Mwaka juzi FEB, 2020 Nikiwa na RAV 4 Old model yangu nilikua natoka mwanza to singida, nilianza safari saa 8 usiku.
Nilipofika maeneo ya ZIBA - TABORA mida ya saa 11 alfajiri nikakutana na lori mbele yangu kama mita 50 ghafla likaibuka lori jingne kwa nyuma ya lile lori mbele yangu linaOvertake, hapo nipo 110 km/hr, nilishika breki nikavuta na Hand brake kwa nguvu zoteee, aseee Lile Lori lilininusa si zaid ya sentimeta 10 linigonge upande wangu.
Nilisimamisha gari nikashuka pale nikakojoa mkojo kama lita 5, mwili unatetemeka, jasho linanitoka wakati ni alfajiri kuna baridi.
Nikasimama pale kama dakika 20 nazungumza pekeangu kama kichaa, natoa matusi makali huku natoa maneno ya kumshukuru Mungu hapo hapo.
Tokea siku hiyo nikasema wallah sitothubutu tena kuendesha gari usiku.