roho wa Bwana" anajulikana hasa kwa wenye "misuli ya imani" na hata wale legelege wa imani kama wewe mtamjua tu kupitia sisi kaka zenu.. Mimi sikuchukii, lakini nakupa ule ukweli fresh toka kwa Roho wa Bwana.. "Pure Spiritual Truth" Hakuna kukupa "uji wa Kiimani" wakati unataka "dona la kiimani".

Mimi nataka ukue kiroho, sio tu kukariri Mungu yupo, shetani yupo, imani ina ngazi basi ndo mwisho.. Mkristo wa kweli, uliyeko katika daraja fulani la kiimani nilitaraji Neno la Bwana liwe msaada wako katika maelezo na mafundisho (sio mabishano) yako, lakini badala yake umejawa na blah blah nyingiiii kwasababu ndani yako Huna Neno la Mungu...

Mungu Akubariki son
Unajikuza tu hata sioni chochote cha maana ulichonacho, umejidumaza akili unajiona fundi wa mipasho tu, huna logic yoyote kwenye maelezo yako.

Umekomaa tu hunichukii...hunichukii... since morning, hujiamini coz una imani fake, nimekupa maneno uyasome na kuyaelewa, wenye viwango vya imani wapo wewe ni arrogant tu.
 
Wanajua, wanajua hadi "One People, different identity (color)" toka kwa hayati LUCKDUBE.

Intelejensia ya Rohoni.
Lazima umuunge mkono mpiga ramli mwenzio, uwezo wako wa kujenga hoja ni mdogo sana, naona unachekacheka tu ndo maana nime ku-dump na "roho wako".
 
Unajikuza tu hata sioni chochote cha maana ulichonacho, umejidumaza akili unajiona fundi wa mipasho tu, huna logic yoyote kwenye maelezo yako.

Umekomaa tu hunichukii...hunichukii... since morning, hujiamini coz una imani fake, nimekupa maneno uyasome na kuyaelewa, wenye viwango vya imani wapo wewe ni arrogant tu.
Sikia wewe nani kaanza habari za chuki? Si wewe Tena baada ya kusema hivo nikakuonea huruma ndio nikakujibu (Only once) SASA TOKA HIYO ASUBUHI INAKUJAJE?

Hapa tunakufundisha kumjua Mungu, Mimi sina ROHO WANGU, ninaongozwa na ROHO WA BWANA..

Simply ngoja nikuambie, Wewe Kama unamjua Mungu ndani yako lazima ujae mafundisho yake, Mafundisho yake utayapata wapi Kama si kwenye Neno Lake..

Wewe kwa sehemu kubwa Sana bado uko gizani, kichwani umejaza ma-theory na ma-principle ya wanadamu wenzio.. toa hayo jaza Neno la Mungu..

Zaburi 119:105
"Neno lako ni taa ya miguu yangu,
Na mwanga wa njia yangu."

Kama huna Neno (Ndivyo ulivyo wewe) mbele yako ni giza tupu, njia yako haina nuru.. na mbaya zaidi Kama unaongozwa na roho wako (Kama ulivyo wewe) basi tambua Umepotea, Mtafute Roho wa Bwana akuongoze..

1 Timotheo 4:1
"Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani;"

Acha kusikiliza hiyo unayoiita "roho yako" hiyo inakudanganya, Mtafute Roho wa Bwana.. atakurudisha yakupasayo kutenda, kunena, n.k.. Pia jaza Neno la Mungu ndani yako uache ili hiyo nafasi iliyokaliwa na mafundisho ya mashetani isiwepo Tena.. Soma Neno, shika Neno, tenda Neno, ishi Neno..

Acha blah blah
 
Lazima umuunge mkono mpiga ramli mwenzio, uwezo wako wa kujenga hoja ni mdogo sana, naona unachekacheka tu ndo maana nime ku-dump na "roho wako".
Mudy na Mwamedi..
"One people different identity (color)"

Nadhani Sasa umeeanza kuelewa.
 
Nyeto bhana. Nilianza kama masihara ikawa ndo basi tena. Nilishahudhuria maombi na makanisa mengi ila wapi. Shetani ni mpumbavu sana.
ili uache lazima ujikane mkuu...ila ukiweza kwa siku 90 basi kurudia itakua ngumu.
 
Pole sana mkuu kwa yaliyokupata. Lakini hongera kwa kupiga hatua kubwa sana kujikwamua na hili janga.
Kila siku ni kupambana maana nikikaa vibaya tarudi tena kwani vishawishi vipi kila eneo.
 
Umesoma Uzi wote?

Mimi nimemuambia afanye Toba kwasababu Yawezekana hajawai kutubu kwa kitendo cha kujichua.

Wewe unakuja kumuelekeza mbinu za kuacha na kukosoa mikakati yake na wakati kaandika kaacha, ni wazi umekurupuka kunijibu (NAFAHAMU HILI nilishakutambua rohoni mpendwa, Karibu), na pia si ajabu wewe na mwandishi ni Mudi na Mwamedi (majina tofauti mtu yuleyule).

Nisamehe Kama nimekukwaza, leo intelejensia ya kiroho ipo kwa kiwango kikubwa Sana.. nisamehe pia kama nimekujibu vibaya.

Asante
Bado nimekuwa nikisubiri maelezo yako kuhusu toba......Je Toba /kutubu ni kufanyaje/nini....
 
Bado nimekuwa nikisubiri maelezo yako kuhusu toba......Je Toba /kutubu ni kufanyaje/nini....
Kumuomba Mungu msamaha kwa kitendo chochote ulichofanya ambacho ni machukizo mbele yake, ukishaomba msamaha inakupasa kuwa mwaminifu mbele zake kwa kutorudia tena kosa hilo.

Tunapofanya jambo ambalo ni machukizo zipo adhabu mbele yetu, ila kwa kuomba msamaha tunaondolewa zile adhabu, na hata madhara ambayo yamepatikana kutokana na tendo hilo yaweza kufutwa na wewe ukairudia hali yako ya zamani..

Je, wewe unatambua na kuamini kitendo chako cha kuangalia video za ngono na kujichua kilikuwa no machukizo mbele ya Mungu?
 
Je kama mkristo ukisha tubu utapaswa kufanya nini ili kuwa mwaminifu na kutokurudia kosa?
 
Mudy na Mwamedi..
"One people different identity (color)"

Nadhani Sasa umeeanza kuelewa.
Kama fikra zangu zitakuwa sahihi kuhusu ulicholenga kukimaanisha hapa basi utakuwa huonyeshi tabia za kumpendeza kristo.
 
Back
Top Bottom