Safari yako ndefu kuendesha gari bila kupumzika ni ipi?

Safari yako ndefu kuendesha gari bila kupumzika ni ipi?

Halafu mimi nikiendeshaga usiku, mfano napotoka Bunju kwa demu wangu narudi Makongo Juu...

Napopishana na magari, ule mwanga wa Headlights huwa ukinipiga machoni, nashindwa kabisa kuona mbele.

Sasa najiuliza nitaweza kweli kusafiri usiku kwenda kwetu Mwanza!
Huo mwanga mtu akipiga full na wewe piga full atleast uweze kuongeza distance ya kuona ila wakati huo concwntrate na line ya katikati hakikisha hauko karibu nayo wala mbali nayo. Huku ukiwa very conscious na viraka hasa tyre ya kushoto mkuu. Ila vinginevyo mtu akija na full light usiku huwa tuna assume tu huku ukijianda kwa kishindo
 
Kwa hali hiyo utoboi mahali.unachotakiwa kufanya usiwe unatazama gari linalokuja mbele yako direct,unatakiwa utizame chaki ya barabara ya kushoto kwako uku unaibia kinamna hilo gari linalokuja mbele yako.Ata mimi uko nyuma nilikua nateseka sana hadi nilipokuja kupewa hiyo mbinu.Ila siku hizi kuna miwani za kichina yangu nilinunua elfu 60 unaivaa unamwaga moto kama mchana.
Mi huwa nakuwa na wasiwasi gari mabovu kuyaingia
 
Vicheche ndio nini. Wale nguchiro wanaovuka barabara usiku?
Kwani wanaleta shida gani, au ukimgonga unaweza pinduka.
Vicheche ni magari mabovu yaliyopata breakdown , mara nyingi huwa hayana alama yoyote!
Unakuta chombo ya mkaa ipo juu ya jeki , ukiigonga kwanza inashuka ,ndo misala mingine inaendelea, pretty horrific when you think about it!
 
Huo mwanga mtu akipiga full na wewe piga full atleast uweze kuongeza distance ya kuona ila wakati huo concwntrate na line ya katikati hakikisha hauko karibu nayo wala mbali nayo. Huku ukiwa very conscious na viraka hasa tyre ya kushoto mkuu. Ila vinginevyo mtu akija na full light usiku huwa tuna assume tu huku ukijianda kwa kishindo
The best trick unapopivwa full beeam ni kuangalia mstari kama ulivyosema , mara nyingi anayekupiga full anakuwa na advantage ya yeye kuona vizuri kushinda wewe, so unaweza kujikuta kwenye scenario unapigwa full na yet unahamia upande wake anakuhonga na unaonekana wewe nduo mwenye makosa ya wrong site ,
Ukipigwa beam usihangaike kuangalia taa za gari iliyokupiga we angalia chini kwenye baranara , mstari kama upo laIma utaonekana .
 
Mwaka juzi FEB, 2020 Nikiwa na RAV 4 Old model yangu nilikua natoka mwanza to singida, nilianza safari saa 8 usiku.

Nilipofika maeneo ya ZIBA - TABORA mida ya saa 11 alfajiri nikakutana na lori mbele yangu kama mita 50 ghafla likaibuka lori jingne kwa nyuma ya lile lori mbele yangu linaOvertake, hapo nipo 110 km/hr, nilishika breki nikavuta na Hand brake kwa nguvu zoteee, aseee Lile Lori lilininusa si zaid ya sentimeta 10 linigonge upande wangu.

Nilisimamisha gari nikashuka pale nikakojoa mkojo kama lita 5, mwili unatetemeka, jasho linanitoka wakati ni alfajiri kuna baridi.

Nikasimama pale kama dakika 20 nazungumza pekeangu kama kichaa, natoa matusi makali huku natoa maneno ya kumshukuru Mungu hapo hapo.

Tokea siku hiyo nikasema wallah sitothubutu tena kuendesha gari usiku.
 
Nimeendesha gari zaidi ya maili 1300, one way, masaa 24 mfululizo wakati wa winter USA. Kusimama ni gas stops only. Halafu nikarudi tena, same route, same distance, nilisimama kujaza mafuta tu.
Hapa kuna Tangawizi ya kutosha.
 
Mimi na baskeli yangu nilienda 169km at an average of 20kph..

Gari ni kilometa 800 na kitu
 
Mimi umbali mrefu ni Kyela-Dar...nilitok Kyela saa 8 mchana kufika Dar saa 9:30 usiku ila ilikua fresh sababu ya ligi..🤣🤣🤣maeneo ya mafinga kuna malory yana mbao hadi lorry linainama kama linadondoka na halina taa za nyuma usiku unatakiwa uwe na macho mazuri na taa nzuri...
 
Usipokamatwa gachuma,kirumi Basi IPO siku magu patakuzingua. Kuwa lakini sana
Nlinusurika kulaza gari siku natoka mwanza kwenda tarime kwenye daraja la kirumi unapoingia kuna kona mm nliingia mzima halafu kuna vikorogeshen mshenzi kidogo kona ikatae
 
Nimeendesha gari zaidi ya maili 1300, one way, masaa 24 mfululizo wakati wa winter USA. Kusimama ni gas stops only. Halafu nikarudi tena, same route, same distance, nilisimama kujaza mafuta tu.
So ulikuwa huli mzee??? Au ndo kwenye hizo gas stops???
 
The best trick unapopivwa full beeam ni kuangalia mstari kama ulivyosema , mara nyingi anayekupiga full anakuwa na advantage ya yeye kuona vizuri kushinda wewe, so unaweza kujikuta kwenye scenario unapigwa full na yet unahamia upande wake anakuhonga na unaonekana wewe nduo mwenye makosa ya wrong site ,
Ukipigwa beam usihangaike kuangalia taa za gari iliyokupiga we angalia chini kwenye baranara , mstari kama upo laIma utaonekana .
Ila kuna madereva wengine hawanaga uungwana kabisa, either kwakutokufahamu ama kwa makusudi mtu unamflash lakini yeye kangangania full afu mitaa kama ya treni, mi nikishaonaga hivi ni mguu kati tu nanyunyiza mpaka nitakapopita ndio nakiwasha tena.
 
Back
Top Bottom