Safari ya Rais Magufuli kwa barabara yawatumbua mameneja wa TANROADS Lindi na Pwani

Safari ya Rais Magufuli kwa barabara yawatumbua mameneja wa TANROADS Lindi na Pwani

Uangalizi wa ile barabara kwa kweli haukuwa mzuri,ina miaka mingi inakufa na hakuna cha maana kilichokuwa kinafanyika...
 
Hakuna kitu cha ajabu nchini kama Katiba, inasema ili uwe Waziri lazima uwe Mbunge. Bunge lilivunjwa Juni, 28 kwa maana hiyo hakuna Mbunge aliyeadarakani. Sasa hawa mawaziri ni Wabunge kwa mujibu wa katiba ipi!?
Hiyohiyo katiba unayoikosoa ndiyo inatamka kuwa waziri atakoma kuwa waziri Kama atakosa sifa ya kuwa mbunge isipokuwa tu kuvunjwa bunge. Hivo bas nikutaarifu ata Ndugai bado ni Spika wa bunge japokuwa bunge limevunjwa.
 
Hakuna kitu cha ajabu nchini kama Katiba, inasema ili uwe Waziri lazima uwe Mbunge. Bunge lilivunjwa Juni, 28 kwa maana hiyo hakuna Mbunge aliyeadarakani. Sasa hawa mawaziri ni Wabunge kwa mujibu wa katiba ipi!?
Sababu ya kuwa na ulazima wa waziri kuwa mbunge ni moja tuu; ili waweze kuingia Bungeni kujibu hoja na maswali ya waheshimiwa wabunge..Na kama sio mbunge huruhusiwi kukanyaga floor ya Bunge..ndio maana ata AG ni mbunge pia. Mawaziri wa SASA wanaendelea kuwa wasaidizi wa Rais mpaka pale utakapofanyika uteuzi mwingine manake serikali iko active muda wote na haivunjwi kama Bunge.
 
Na rais hawezi kutoa pesa kama hamjaenda kuomba mzee
Pesa ya ujenzi wa km 90 ni zaidi ya b100, unafikiri hizo zinaombwa kwa rais? Hiyo ni bajeti ambayo sharti bunge liidhinishe.Sasa kwenye bajeti pesa ilitengwa kwa ajili ya matengenezo hayo?
 
Kwahiyo waziri hawezi kuamua swala kama hili mpaka Rais aseme?Kuna haja gani ya wao kuepo sasa?
 
Fedha zipo? Pole zao mameneja.

Btw, hivi mawaziri nyazifa zao zinakoma lini? Au mpaka baraza jipya liundwe?
Ni kama nchi imeanza kuwepo mwaka jana, kila kitu kimekuwa kipya.
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Rais Magufuli hatoi fedha za road maintenance. Huwa anapiga porojo nyingi ili aonekane anajali!
Zile kelele za juzi ilikuwa kuzima maneno Jk aliyo ongea msibani kwa Mh. Ben
Sio barabara hiyo tuu ndiyo tatizo. N Mh. Kamwelwe ana waadhibu hao mameneja bila kuwaza.
Maana barabara nyingi za Tanzania kw sasa ni mbaya. Kwa mfano barabara ya Dodoma / Mtera Iringa haifai. Nimeipita juzi.
Barbara yaMbalizi kwenda makao makuu ya wilaya ya Songwe na maanisha Mkwajuni hadi Shanta gold mine. Ni kilomita 100 lakini lazima utumie masaa matatu kwa4*4 hao mbona bado wako kazini.
Viongozi mnatakiwa kumshauri Mh. Rais vyema na sio kucheza ngoma anayo itaka. Mvua ziliharibu barabara nyingi sana..
 
Hakuna kitu cha ajabu nchini kama Katiba, inasema ili uwe Waziri lazima uwe Mbunge. Bunge lilivunjwa Juni, 28 kwa maana hiyo hakuna Mbunge aliyeadarakani. Sasa hawa mawaziri ni Wabunge kwa mujibu wa katiba ipi!?
Acha kulisha watu matango pori. Bunge limevunjwa rasmi jana ambapo taarifa imetoka katika Gazeti la serikali
 
Waziri wa ujenzi mh Kamwele amewaondoa madarakani mameneja wa Tanroads wa mikoa ya Lindi na Pwani kufuatia kushindwa kuifanyia matengenezo barabara ya Dar hadi Mtwara.

Maamuzi hayo ya mh Kamwelwe yanafuatia maagizo yaliyotolewa jana na Rais Magufuli ya kutaka hatua zichukuliwe kutikana na ubovu wa barabara alioushuhudia kwenye takribani zaidi ya km 90 .

Source Channel ten

Maendeleo hayana vyama!
Tatizo fedha za maintenance hakuna.Watafukuza sana
 
Hata mimi wakati naenda mtwara nilishangaa sana Aisee ubovu wa barabara, Nilijaribu kureport sehemu tena ndani ya huu huu mwaka ila sikuoni actions zozote Ni Aibu sana kwa Kuwa waziri hajui kuwa Kule kusini road ni mbaya mpaka Mkuu wa nchi apite ndio achukue maamuzi
 
Bwashee huu utaratibu wa hadi rais aone ndipo achukue hatua ni wa hovyo sana, mapema kwenye utawala wake watu walionya kuhusu 'one man show'.

Kama taifa tunahitaji mifumo imara sio kiongozi mmoja anayetaka kufanya kila jambo, nchi ni kubwa hii. Yeye pakee anaweza kutembelea/kufika maeneo mangapi kwa wakati mmoja?

Yaani rais anadeal hadi na issues za vyoo, madarasa, kesi za mirathi nk nk, kweli? Sasa hayo maeneo mengine ambayo hajafika kwa miaka yake mitano kuna hali gani imagine.

Kwa kifupi hilo koti mlilomvika Meko ni kubwa sana halimtoshi, yafaa october avuliwe asubuhi na mapema kabla watu hawajala vitumbua vyao.
 
Hakuna kitu cha ajabu nchini kama Katiba, inasema ili uwe Waziri lazima uwe Mbunge. Bunge lilivunjwa Juni, 28 kwa maana hiyo hakuna Mbunge aliyeadarakani. Sasa hawa mawaziri ni Wabunge kwa mujibu wa katiba ipi!?
Ni utapeli na usanii, wakati huo huo wakiwa mawaziri kupitia ubunge,wamerudi kuomba ridhaa ya kuwa wabunge tena. Yaani kwa kifupi baadhi ya majimbo nafasi ya ubunge na urais inagombewa wakati 'haipo'.
 
Rais Magufuli hatoi fedha za road maintenance. Huwa anapiga porojo nyingi ili aonekane anajali!
Sio kweli lazima ukubali kuna uzembe wa watendaji haiwezekani barabara inaharibika kiwango kile na wewe upo tu unaamka asubuhi unamuaga mkeo/mumeo unaenda kazini wakati huendi kufanya chochote halafu mnakuja na kisingizio cha kukosa pesa😕

Tupunguze kufanya kazi kwa mazoea (Business as usual)
 
Back
Top Bottom