Safari ya Mwanza - Dar Kwa bus ni adhabu

Safari ya Mwanza - Dar Kwa bus ni adhabu

Bado haiondoi umbali.
Mwanza-Dar siku hizi pamekuwa parefu tofauti hata zamani. Tulikuwa tunafika siku hiyohiyo kwenye saa 1 jioni au saa2 na Zuberi.
Leo hii masaa yameongezeka, mnasafiri njiani hadi unahisi kizunguzungu.
Nini kimeongeza umbali ?
 
Mnampa sifa asizostahili kabisa.
Aliyemzaa mtoto na kufariki baada ya miaka 5 na aliyemtoa hapo kwa kumlea kimaadili, kumvisha,kumsomesha,kumuoza,nk nani apewe sifa zaidi?
Magu hata Chalinze angekuwa bado. Srma alikuwa mtu wa kupenda misifa. Sikopiii nje huku anakopa kimya kimyaa
Pole.
 
Geuza safar ndefu kua utalii itakusaidia sana, ushajua safar yako itachukua masaa 12 na kuendelea basi tafuta bas zuri siti nzuri na mtu utakae kaa nae jitaid upate mtu poa na msafi

Ttzo tunapenda kuleta siasa kwenye kila jambo sa sehemu ina km800+ sa unataka serikal ipafupishe kwa njia gan , ndege haiwezi kua solusheni ata km bei zikishushwa sabu ndege zenyewe hazitoshi lakin pia sio wote wenye uwezo wa kupanda ndege
 
We acha tu mkuu
Pole sana...kuna mbinu za kufanya ili safari ndefu iwe enjoyable. Kwanza kwa kuwa huwezi kupanda ndege basi walau panda Bus zuri la Luxury kama Ally's and others. Pili uwe na kitabu kizuri cha kusoma, hard copy au hata soft copy PDF kwenye simu. Kama huwezi kusoma au hupendi kusoma basi andaa movies nzuri kwenye simu yako. Ukitaka safari yoyote iwe boring na ya kuchosha uwe huna kitu cha kufanya. Kumbuka kuna watu wanasafiri kutoka bongo mpaka South Africa kwa Bus.
 
Umasiki mbaya aisee,

Natoka Mwanza naenda Dar hapa ni saa 5 kasoro ndiyo natoka Shinyanga nimeanza safari saa 1 jioni na hapa nimechoka sana na tunafika Dar kesho saa 7 mchana aisee sijui nitakuwa na hali gani

Mungu nijalie wakati wa kurudi nipande Air Tanzania
Uko sahihi,route zote ndefu za kuanzia km 700 Kwa basi ni majanga sana.

Na balaa kinaanza pale ambapo unaamua kusafiri masaa yote hayo Kwa siku Moja,Bora usafiri nusu nusu.

Kuna
Dar-Sumbawanga
Dar-Musoma
Dar-Mpanda
Dar-Kigoma
Dar-Tunduma
Dar-Bukoba
Dar-Geita nk nk
 
Back
Top Bottom