Safari ya mwisho ya maisha-Kijijini au Mjini?

Masanja

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2007
Posts
5,319
Reaction score
10,416
Wanabodi hebu leo tutatazame kitu tofautI,

Majority ya wengi wetu tumekuja mjini kutafuta maisha. Na hii ni kwetu almost wote, at least 90%. Na hii inasababishwa na ukweli kwamba fursa nyingi zipo mjini. Wengi tukifika mjini tunapambana na kufanikiwa. Wengine wanajenga majumba na kumiliki mali kadhaa. wengine wanapata elimu na kukuza uchumi wao na familia zao. Ilimradi kila mtu anapambana kivyake.

Katika hizi harakati wengi wanapasahau au wanapapotezea kijijini walipotoka. Ni wachache wanaokuwa na uthubutu wa kwenda kujenga nyumba/miji yao kijijini walipotokea. Wengi wanakuwa na sababu mbalimbali kwa nini hawawezi kwenda kuwekeza hela zao vijijini. Wengine watakwambia, hawawezi kujenga kwa sababu ya uchawi nk. In fact, wengine wakiondoka hawarudi. Ndo imeisha hiyo.

kilichonifanya nilete huu uzi, Naamini wengi ni wahanga wa hili, either personally au wazazi. Unakuta mtu huna hata kibanda kijijini, Ila ukitangulia mbele ya haki familia yako ina insist kwamba marehemu aliagiza akitangulia mbele ya haki akazikwe kijijini karibu na makaburi ya wazazi wake. Au familia inakazia kwamba lazima jamaa mwili wake ukazikwe kijijini. Au pia kwa sababu za kiuchumi, familia inabidi irudi tuu kijijini hakuna namna. Au kwa sababu jamaa ni mtu wa mfumo….na serikali inagharimia…inabidi tuu apelekwe kwao.

Katika haya maamuzi ya kurudisha mwili wengi wamekumbana na changamoto nyingi. Mshua alikuwa mtu mzito mjini, kaacha mali nyingi na familia imesimama huko mjini. Lakini anazikwa kama swala. Kwa sababu hakuwahi kujenga hata banda la mbuzi. Unakuta msiba unawekwa kwa jirani au hata watu baki tuu au hata kwa Mwenyekiti wa mtaa. Kiufupi hata familia yake pale haifahamiki kabisa. Watu wanazika, then watu waliosindikiza mwili wanasepa.

Concern yangu ni kwa nini kama unajua huna mji au hata kibanda kijijini, familia yako au hata wewe ukiwa hai uagize kwamba siku ukitangulia mbele ya haki, ukazikwe kwenu? Kwa nini usimalizie safari yako ya mwisho mjini? Maamuzi yako ya kuishi town kila mtu lazima ayaheshimu. Lakini pia na wewe jitahidi ukiondoka usiwe mzigo kwa waliobaki. Especially huko kijijini ambapo ulipapotezea kitambo!

Ushauri wangu: Kama wewe umeamua kwamba maisha yako ni mjini, weka maelezo kabisa ukiwa hai. Siku nikitangulia mbele ya haki, nizikwe mjini. kama una plan ya kupumzishwa kijijini, tafadhali fanya maandalizi kijijini kwenu. Weka hata room moja. Maamuzi yako ya kuishi mjini tunayaheshimu sana na wala kujenga kijijini siyo lazima. Lakini pia, mambo ya kusumbuana mwili wako unaletwa kwenu unafikishiwa kwa mwenyekiti wa mtaa, siyo poa. Unakuwa unazingua.

Nimeandika baada ya mwili wa jamaa yangu don wa mjini mwili wake kuletwa kijijini na kufikishiwa kwa Mwenyekiti wa mtaa Kwa sababu kwao hakuweka hata kibanda. Hata costa Iliyo leta mwili Ilikosa parking! Siyo powa kabisa, kwa vyombo alivyokuwa navyo jamaa. Anyway may he RIP.

Wasalaam,
 
Haya tumekuelewa.

Kwa hiyo sisi tuliopanga kuzikwa popote kifo kitakapotukuta hata kama nimeenda mkoa Fulani kwa muda mfupi unatushaurije?
 
Wako wengi tu mkuu rejea ule uzi wangu wa @orodha ya watanzania maarufu waliokufa bila kujenga
 
Hata
Haya tumekuelewa.


Kwa hiyo sisi tuliopanga kuzikwa popote kifo kitakapotukuta hata kama nimeenda mkoa Fulani kwa muda mfupi unatushaurije?
Mimi nimepanga. Ila sitaki kusumbua ndugu na marafiki kupelekwa kijijini ambako sina makazi. Kama vipi, tutamalizana kimjinimjini.
 
Miaka kama 20 hivi iliyopita, nikiwa primary kijijini, nakumbuka ilikuwa Jmosi. Hatukuwa tunakwenda shule siku ile, japo tuliamshwa mapema sana kukoboa mahindi (waliokulia vijijini watakuwa wanaikumbuka). Mara kwa barabarani tukaona lori la jeshi. Kulivyokucha vyema ndo taarifa zikasambaa kwamba kuna mjeshi amekufa, na alitoaga maelezo kwamba pande zile ndo kwao, ila exactly wapi haikujulikana.

Hata jina lilipotajwa, hakuwa wa kule wala hakuna ndugu hata wa mbali aliyejitokeza. Mkuu wa msafara ule aliomba pale kijijini kwamba wazike maana wameshazunguka sana na maiti kitafuta kwao na ndugu zake bila mafanikio. Kengele likapigwa pale, na msiba ukaja wekwa home, kwa ombi la mwenyekiti. Wanakijiji, kama desturi zolivyokuwa, walishiriki maziko, bila hata kujua aliyekufa ni nani. Sina kumbukumbu vizuri kama aliswaliwa, ila nakumbuka risasi zilirindima baada ya mazishi. Marehemu, sio tu kwamba alipakacha kwao, ila alitoa na taarifa za uongo kuhusu kwao.

Na zaidi ya wanajeshi hapakuwa hata na ndugu yake mmoja, ila baadae, kama baada ya miaka mitatu au minne, mama yake pamoja na ndugu zake wawili walifikaga home kumshukuru mother na father kwa kuhost msiba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…