Safari ya Yanga kuishia kwenye makundi?, Mc Alger na Al Hilal zitasonga mbele Robo fainali?

Safari ya Yanga kuishia kwenye makundi?, Mc Alger na Al Hilal zitasonga mbele Robo fainali?

Yanga anaweza kukaza tu, sema kumaliza kwenye nafasi mbili za juu bado ni kitendawili kwao.Bado akiwin game zake mbili inabidi kuomba pia Mazembe amfanyie wepesi kwa Mc Alger tabu tupu
Na mlivowafanyia MAOVYOVYO sjui kama watawasaidia
 
1000039609.jpg

Uto wakitumia zana mbalimbali kupima nafasi yao ya kufuzu. Hapo bado hawajaingia vilingeni.
 
Al hilal hawawezi kukubali kumaliza nafasi ya pili hata kidogo kwanini? Kwasababu watakutana na timu ngumu kama al ahly,esperance n.k so mechi dhidi ya yanga watataka washinde au wasare wajihakikishie nafasi ya kwanza.

Kumbuka wakipigwa tatu bila halafu yanga akampiga mc algiers yanga anaweza kuongoza kundi kumbuka game ya mwisho watakuwa away na tp.

Waarabu kwa namna wanavyocheza yanga acheze kweli kwa mkapa ili ashinde.
 
Nikusahihishe kolo, MC alger game ya mwisho anamaliza kwa mkapa na yanga

Gusa achia twende kwao yanga anatakiwa ashinde game mbili zilizobaki bila kujali matokeo ya wengine anafuzu
Mnadhani MC ALGERS ni Mazembe iliyooza? Nyie hapo ndio mwisho mtajitutumua Sana lakini "."
 
si lazima adhinde zote kumbuka yanga na CR b mwaka jana head to head ndy iliamua matokeo
Hapo hakuna head to head.

Yanga anapoint 4. Akishinda Moja na kudraw Moja anakuwa na point 8.

Alger akimpiga Mazembe atafikisha point 8 pia. Hiyo mechi ya draw manaake inakuwa Yanga na Alger. Alger anakuwa na point 9.

Lazima ashinde zote
 
Al hilal hawawezi kukubali kumaliza nafasi ya pili hata kidogo kwanini? Kwasababu watakutana na timu ngumu kama al ahly,esperance n.k so mechi dhidi ya yanga watataka washinde au wasare wajihakikishie nafasi ya kwanza.

Kumbuka wakipigwa tatu bila halafu yanga akampiga mc algiers yanga anaweza kuongoza kundi kumbuka game ya mwisho watakuwa away na tp.

Waarabu kwa namna wanavyocheza yanga acheze kweli kwa mkapa ili ashinde.
Al hilal anampiga TP Mazembe na kujihakikisha nafasi ya kwanza. Kwa hivyo kwa vyovyote yuko namba Moja.
 
Hapo hakuna head to head.

Yanga anapoint 4. Akishinda Moja na kudraw Moja anakuwa na point 8.

Alger akimpiga Mazembe atafikisha point 8 pia. Hiyo mechi ya draw manaake inakuwa Yanga na Alger. Alger anakuwa na point 9.

Lazima ashinde zote
mfano yanga ikidrow na ibenge,yanga atakuwa na point 5.

mfano alger akifungwa na tp ,alger arakuwa na point 5.

mechi ya mwisho yanga vs Alger hapa head to head lazima ihusike tu. kama ilivyo kuwa mwaka jana yanga vs CR B
 
Alger game inayofuata yupo home na Tp, hii game anashinda....Yanga atakua ugenini na Al Hilal. Sasa Yanga akipoteza,Alger akashinda...kipindi kitakua kimejifunga bila kusubiri game za mwisho.
Yanga inabidi akomae,Al Hilal sio wa kufikiria kuwashinda kirahisi ,ila Alger akidroo na Tp hata Yanga akifungwa na Al Hilal,game ya mwisho kwa mkapa itakua ni vita ya tatu ya Dunia,na anaweza penya.
 
Good Bye Yanga !! Mpaka mwakani.

Njia pekee ya Yanga kushinda mechi zote zilizobaki 😃😃 Yani amfunge Al Hilal Nyumbani kwao na amfunge Mwarabu kwa Mkapa,

Walichobakiza Yanga ni kukamilishe Ratiba

View attachment 3193688
Rage ajengewe mnara amefuga mandondocha wengi sana,,kama Mc alger angeshinda ndio ingekuwa mwisho wa yanga but katoa sare Ina maana bado nafasi ya pili Iko wazi kwa hizo timu 2, na yanga akimkaanga Al hilal ambae keshafuzu na akamtandika Mc alger anafuzu mapema tu bila kuangalia matokeo ya alger na mazembe
 
Yanga anaweza kukaza tu, sema kumaliza kwenye nafasi mbili za juu bado ni kitendawili kwao.Bado akiwin game zake mbili inabidi kuomba pia Mazembe amfanyie wepesi kwa Mc Alger tabu tupu
Yanga akishamchapa Al hilal ambae 98% keshafuzu na akimtandika Mc alger kwa mkapa biashara inakuwa imekwisha ata Mc alger akimfunga mazembe inakuwa aiwasaidii chochote yanga anafuzu!
 
Ni ngumu ila tukishinda hiyo ya away tunatoboa, hiyo ndo mechi ngumu.
Ya hapa home tutawapiga sindano na kupuliza dawa vyumba vya wapinzani.
 
Sote tunatakiwa kujua haya.
-Al hilal ameshafuzu.
-Wengine wote waliobaki wanayo pia nafasi ya kupambania kufuzu
-Yanga akishinda game zake zote anafuzu moja kwa moja
-Yanga akitoa sare moja dhidi ya Al hilal) na akimfunga MC alger goli za kutosha sana (tofauti ya goli tatu) anafuzu moja kwa moja.
 
Hapa ni kupata ushindi dhidi ya Al Hilal, tukimpasua huyu, muarabu kwa mkapa hatoki.
 
Back
Top Bottom