SoC01 Safari ya miaka 7 katika uraibu wa filamu za ngono

SoC01 Safari ya miaka 7 katika uraibu wa filamu za ngono

Stories of Change - 2021 Competition

longi mapexa

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2015
Posts
3,265
Reaction score
4,250
Habari Natumaini upo na Uzima.

Basi tumshukuru Mungu kwa hilo. Lakini kama Pia haupo sawa amini kwamba wakati wako Utafika tu.

Bila kupoteza wakati acha nikushirikishe mkasa huu ulionipata na namna nilifanikiwa kujitoa Katika Uraibu wa Machapisho, Picha na Video za Ngono kwa Miaka 7.

Nikiwa na umri mdogo tu wa kati ya 14 au 15 nilijikuta kwa mara ya kwanza natazama picha ya mwanamke akiwa Uchi kabisa. Hii ni baada kupekua simu ya Kaka yangu aliyokuwa kaiweka katika chaji japo Akili yangu ilibadilika nikapatwa na mshangao uliochanganyikana na uwoga kwa haraka nilirudisha simu kisha nikaendelea na mambo mengine.

Ajabu ni kuwa picha ile ilizidi kujirudia kichwani mwangu zaidi na zaidi. Hali hii ilinipelekea kutamani kuziona tena.
Wakati mwingine ulipofika nikajaribu bahati yangu Na kwa hakika nilifanikiwa. Tofauti na wakati uliopita, sikutazama moja tu bali nilikutana na nyingine nyingi sana. Huu ukawa mwanzo wa mimi kupenda picha za wanawake walio uchi kila wakati nikipata nafasi nikawa nazitazama.

Miezi michache mbele nilifanikiwa kumiliki simu najua utashanga. Sikununua nilipewa palepale nyumbani nadiriki kusema kwamba kwa hili familia ilikosea sana. Japo Simu haikua simu janja ila ilikuwa na sehemu ya Intaneti nafkiri kasi ya mtandao ilikuwa ni 2G Hapa nilianza kutumia Google kusearch maneno yoyote yenye kuashiria habari za ngono.

Nayo Google ikanipatia kila nililolitafuta Ikiwa ni pamoja na Simulizi za ngono, Picha na sasa nikaanza hata kupakua video japo ilichukuwa muda mrefu kulingana na kasi ya mtandao.

Wakati wa usiku ndio niliutumia kwani hakukuwa na yeyote wakunishika wala kuniona. Sikupenda usingizi tena nilipenda kutazama ngono kila wakati.

Hii ilifanya wakati mwingine hata mama kukaribia kunikamata. Nakumbuka Mama yangu aliwahi kukuta picha niliyochora kwa penseli japo picha ile ilikuwa ni Ya Ngono kwa asilimia zote. Nilizikana sana ila nafahamu mama alijua tu mwanae nshaharibikiwa.

Shuleni matokeo yakaanza kuporomoka. Nilazima ingekuwa hivyo kwani usiku wote nilikesha mitandaoni. Wakati wa kuamka mimi ndo naanza kulala.

Najivunia kwamba Nikipindi hicho hicho ndicho ambacho nilibahatika kujiunga pia na JamiiForums.

Nilifanya mtihani wa kidato cha nne kinyume na matarajio ya familia nilifanya vibaya sana japo nilifanikiwa pia kwenda kidato cha tano. Lakini nililaumiwa sana kwa kufanya uzembe nilifahamu wapi chanzo cha tatizo lilipo hivyo nilijiapiza kubadilika.

Maisha ya High school Yalinisaidia kupunguza uraibu kwani sikuweza tena kupata simu... Tatizo ni kwamba zile picha nilizozitazama bado zilikuwa zimehifadhiwa kichwani zikijirudia hata kwa njia ya ndoto.

Mfumo wa maisha yangu Ya uraibu ulikuwa ukiendelea pindi napokuwa likizo kwa kuhakikisha kuwa nakata kiu ya uteja wangu.

Miaka ikasogea nikamaliza Kidato cha sita Namshkuru Mungu matokeo yalikuwa mazuri hii ikafanya hata nyumbani wanipumzishe kunisemaa.

Nilipata nafasi ya kujiunga na chuo fulani maarufu hapa Dar es Salaam kwa Kozi ya miaka mitatu. Nikamiliki simu janja Yenye kasi ya 4G Hapa nilibadilika nakujikita rasmi kwenye Uraibu nikawa Porn hunter natazama napakua nahifadhi hata nikaamua kujiunga kwenye porn sites mbalimbali Nilifahamu Porn Stars wengi Hata wakitumika kwenye Memes ilikua rahisi kwangu kuwafahamu.

Sio Tanzania tu bali duniani Kote.
Nilianza kuchagua mpaka aina ya video hatari kubwa ni kuwa kila siku nilikesha kutafuta video za kusisimua zaidi kwani ilifika hatua nikawa sisisimuki kwa baadhi ya video. Mpaka muda huo sikuwa nimewahi kushiriki tendo lenyewe kwa uhalisia.

Maisha ya uhuru chuoni nilijikuta katika uhusiano na binti fulani. Lakini kwa bahati mbaya haukudumu. Sikuwa na tabia za kupendeza nilitaka kuishi na binti yule kama Pornstars wafanyavyo katika videos nilichojali ni ngono hakuna mazungumzo hakuna kubembeleza nilichotaka ni kufanya ngono kadri muda unavyoruhusu Hostel Chuo Barabarani popote kila nikimtazama naona ngono tu. Maskini binti yule hakuyaweza hayo.

Sikujali sana kuhusu mahusiano kwani wapenzi wangu wako kwenye simu nawaona mda wowote nikiwahitaji na wanafanya kile nachotegemea kuona wakifanya. Sikufahamu kwamba nimepoteza Ufahamu wa kawaida.

Miezi ikazidi kusonga lakini tofauti na vijana wengine mimi sikuwa natesekea mahusiano, Sikupenda habari za mapenzi nilikuwa bingwa wa majibu machafu. Kwanini nikasumbuane na wasichana ambao hawafanani na wanawake waliopo kwatika simu yangu.

Kiukweli sikuwa na heshima kwa wadada niliwafokea sikutaka wanizoee wengine niliwaona kabisa wakiumia lakini ningefanyaje?

Kuna wakati Ndani yangu nilihisi nina hatia. Ukweli sikuwa najiamini hivyo nilifanya yote hayo kukinga ukosoaji ni vipi wakigundua tabia yangu ya sirini?

Kila nikiwa kanisani mahubiri yalinichoma. Ajabu wakati wote baada ya kutazama videos nilijiapiza kutokuziangalia tena nikaweka mpaka nadhiri mbele za Bwana Nikaandika tarehe na kuzisaini kabisa kwa vitabu nikajaribu mpaka kufunga na maombi lakini wapi. Niliishia kuteleza na kurudia uteja wangu tena kwa kasi zaidi Kwanini?

Kwa sababu Video na picha za ngono ni tofauti na vilevi ama madwa ya kulevya ambavyo vinahitaji Fedha pia Upatkanaji wake ni mgumu pamoja na Usiri. Ukilewa kila mtu atafahamu. Ila kwa upande wa Porn materials unazipata kwa urahisi bila mtu kufahamu tena kwa uhakika kabisaa. Mtandao unaweza kuwa chini lakini kwenye Pornsites unaperuzi bila shida kabisa.

Namshukuru Mungu mimi ninapenda kujisomea vitabu kupitia hapa nilianza kusoma namna ya kujikwamua kwani Hatia ilinizidia. Njia nilizozipata kupitia vitabu nilianza kuzitumia japo kila wakati nilianguka, Sikukata tamaa kwani niliona nikiwa napunguza kasi ya kutazama mitandao hiyo.

Baada ya muda niliingia katika uhusiano mwingine sijui ilikuaje lakini moyo ulikuwa dhaifu kwa binti yule nilimpenda. Muda mwingi nikatumia kumuona kama malaika wakuniondoa katika janga lile aliweza vumilia ujinga wangu wote hata nikaona napaswa kubadilika.

Ni kweli nilijikuta napunguza muda wa kupita kwenye Porn webs mpaka atleast mara moja kwa Wiki hapa ilikua ni kipindi ambacho yeye anakuwa hayupo na mimi.

Taratiibu nikawa na imarika nikiteleza basi inakuwa ni bahati mbaya tu umepita mtandaoni unakutana nazo(Hii mpaka sasa ni changamoto)

Nilimaliza Chuo lakini uhusiano ukiwa imara sana nampenda Sana binti huyu Siwafikirii tena Pornstars. Kwa sasa Nafikiria namna gani nitaokoa vijana wenzangu.

Ikiwezekana Siku moja nitoke hadharani nishuhudie ili walio dhaifu wapate nguvu kupitia mimi.

Kiukweli madhara ya machapisho Video na picha za ngono naziona mpaka sasa japo nimestaafu kabisa lakini picha zile bado zipo kichwani hata baadhi ya mambo nayoyapenda kitandani ni matokeo ya janga lile.

Kwa sasa nimejitengenezea mpango wa kusafisha mawazo yangu kama ikiwezekana nizisahau kabisa.

Nimalize kwa kusema Kuwa huru kutoka kwenye uraibu wa picha video na machapisho ya Ngono inawezekana.

Chukua hatua madhubuti kwani Ubongo wako ni muhimu sana kwa kuwa huo ndio unaokufanya uwe Wewe. Wewe ni matokeo ya ubongo wako.

Kuna msemo unasema " Kila mtu ana majitu makubwa mawili moja baya moja zuri na siku zote huwa yana pigana Je! wewe unadhani ni yupi atakayeshinda? Atakayeshinda ni yule unaye mlisha" Mungu akubariki!

Njia Nilizotumia.
♡ Nimekuwa nikitafuta maarifa zaidi kuhusu imani yangu na uhusiano na Mungu.
♡ Nimetoa kipaumbele sana kwenye mambo mengine nayopenda tofauti na kazi Kama kupiga Gitaa na Kuchora.
♡ Kwa namna yoyote nimekuwa nikikwepa kukaa mwenyewe kwa muda mrefu.
♡ Kila mara nina utaratibu wa kupitia mabandiko yanayohusu madhara ya Video picha na mabandiko ya ngono ( ukitaka kuua mbwa mpe jina baya ).
♡ Nimemshirikisha mwenza wangu changamoto hii hivyo amekuwa masaada kwangu.
♡ Nimetengeneza ratiba inayoeleweka isiyotoa nafasi ya kuingiza wazo la kutazama Porn sites
kila napofikiria kufanya hivyo nabadili haraka wazo hilo.
♡ Mwisho nilipakuwa App fulani inayofungia picha video ama tangazo lolote la ngono kunifikia.
♡ Simu siweki password ama pattern yeyote akiingia kwa simu yuko huru hii inakuwa kama ulinzi kwamba ukikutwa na porn video ni aibu na sipo tayari kuaibika.

Kila la Kheri.
 
Upvote 52
Nyeto bhana. Nilianza kama masihara ikawa ndo basi tena. Nilishahudhuria maombi na makanisa mengi ila wapi. Shetani ni mpumbavu sana.
[emoji23][emoji23] sipend hata kukumbuka ilivoniteka enz izo fom 3
 
wala usijilazimishe kuacha mkuu, we kama hamu ipo na hisia zipo piga kistaarabu tu, unapitisha siku tatu au mbili sio unapiga kila siku
Sometimes ata week 1, 2 au mwez unafikisha inatokea pia ukiwa na dem inakua rahis zaid
 
Sometimes ata week 1, 2 au mwez unafikisha inatokea pia ukiwa na dem inakua rahis zaid
Apo ww mbona fresh tu mze, nyeto ukiipiga kwa afya ni nzur sana inaimarisha afya ya mwanaume. Tatizo linalokuja kwa upigaji wa nyeto ni kupiga kupita kiasi kwa sababu ya upataikanaji wake. Mda wowote ipo, ila ata Ngono ukifanya sana bila kiasi madhara yake ni makubwa sana ata nyeto haifikii kwanza nyeto haina madhara kama Ngono isio na kiasi
 
[emoji23][emoji23][emoji119]
 
Unawez usiache maan we ni mwanaume, sema sas uwe na maamuz ya uwezo wa kujicontrol ukiamua nisipige unaweza
Kwann uache, akat ni tamu [emoji3] wengi wanapiga nyeto, sema tu tunatofautiania kiasi na aina ya upigaji
 
Kiukwel mimi nyeto nilianza nikiwa form 3 2017 hyo ilitokana na mimi kuangalia sana porno hasa usiku nikapiga siku ya kwanza niliona raha sana huo mwaka sikupiga saana hata mara kumi haivuki maana nilikua nikifanya sana mapenz pia asa mwaka 2018 nilipiga mara moja moja pia kasheshe ilianza mwaka 2019 baada ya kupata likizo ndefu ya form4 kuna kipind napiga sanaaaaa hata bao 5 kwa siku af natulia hata week kadhaa kutokana na kuwa na harakat mbal mbal ila siku nikiwa mwenyewe tu bas lazma nipige bao kuanzia mbil ila nilipoenda advance ikawa mara moja moja sana maana ubize na masomo pia kufanya sana mapenz ila pia baada ya kumaliza advance nilipiga mara kadhaa pia ila hal ilikoma baada ya kwenda jeshin ila now niko chuo nyeto pia kuna mda napiga sana had kuna time mkuyati ulichubuka chanzo kikubwa ni porno aisee ila nashukuru mungu uwezo wa kujicontrol nnao pia nimekua na taratibu ya kula vitu kama mbegu za maboga na karanga mbichi pia maji meng huwa nakunywa hvo natumai kila nnachopoteza bas huwa nakijrejesha ila pia mazoez napiga sana this why najiamin hata ikitokea inabd nile mbususu power ipo ya kutosha ila vita ya kuacha nyeto ni kubwa sana maana unaweza kili mungu naomba nikipiga tena nife ila unajikuta unapiga ila nyeto inaachika ni suala la kujiakataa pia kuhakikisha hukai peke ako
nawasilisha.
 
Ko hujaacha mzee
 
Swala ni kujicontrol na ukiweza kujicontrol sio uraibu tena, self guilty unayoipata baada ya hilo tendo mara nyingi huchangiwa na mitizamo ya kiimani, ila kuna imani nyingine zinaamini nyeto ni tendo salama na njia bora ya mwanaume kuujua uanaume wake.
Kwa mfano Taoist wao hutumia tendo hilo kuwafundisha vijana wanaobalehe namna ya kuweza kuzitambua hisia zao na kuzicontrol, yaani kuna namna ukiitumia nyeto unaweza kujifunza jinsi ya kucontrol misuli ya uume ili uweze kuzuia bao linapotaka kutoka mapema. Ukimaster hili unaweza kucontrol mshindo kwa kutumia akili tu yaani unaweza kufanya mapenzi hata masaa 6 bila kukojoa (ila zoezi hili halihusishi porno au material yoyote ya design hiyo just your mental imagination of the real woman you like around your society).
Ni kama hadithi ila ni mambo yapo japo yanahitaji mafunzo na umakini wa hali ya juu sana.
Hii siri nawaibia, ukipiga nyeto on reverse way yaani mkono kutoka nyuma kwenda mbele kwenye kichwa kidogo ni njia safi na salama ya kuongeza girth/unene wa dushe.
ONYO: kuna vitu kwanza unapaswa kuvijua namna ya kufanya hili zoezi, maandalizi, round ngapi, nini ufanye baada ya kumaliza na sharti mpaka unamaliza usikojoe wala dushe lisikaze, ni somo refu hivyo usikurupuke ukajikuta umeharibu mambo kabisa
 
Hapo kwenye Siri hamna punyeto,
Punyeto Ni mpaka mtu akojoe[emoji16][emoji16][emoji16]
 
Kuacha inataka moyo kwa kweli unaweza ukaacha hata mwaka mara unapita Instagram na Facebook unasikia kuna connection mpya unaitafuta ukiipata unaanza kujichukulia sheria mkononi hujakaa sawa Instagram unaona picha ya linah sanga hata chupi hana kapost aisee ni mungu tu kwa kweli au ujizuie usitumie smart phone kabisa.
 
Tuishi humo
20220315_074257.jpg
 
Back
Top Bottom