Safari yangu "Kitchanga" mji uliotekwa M23

Safari yangu "Kitchanga" mji uliotekwa M23

Justine Marack

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2014
Posts
612
Reaction score
1,698
.
Katika harakati zangu za kujikomboa na umasikini, niliamua kufanya ziara ya kusaka fursa Mpya nchini Congo. Nilikua tayari nimeshapata masimulizi mengi ya upatikanaji wa madini ya dhahabu na Rubi.

Ni mnamo mwaka Juzi mwanzoni nikiwa mji wa Uvira amabapo jilikutana najamaa Akiwa na jiwe alilo dai kuwa ni Rubi

Screenshot_20230127-165416.jpg

Baada ya mazungumzo marefu jamaa alikubali kunipa jiwe Moja ambalo alisema kuwa alishawahi kulipeleka Kigali Rwanda lakini katika vipimo ilitoa majibu yanayo Changanya. Ilisoma upande Moja ni Rubi na wakati mwingine inasoma Spinel. Sasa akanionesha ndoo imekaa mawe ya Kila namna. Kazi yangu nilitakiwa kwanza kwenda Tanzania kupima jiwe hilo ili tujue ni aina Gani ya jiwe Kisha nitafute mteja wa Uhakika ambaye tutakuwa tunampa Mzigo.

Kazi hiyo nikaichukua na kuanza safari, sikuhiyo nililala Bujumbura na keshoyake nikalala Kigoma. Asubuhi nilianza safari mpaka Arusha. Pamoja na kuzongwa na matapale na kashkash nyingi nilifanikiwa kufanya vipimo na bahati mbaya jiwe lilikua feki.

Pale Arusha nilikutana na wadau wengi sana na kupewa michongo nankutiwa moyo sana. Nilianza kuiona Dunia ya dealers. Sasa kazi ilaanza kutafuta connection ili nikasake Mzigo. Hapo ndipo safari wa Kivu kaskazini ikaanza.

Kiukweli sikuwa najua mawazo yangu ni hatari kiasi gani lakini laiti ningelijua pengine ningeanza kuungama dhambi zangu kwanza kabla ya kuanza safari katika ukanda wa damu mbichi.

Wakati ukawadia na safari ikaanza, niliambiwa nitafute biashara ya kwenda mayo ili nizugie kuingia mayo maeneo ya ndani na machimboni. Kwanza nikawaza kupeleka Nguo za kiume Jeans za masela na Viatu moka za Bakulutu na Kisha nikafikiria kupeleka Mchele. Baada tathmini jikapeleka Jeans Viatu na Samaki. Nilidhamilia kukutana na kamii ya Kila namna nanjinsia zote nilidhamilia kufa au kurudi na Mali. Militia taarifa za AWALI kujua hata mavazi ninayotakiwa kuvaa nikiwa huko. Nilihakikisha ninachukua kilataarifa Kwa uzito unao stahili.

Nilijifunza kuhisabu na kutaja pesa Kwa kifaransa, ndani ya wiki Moja nilijua kuhesabu Moja mpaka Milioni na kutaja pesa na maneno muhim ya kibiashara. Mfano Congo neno Kuuza wao linamaana ya kununua kuuu. Nipatie, kombola, mbasela na maneno mengine kama kutaja rangi na kusalimia. Bahati ni kwamba Kiswahili Cha Kivu kinafanana sana na Kiswahili Cha Tanzania Bara tofauti na hawachanganyi sana french kama wale wa Lubumbashi na Kinshasa.
Screenshot_20230127-165613.jpg

Safari ilianza Kwa kupitia Burundi Kisha kuingia mji wa Uvira. Hapo nililala na kesho nikapanda Hiache kwenda Mji wa Bukavu. Nilikua na machaguo mawili aidha kupitia Barabara ya ndani ya Congo au kupitia Rusizi Kisha Rwanda na kurudi tena Congo. Barabara ya ndani ya Congo ni mbaya sana na hatari sana, wanapita watu wahalifu na wanao ogopa ukaguzi wa Rwanda na ukifika unafanyiwa sherehe yaani makorongo na magari kuanguka sio habari tena, kutekwa na kuuwawa ni kawaida kuliko kusaliklmiana. Hii inaitwa Barabara ya Ngomo(Kaburi wazi)

Changamoto ya kupitia Rwanda, ukiwa na Visa ya Dola 50 basi ukiingia Rwanda Visa ya Congo imeisha na ukitaka tena kuingia Congo Kwa kutokea Barabara mchepuko ya Rwanda basi utalazimika kulipia Visa tena, kwahiyo kupitia njia hiyo utalipa Dola 200 kwenda na kurudi. Suluhisho ni Visa ya Dolar100 ambayo unapewa miezi mitatu na unaweza kutoka Congo na kuingia kadili uwezavyo. Hilo nilisha lifuatilia mapemaa, nikawa na Visa ya Dola100 nikapita Rwanda. Kuna mengi hapa Rwanda lakini kwakua sio mada ya Leo itoshe kusema ni Dunia tofauti sana. Tuishi bongo tu, amani inatosha.

Sasa niliingia mjini Bukavu kupitia mpaka wa Rusizi. Pale Bukavu wakati nimeingia nikakuta watu wanafunga maduka na kukimbia kujificha, nilipojaribu kuuliza wakasema Kuna vita imetangazwa M23 wanaingia Leo. Hapo nilitetemeka sana, nikawaza nirudi Rwanda lakini ukaguzi na Mahojiano ya Rwanda yalinipa hofu, maana ilifika wakati nashuhswa kwenye gari nafanyiwa Mahojiano maalum . Nilishangaa Kila yulipopita nakuta askari wanajua Kuna Mtanzani Yuko kwenye gari. Nilikua nahojiwa Kwa muda mrefu mpaka abiria wanalalamika, abiria Wote walikua Wakongo na karoko mswahili Mimi, askari wa Rwanda hawamuelewi wanashangaa Mtanzani kupitia pale.

Sasa Hali Ile ilinipa hofu ya kurudi Rwanda na nikakumbuka adhima yangu Bado, safari yangu Bado na lazima nifike.

Hapo nilisajili lakini ya Simu na kuweka vocha niajiunga mitandao yote na kupata dakika 3 Kwa Buku...
Haraharaka nikapita mtu wa toroli wao wanapita shareti, nikapakia mizigo tukaelekea Bandarini. Kutoka Bukavu kwenda Guma Kuna ziwa Kivu hapo unapanda meli usiku Kucha unafika kesho Asubuhi. Lengo langu niondoka Bukavu na usiku niwe kwenye meli ili hata vita ikitokea Mimi nakua kwenye meli.

Bandarini nilikuta Meli nyingi ila nikaamua kupanda "Emanele04" waniita Emauele katre, hii Bei yake Iko juu na wanapanda watu wenye uwezo na mabishoo. Lengo langu nilitaka kuanza kukutana na watu ambao wanaweza kunipa michongo ya machimbo au kupata connection za dealer wazuri. Katika safari yangu nilikua mkimya sana kwani Kila nilipo jaribu kuongea watu waligeuka kunitazama, nikagindua Kiswahili changu kinaniumbu jambo ambalo sikulitaka hasa kulingana na treatment ya Wanyarwanda.

Usiku niliingia Club na kukaa Kwa muda Kisha nikarudi, mpaka wakati huo sikupata mtu wa kuanza mazungumzo naye. Tukiwa njiani upande Moja nchi kavu kulikuwa Giza huko ni Congo kisiwa kinaitwa Idjwi na upande mwingine Kuna mataa sana, huko ni Rwanda na mataa yale ni miji na vijiji.

Asubuhi tulifika Bandarini Goma. Hapo nilikuwa makini kuangalia watu wenye mizigo kama yangu hasa samaki ili nijue wanako wapeleka. Kuna dada Moja alikua na Samaki mwengi. Niliadhimia kujiweka karibu yake. Wakati anapakia kwenye gari kupeleka stoo ndipo nikasogea na kumuomba anipakilie Mzigo wangu nitachangia garama, dada yule alikubali na Alipo niuliza napeleka wapi nikamwambia Kuna mtu tutamkuta hapo mbele ndiye anajua stoo ilipo, lakini haikua kweli.

Tulienda mpaka nakoenda yeye, na tukiwa njiani nilikwambia ukweli kuwa sina stoo Bali nimekuja tujaribu biashara. Alipo niuliza Bei za Samaki Tanzania nilimdanganya nikamwambia Bei ya chini sana kiasi akawa anatamani nimpeleke huko chimbo. Leongo langu lilitimia na tulipo fika stoo kitu cha kwanza alimueleza mume wake kuhusu Bei za Samaki Tanzania na kuanzia hapo hao wakawa weneji wangu. Kesho yake nilizunguka mjini Goma mpaka sehem inaitwa Bireree hapo ni mjini na ndipo mpakani na Gisenyi Rwanda, yaani border Ile Iko kama ilivyoisha Tunduma na Nakonde Zambia. Nyumba zimeungana za Rwanda na Congo. Soko na mishe nyingi ziko upande wa Congo . Asubuhi Wanyarwanda wanavuka kufungua biashara zao huko Goma ni jioni kurejea kwao.

Screenshot_20230127-165639.jpg
 
Attachments

  • Screenshot_20230127-165416.jpg
    Screenshot_20230127-165416.jpg
    55.5 KB · Views: 83
  • Screenshot_20230127-165348.jpg
    Screenshot_20230127-165348.jpg
    72 KB · Views: 70
.
Katika harakati zangu za kujikomboa na umasikini, niliamua kufanya ziara ya kusaka fursa Mpya nchini Congo. Nilikua tayari nimeshapata masimulizi mengi ya upatikanaji wa madini ya dhahabu na Rubi.

Ni mnamo mwaka Juzi mwanzoni nikiwa mji wa Uvira amabapo jilikutana najamaa Akiwa na jiwe alilo dai kuwa ni Rubi

View attachment 2497370
Baada ya mazungumzo marefu jamaa alikubali kunipa jiwe Moja ambalo alisema kuwa alishawahi kulipeleka Kigali Rwanda lakini katika vipimo ilitoa majibu yanayo Changanya. Ilisoma upande Moja ni Rubi na wakati mwingine inasoma Spinel. Sasa akanionesha ndoo imekaa mawe ya Kila namna. Kazi yangu nilitakiwa kwanza kwenda Tanzania kupima jiwe hilo ili tujue ni aina Gani ya jiwe Kisha nitafute mteja wa Uhakika ambaye tutakuwa tunampa Mzigo.

Kazi hiyo nikaichukua na kuanza safari, sikuhiyo nililala Bujumbura na keshoyake nikalala Kigoma. Asubuhi nilianza safari mpaka Arusha. Pamoja na kuzongwa na matapale na kashkash nyingi nilifanikiwa kufanya vipimo na bahati mbaya jiwe lilikua feki .
Pale Arusha nilikutana na wadau wengi sana na kupewa michongo nankutiwa moyo sana. Nilianza kuiona Dunia ya dealers. Sasa kazi ilaanza kutafuta connection ili nikasake Mzigo. Hapo ndipo safari wa Kivu kaskazini ikaanza.

Kiukweli sikuwa najua mawazo yangu ni hatari kiasi gani lakini laiti ningelijua pengine ningeanza kuungama dhambi zangu kwanza kabla ya kuanza safari katika ukanda wa damu mbichi.

Wakati ukawadia na safari ikaanza, niliambiwa nitafute biashara ya kwenda mayo ili nizugie kuingia mayo maeneo ya ndani na machimboni. Kwanza nikawaza kupeleka Nguo za kiume Jeans za masela na Viatu moka za Bakulutu na Kisha nikafikiria kupeleka Mchele. Baada tathmini jikapeleka Jeans Viatu na Samaki. Nilidhamilia kukutana na kamii ya Kila namna nanjinsia zote nilidhamilia kufa au kurudi na Mali. Militia taarifa za AWALI kujua hata mavazi ninayotakiwa kuvaa nikiwa huko. Nilihakikisha ninachukua kilataarifa Kwa uzito unao stahili.

Nilijifunza kuhisabu na kutaja pesa Kwa kifaransa, ndani ya wiki Moja nilijua kuhesabu Moja mpaka Milioni na kutaja pesa na maneno muhim ya kibiashara. Mfano Congo neno Kuuza wao linamaana ya kununua kuuu. Nipatie, kombola, mbasela na maneno mengine kama kutaja rangi na kusalimia. Bahati ni kwamba Kiswahili Cha Kivu kinafanana sana na Kiswahili Cha Tanzania Bara tofauti na hawachanganyi sana french kama wale wa Lubumbashi na Kinshasa.
View attachment 2497368
Safari ilianza Kwa kupitia Burundi Kisha kuingia mji wa Uvira. Hapo nililala na kesho nikapanda Hiache kwenda Mji wa Bukavu. Nilikua na machaguo mawili aidha kupitia Barabara ya ndani ya Congo au kupitia Rusizi Kisha Rwanda na kurudi tena Congo.
Barabara ya ndani ya Congo ni mbaya sana na hatari sana, wanapita watu wahalifu na wanao ogopa ukaguzi wa Rwanda na ukifika unafanyiwa sherehe yaani makorongo na magari kuanguka sio habari tena, kutekwa na kuuwawa ni kawaida kuliko kusaliklmiana. Hii inaitwa Barabara ya Ngomo(Kaburi wazi)

Changamoto ya kupitia Rwanda, ukiwa na Visa ya Dola 50 basi ukiingia Rwanda Visa ya Congo imeisha na ukitaka tena kuingia Congo Kwa kutokea Barabara mchepuko ya Rwanda basi utalazimika kulipia Visa tena, kwahiyo kupitia njia hiyo utalipa Dola 200 kwenda na kurudi.

Suluhisho ni Visa ya Dolar100 ambayo unapewa miezi mitatu na unaweza kutoka Congo na kuingia kadili uwezavyo. Hilo nilisha lifuatilia mapemaa, nikawa na Visa ya Dola100 nikapita Rwanda. Kuna mengi hapa Rwanda lakini kwakua sio mada ya Leo itoshe kusema ni Dunia tofauti sana. Tuishi bongo tu, amani inatosha .

Sasa niliingia mjini Bukavu kupitia mpaka wa Rusizi. Pale Bukavu wakati nimeingia nikakuta watu wanafunga maduka na kukimbia kujificha, nilipojaribu kuuliza wakasema Kuna vita imetangazwa M23 wanaingia Leo.

Hapo nilitetemeka sana, nikawaza nirudi Rwanda lakini ukaguzi na Mahojiano ya Rwanda yalinipa hofu, maana ilifika wakati nashuhswa kwenye gari nafanyiwa Mahojiano maalum . Nilishangaa Kila yulipopita nakuta askari wanajua Kuna Mtanzani Yuko kwenye gari.

Nilikuwa nahojiwa Kwa muda mrefu mpaka abiria wanalalamika, abiria Wote walikua Wakongo na karoko mswahili Mimi, askari wa Rwanda hawamuelewi wanashangaa Mtanzani kupitia pale.

Sasa Hali Ile ilinipa hofu ya kurudi Rwanda na nikakumbuka adhima yangu Bado, safari yangu Bado na lazima nifike.

Hapo nilisajili lakini ya Simu na kuweka vocha niajiunga mitandao yote na kupata dakika 3 Kwa Buku...

Haraharaka nikapita mtu wa toroli wao wanapita shareti, nikapakia mizigo tukaelekea Bandarini. Kutoka Bukavu kwenda Guma Kuna ziwa Kivu hapo unapanda meli usiku Kucha unafika kesho Asubuhi. Lengo langu niondoka Bukavu na usiku niwe kwenye meli ili hata vita ikitokea Mimi nakua kwenye meli. Bandarini nilikuta Meli nyingi ila nikaamua kupanda "Emanele04" waniita Emauele katre, hii Bei yake Iko juu na wanapanda watu wenye uwezo na mabishoo.

Lengo langu nilitaka kuanza kukutana na watu ambao wanaweza kunipa michongo ya machimbo au kupata connection za dealer wazuri. Katika safari yangu nilikua mkimya sana kwani Kila nilipo jaribu kuongea watu waligeuka kunitazama, nikagindua Kiswahili changu kinaniumbu jambo ambalo sikulitaka hasa kulingana na treatment ya Wanyarwanda.

Usiku niliingia Club na kukaa Kwa muda Kisha nikarudi, mpaka wakati huo sikupata mtu wa kuanza mazungumzo naye. Tukiwa njiani upande Moja nchi kavu kulikuwa Giza huko ni Congo kisiwa kinaitwa Idjwi na upande mwingine Kuna mataa sana, huko ni Rwanda na mataa yale ni miji na vijiji.
Asubuhi tulifika Bandarini Goma.

Hapo nilikuwa makini kuangalia watu wenye mizigo kama yangu hasa samaki ili nijue wanako wapeleka. Kuna dada Moja alikua na Samaki mwengi. Niliadhimia kujiweka karibu yake.

Wakati anapakia kwenye gari kupeleka stoo ndipo nikasogea na kumuomba anipakilie Mzigo wangu nitachangia garama, dada yule alikubali na Alipo niuliza napeleka wapi nikamwambia Kuna mtu tutamkuta hapo mbele ndiye anajua stoo ilipo, lakini haikua kweli..

Tulienda mpaka nakoenda yeye, na tukiwa njiani nilikwambia ukweli kuwa sina stoo Bali nimekuja tujaribu biashara. Alipo niuliza Bei za Samaki Tanzania nilimdanganya nikamwambia Bei ya chini sana kiasi akawa anatamani nimpeleke huko chimbo. Leongo langu lilitimia na tulipo fika stoo kitu Cha kwanza alimueleza mume wake kuhusu Bei za Samaki Tanzania na kuanzia hapo hao wakawa weneji wangu.

Kesho yake nilizunguka mjini Goma mpaka sehem inaitwa Bireree hapo ni mjini na ndipo mpakani na Gisenyi Rwanda, yaani border Ile Iko kama ilivyoisha Tunduma na Nakonde Zambia.

Nyumba zimeungana za Rwanda na Congo. Soko na mishe nyingi ziko upande wa Congo . Asubuhi Wanyarwanda wanavuka kufungua biashara zao huko Goma ni jioni kurejea kwao.

View attachment 2497412
Hapo ni katikati ya mji wa Goma. Sanamu la Chukudu kama alama za vijana kuchapa kazi.

Nilitumia siku tatu nilizo Kaa hapo Goma ili kukusanya intelijensia muhim Kwa safari yangu. Nilioewa masimulizi ya vita na uharifu. Mji wa Goma mpaka Sasa uko Chini ya utawala wa Kijeshi.

Pale hakuna mbunge wala mkuu wa Mkoa. Niuongizi wa Kijeshi, hii ni sababu mji wa Goma na wilaya zake ni ukanda wa Vita na machafuko Kila wakati.

Pale nilishuhudia kusikia Simulizi za YouTuber wa Tanzania Denis Mpagaze zikipigwa redioni akisikuli mambo ya uzalendo Kwa Afrika.

Pia Kuna redio ya watu wanajiita Kimbanguist hao wanarusha hotuba za Magufuli na kumtaja kama shujaa wa Afrika. Wakati huo Stori za Magufuli zilivutia sana na nikama ukimzungumzia vizuri tu, hapo niliwasoma mapema Wakongo nikawa namsifia Magufuli basi wakanipenda na kupata marafiki.

Nilianza kuoneshwa askari waasibwa maimai wakiwa mtaani kama raia wa kawaida tu.

Mji wa Goma umefimikwa na mawe ya Volcano na nyumba karibu zote zimejengwa Kwa mawe ya Volcano au mbao.

Nilifanya intelijensia yangu na kukamilisha Sasa safari ikawa ni kuelekea sehem inaitwa Walikale.

Mwanzo nilitaka kwenda semem inaitwa Beni au Butembo huko mnako sikia vita Kila siku lakini kilikua kumepigwa vita Kali sana na ADF wamechinja watu.

Pia kilikua na taarifa za watanzania kukutwa kwenye jeshi la ADF na wakatekwa. Hii ilinipa hofu nikajua huku Watanzania hautuaminiki tena na kwakua ni ukanda wa Vita wanaweza kunikamata Kwa kushakia usalama wao tu. Pia ilitakiwa nipitie mji wa Rutchuru huko M23 waliko ondoka baada ya Kenya kupeleka majeshi.

Niliambiwa tungepita Virunga na huko tunapata escort ya jeshi lakini kikinuka majeshi wanakimbia mnaachwa porini na kutekwa. Wanaume mnalazimisha kujiunga na jeshi la waasi na wanawake wanaolewa na ADF au M23. Hiyo ikatosha kiua mpango wangu.

Sasa uslekeo ni Walikale na nisafari ya wiki Moja na Sio Chini ya siku Tano. Huko wakaniambia wanafanya butter trade yaani unawapa samaki.

Pia masela wakipenda jeans hasa zile zenye mapichapicha basi wanakupa Madini hasa dhahabu na hapo mnakadiliaana tu.

Huko ikawa changua Bora. Kitu ambacho sikuzingatia ni usalama wa Barabara na aina ya usafiri. Mawazo yangu yalikua kwenye Madini tu. Safari ikawadia nikiwa na yule dada wa samaki mwenyeji wangu. Wakati huo Wote sikuwa nimemueleza lengo la safari yangu, yeye alikua anafurahi kuja Tanzania kuzoa samaki Kwa Bei Chee. Alinipa Kila msada ilimradi tu niwe na amani.
Siku ya safari Tulienda sehem inaitwa KwaAroxii , hapo tulikuta Maroli mengi aina ya Mercedes Benz Actros yakiwa yanapakia. Magari yalikua wazi Kwa Nyuma na hayana Bomba.
Hapo mizigo inapakiwa mapaka juuu, Kisha watu wanagombania kukaa juu ya mizigo. Nilijaribu kupya sehem nzuri lakini nilishindwa. Nilijibana Kwa mbele hapo nilikaa kwenye body huku miguu ukiwa juu ya Cabin juu ya dereva. Gari likinesa miguu inaning'inia na kutua juu ya Cabin, napo nimekalia tako Moja. Nilijibana sana nikakaa katikati. Safari ikaanza na hapo sikujua kumbe tulikua tunaingia Dunia ya wafu, huko kufa ni kawaida kuliko kuishi, Wanasema Zone rujhe yaani Red zone au Ukanda wa Damu.
Baada ya safari ya kama kilomita 50 tulikua nje ya mji wa Goma na hapo tulikuta Kuzuizi Cha jeshi. Hapo wanakagua Kila mtu kujua anakoenda na anaenda kufanya nini. Nilijaribu sana kukwepa lakini ilitoka amri ya wanaume Wote kushuka Chini.
Yule dada alinisogele na akasema ukiulizwa waambie Mimi ni mke wako tunakwenda kusalimia ukweni. Ikafika zamu yangu kupekuliwa, pesa nilikua na karobia Dola 500 nimezificha kwenye begi ambalo yukonalo yule dada.
"Peti yakawa,...... , Hapo ilimwagija lingala ya vitisho na walipooona sijibu Moja alikua pembeni alikoki silaha yake. Na kusogea pembeni, moyo ukienda mbio nikajua anataka kunifyatulia risasi. Niliamua kuongea Kiswahili Cha Tanzania pure, na hapo wakajua Mimi ni mbongo. Yule askari akamzuwia mwenzie nabkumuita. Jamaa alikua ananuka Bangi na pombe, gwanda zimechoka vibaya. Taarifa kuwa Kuna Mtanzani zikasambaa wakaanza kukusanyika. Dakika mbili mbele ikatoka amri nikaonane na Mkuu wako "Weye kuya hapa Kwa shefu" kilikua na Banda la turubai pembeni huko yupo boss wao. Nikaingia Kwa kuinama. Huko nilimkuta jamaa mstaaarabu Akiwa amezungukwa na walizi.
Pembeni kulikuwa na vijana wanne watusi na walikua wameshakiwa kuwa ni M23. Simu zao zilikiua Inapekuliwa nankukutwa picha zao wakiwa na kombati za jeshi la Rwanda. Gafla wakatolewa nje, nikiwa mle ndani nikihojiwa gafla ilisikika mlio wa risai. Yule boss aligundua hufu yangu, akaniuliza "weye mtanzania unaenda huko huyo bibi yako hayakuambia kama kule ni fasi ya mubaya?" Mikamwambia kuwa ninajua lakini titawahi kurudi haraka. Jamaa aliniomba Hela ya bia nikampa Franga 2000. Kitu inatakiwa kujua ni Askari wa Congo hawaombi Hela nyingi.
Nilipotoka nikakuta nasubiriwa Mimi peke yangu. Wale M23 sikujua nini kimewakuta zaidi ya ule mshindo wa chuma.
Safari ikaendea mpaka mji wa Masisi hapo ni kama mwisho wa kuona majumba, Sasa tunaanza milima na maporomoko ya msitumi. Huko utakuta vibanda vya Nyasi Kandi ya Barabara na askari wa Serikali wako hapo wanafanya doria. Baada ya kutembea kama kilomita 200 tulikua uwanda wa juu sana, baridi na upepo mkali. Nilianza kuona makundi makubwa ya ng'ombe wanao lindwa na walizi wa kitusi. Nilipo uliza nikaambiwa kuwa hao ni ng'ombe wa Raia Joseph Kabila. Wengine walisema ng'ombe wa Kagame. Tumesafiri zaidi ya kilomita 100 tukiwa katika ya makundi ya ng'ombe. Safari iliendelea mpaka kufika saa tatu usiku tulifika katika mji wa KITCHANGA, mji huu ambao M23 Leo wameuteka. Hao ni mji muhim sana kwani unaunganisha miji ya Goma na Bukavu Kwa upande wa magharibi na ni mji unao pitisha huduma ya chakula kwenda miji mingi sana. Mji huu ni kama roho ya maisha ya watu na uchumi.
Tulifika na kulala kwenye mgahawa wa mbao na wengine walilala nje. Hapo Kuna baridi Kali sana. Ilipofika usiku wa manane ilitoka amri ya kuzima mataa na kukaa kimya. Tulishangaa bila kujua kinachowndelea. Yule mama mmiliki wa mgahawa alijisahau kuzima taa chumbani mwake, kumbe wajuba waliona mwanga Kwa nje. Dakika chache baadae vilisikika vishindo vikumbwa sana na sauti za kiume ambazo ni kama walikua wakiimba huku wamefunga midomo. Wakiimba na kupiga vishindo Kwa pamoja na kuitikia Kwa kuunguruma. Tulipata hofu sana. Walikuja na kuzunguka Ile mgahawa wa mbao. Yule mama akatueleza kulala Chini sakafuni na tusikijitikise Kisha akajitosa yeye kuokoa maisha yetu. Wakamuamuru kuzima taa Kisha wakondoka naye kusikojulikana. Yulikaa mpaka asubuhi tukiwa na hofu sana.
Ilipofika asubuhi yule mama alikuja na kuomba tumchangie pesa ili anunue mbuzi wawili wa faini. Akatueleza kuwa wale walikua ni wazee wa Mila wanafanya tambiko la mji ule na kukutwa hajazima taa ni kosa na wangejua mule Kuna wageni basi tunguwawa. Anasema wale wajuba walikua na vichwa vya watu vimetungwa kwenye miti na kule walipo mpeleka alishuhudia wanazika mtu Akiwa hai inagwa hakumjua yule mtu. Yeye walimzuwia wakasema atakesha nao na kesho saa sita apeleke mbuzi wawili Kwa chifu wao. Tulipo muuliza akasema ni kawaida kufanya Tambiko Kila ifikapo mwisho wa mwaka. Na sikuile ilikua siku ya Tambiko.
Hapo KITCHANGA Kuna sananu la mwanamke linaabudiwa na linabadilishwa Nguo Kila mwaka.
Safari iliendelea na huko mbele kadili tulivyokua tukisogea ndivyo tulikua tunazidi kukiendea kifo. Hapo KITCHANGA ndio mwisho wa kupata internet na mpaka hapo sikuwa na mawasiliano na Ndugu zangu nilipiga simu za mwisho na kutoa malekekezo Kwa kina katika Kila jambo langu. Nilikua kama naaga au kutoa wosia wa mwisho bila ndugu zangu kujua. Nilikata tamaa ya kurudi hai, tulikua tayari katikati ya makundi zaidi ya 20 ya waasi na magenge ya watekaji. Wenyeji walionekana kuwa na hofu huku Mimi nikiwa hoitaabani. Masimulizi ya ujambazi na vita yalitawala, tulipita maeneo yenye Kila kumbukumbu ya mauaji. Jambo la kushangaza ni kuwa huko ni kama tulikua tumevuka mpaka na kuingia Rwanda, watu wanao ongea Kiswahili walizidi kupugua na wengi walibaki waliokua kwenye gari. Tulianza kupitia vijiji vya Watusi na vijiji vya wahutu Wote kutoka Rwanda. Hofu ilizidi kutanda.Tulifika sehem inaitwa Mweso, hapo ni Kambi wa wakimbizi wa Rwanda ambao wameshafanya Kijiji na Kuna Kambi ya Majeshi ya MUNOSCO na ofisi za nji nyingi zenye Operation zao Congo. Mabango ya UN,UNICEF , USaid na Japan aid na Kila shirika la kimataifa basi liko hapo. Pomoja na hivyo haizuwii kitu sababu hao Wote hawaingilii mapigano yoyote.
Tulipumzika hapo kidogo Kisha safari iliendelea.
Kabla ya kukiacha hiki Kijiji dereva alisisimama sehem watu wakashuka kuchimba dawa na Kisha wakakusanyika na kuanza kuomba Mungu. Kitendo hicho kilinipa hafu ambayo sijawahi kuipata na kwamara ya Kwanza nikatamani kurudi Nyuma , niliuliza kama naweza kupata usafiri lakini wakasema mpaka gari hilo lirudi hivyo hakuna kurudi Nyuma. Yake maombi sikutaka hata kuuliza maana waliomba Kwa Kiswahili na ni kama ilikua Sala ya toba na kukabidhi roho Kwa Muumba...
Itandelea

Sehemu ya Pili:
Kwanza niombe radhi Kwa uandishi mbaya. Mimi sio mziefu wa kuandika Stori ndefu hasa hapa jf.Pia sikua na maandalizi ya kuandika hii Simulizi, nilijikuta naandika baada ya M23 kuuteka huo mji wa KITCHANGA. Naamini Mimi ni miongoni mwa Watanzania wachache wanao elewa uhalisia na hatari ya hao M23 hasa wa hatua waliyo fikia.Imagine mpaka hivi navyandika Bado nawasiliana na watu walio mafichoni huku risasi zinasikika. Kuhusu mawasiliano huko Congo ni gharama sana kupiga simu.Fikiria Shikingi miatano unajiunga SMS tatu, labda kama wamebadilisha Jana.
Ni rahisi kutumia Whatsap Congo na hata raia wengi wanalizika kuwa na smart phone ili kurahisisha mawasiliano.
Kwa mtu anateijua eneo la KITCHANGA kama unaelekea Mweso hapo Kuna barrier ya wanajeshi na mbele Kuna mto ambao unawakuta akinamama na watoto wanaoga na kufua na wengine kuchezea Maji kama beach, basi hapo ngg'ambo ya mto ndiko yalipo majeshi ya selikali na upande wa pili wapo M23. Mapigano makali wanatunguana live live. Kupoteza mji huo ni pigo kubwa sana, Kwa Congo na washirika wake.**********************************
Sasa tuendelee pale tulipoishia. Ni kwamba baada ya watu kuanza kuomba na kusali pale nilijua kabisa tunako elekea ni kugumu zaidi. Nilijitahidi sana kuficha hofu yangu. Tangu mwanzo nilijitahidi sana kuficha utambulisho wangu, sikuwa tayari Kuonesha passport yangu kirahisirahisi. Hata uvaaji nilijifananisha na watu wa huko. Nilivaa kofia muda Wote, nguao nilivaa chafuchafu na koti lango huku usoni sikutaka kunawa wala kipaka mafuta ili nindelee kufanana nao. Ingawa Kwa ukaribu mtu aliweza kuona utofauti wa ngozi ya mkono wangu kwani kidogo ilionekana kuwa angafu kidogo ndiomaana sikutaka usoni nionekane angavu.
Hapo tulipo tayari nilikua nje ya intelijensia yangu niliyo ifanya,maana sikujua kama hatari iko Kwa kiasi hicho.
Watu Wote walipanda kwenye gari na safari hii kidogo hakuna mbanano na tayari nilishatokan kule juu ya Cabin nankukaa Nyuma karibu na yule dada mwenyeji wangu. Yule dada alishajua Jina hofu na hata yeye alikua na hofu lakini alijaribu kuficha hofu yake ili kunitia moyo Mimi.

Safari ilianza huku watu wengi wakiwa kimya. Kitu Cha ajabu ni kwamba Kila sehem tuliokua tunapita basi Kuna mtu anakumbuka tukio flani la uhalifu lilio mtokea katika eneo hilo. Basi kumbukumbu hizo zikawa zinawalazimu kuanza kusimulia MATUKIO. Yule dada alijaribu kuniuliza habari za Samaki huko Tanzania nami nilimjibu lakini sukwa makini naye sana. Masikio yangu yalikua kwenye kusikiliza Stori za Mikasa ya hilo eneo. Kila mkasa uligusia watu kufakufa tu. Ni mkasa Mmoja tu amani ilikua wa kutia moyo angalau.
Hapo kulikuwa na mama Mmoja mcheshi sana yaani yeye alishakomaa roho na MATUKIO mpaka anaona kawaida. Huyo anaitwa Nyabadee, yaani huko Congo neno badee inamaana ya wawili Sasa huyo Nyabadee ni mama aliyezaa mapacha ambapo Kwa Tanzania wanaitwa mamawawili.
Tulifika sehem flani Kuna korongo hapo gari inapunguza mwendo na ni sehem rahisi Kwa majambazi kuteka magari na kuwavua watu Nguo na kupora. Hapo watu walikua kimya wakisubiri lolote hasa amri ya kusimamisha gari au mlio wa risasi, lakini Kwa mama Nyabadee yeye akifika sehem yake ya matukio. Hapo bila woga akaanza Simulizi yake, kuwa wiki mbili zilizo pita hapo alipambana na jambazi Mmoja na wakampokonya silaha. Alikua yeye na dereva bodaboda wakitoka huko tunako elekea kurudi Goma, ndipo walipofika hapo wakamkuta jambazi maarufu wanamwita kadogoo. Huyo kadogoo alikua na kundi lake la vijana wadogo naye alikua mkuu wa hilo kundi. Wao wanaishi kwenye msitu huo na kufanya ujambazi wao. Wanaamini kadogoo ni jambazi anaye tumia uchawi Kufanya ujambazi wake. Badi Nyabadee nasema walipofika wakakuta huyo kadogoo na kijana wake Mmoja wakiwa na silaha Moja. Baada ya kuwasimamisha, kadogoo bakaomba pesa na chakula. Nyabadee hakuwa tayari kutoa pesa.Baada ya Mabishano ndipo Nyabadee alimrukia kadogoo na kumkaba shingoni na kuanza kupigana. Hali ikawa mbaya Kwa kadogoo,akatoa amri Kwa yule kijana wake afyatua risasi ili amuue yule mama Nyabadee. Lakini yule kijana alishindwa sababu hakikua na ukutuvi maana angeweza kuwau Wote. Ikabidi yule kadogoo akurupuke nankukimbia Kisha yule kijana akamfuata Nyuma na kutokomea porini. Hapo utajiuliza yule bodaboda alikua wapi? Ni kwamba hao bodaboda wa hayo Maeneo ni vijana wa huko na hiyo ndio kazi Yao, kwahiyo Huwa hawapendi kuingia kwenye kazi za watu. Sababu wao hawapokonywi pesa wala pikipiki zao. Kwahiyo Huwa wanakaa pembeni au kusogea mbele wanakuacha umalizane na wajuba na ukitoka salama basi anakuja kuchukua safari inaendelea. Jambo la muhim Kwa hao bodaboda wao wanachukua nauli yao mapema.
Masimulizi ya Nyabadee yalizidi kumvuruga yule dada huku Mimi yakiniacha bila roho wala nafsi yaani nilikua nusu mfu. Niliangaza sana nila kuona dalili za nyumba wala kijiji Kwa mbali au karibu. Kilikua na ukimya kiasi kikubwa huku watu wengi wakiwa amejiinamia.
Nilitamani niulize mambo kadhaa lakini Kila mtu alikua anaoneka kukata tamaa, nata Nyabadee Sasa alikua kimya. Ukimya ilizidi sana kiasi hata uendeshaji nao ukawa wa taratibu sana, hago ilizidi sana. Ikafikia hatua nikaanza kuangalia Kila pande ya Barabara kuanzia karibu mpaka mbali, niliwanza namna gani nitafanya endapo tukivamiwa. Nilianza kuangalia semem ya kukimbilia iwapo italazimika, moyoni nilishaamua kuwa ikiwa litatokea lolote basi Bora nife nikiwa nakimbia kujiokoa. Nilichukuo begi langu na kuitoa passport Kisha nikaiweka mfukoni. Kisha nikavyaa Viatu na kukaza vizuri. Hapo nikawa kamili Kwa lolote.
Baada ya mwendo kama wa dakika 45 tulikua tunakaribia sehem yenye vijumba vya Nyasi. Vilionekana Kwa mbali kidogo. Niliona vibanda kama vitatu na kimoja kama turubai la Bluu.
Tulivyozidi kukaribia ndipo nikaona Kuna askari wawili Kwa nje na wengine kama sita wako Nyuma ya Banda la turubai. Tulipozidi kukaribia niliona kulikuwa na kizuizi njiani na hapo dereva akasimama. Nilishindwa kufurahi wala kuhofu maana sikujua hao ni akina nani. Lakini Kwa namna walivyokua Na makazi kama ya kudumu sana, milihisi hao itakua ni mojabya jeshi aidha serikali au waasi, lakini sio majambazi.
Amri ilitoka ya watu Wote kushuka Chini. Ajabu ni kwamba hakuna aliyeshuka haraka, Bali watu walikua wanazugazuga na sikujua kwanini watu hawashuki. Binafsi nilitamani tushuke ili kama Kuna zoezi lifanyike bila kuanza kusukumana.
Kumbe pale watu walitaka dereva aende kuwapoza wale jamaa ili kuokoa changamoto za watu Wote kukaguliwa. Hilo niliona ni jambo jema maana Mimi pia sikutaka kukaguliwa wala kutambulika. Walu walianza kuongea wanamwita dereva Kwa Jina la "Chofe" ili aende akamalizane nao.
Kitendo Cha dereva kukawia nacho kiliwaudhi wali amajamaa, kumbe walitaka kushusha watu Wote ili dereva aende kuongea nao kama njia ya kuokoa muda na kuhakikisha abiria wake wanakua salama. Lakini dereva sijui kwanini alikawia wakati anajua wao jamaa. Labda sababu ndio sehem yake ya kazi na alifanya mazowea. Sasa kibao kikageu kwa dereva, jamaa walimshusha Kwa nguvu na kuanza kumpiga. Dereva alipigwa kitako Cha bunduki mpaka kuanguka Chini. Watu Wote kimyaaa. Walimburuta mpaka Nyuma ya kijumba walipokua wale sita.Kipigo kiliendelea huko Kwa muda kukawa kimya. Yule mama Nyabadee ndipo akaanza kuongea na wale askari, alishuka kwenye gari na kuwasogelea, Kisha baadabya dakika mbilitatu yule mama alirudi na kuanza kuchangisha pesa. Mimi nilitoa Franga 2000 na wengine walitoa walizokuwa nazo. Kisha yule mama akaenda kuwapelekea.
Zilipita dakika kadhaa ndipo dereva yule akarejea huku akionekana Kuchoka sana.

Safari iliendelea, huku Nyabadee akiendelea na Stori taratibu na kupata wachangiaji wachache sana tofauti na awali. Hii ilinipa picha mbili kuwa aidha Bado tuko sehem hatari au watu wakechoka. Lakini kwangu nilikua na vyote mchoko na hofu.Baada ya kuuliza niliambiwa kuwa wale ni FARDC yaani askari wa keshi la Congo. Wao walitaka kukufanyia mbaya basi wanakupa uhusiano na M23,Maimai au Isamic state ilimradi tu wakuvishe ubaya Wote kutimiz malengo yao na hasa kukupora. Kule Congo kunakuwa na majambazi ambao wanamiliki maeneo yao ya utawala na wanapeana mipaka na jeshi la serikali na inasadikika kuwa hao wanajeshi ndio wanawapatia silaha majambazi wapige kazi Kisha wanagawana au wanajeshi ndio wanao fanya ujambazi.
Kuna sehem tulifika na Kila mtu kwenye gari alikua na neno la kusimulia. Hapo Wanasema kilikua na kundi Moja ambalo ni hatari sana na karibu Kila Mmoja tayari mewahi kukutana nao hao majamaa. Dalili zilionesha hao ni hatari kuliko Wote. Jambo pekee la faraja ni kuwa hao jamaa walihama kurudi kule Nyuma yulikotoka. Angalau hiyo ilikua habari njema kuwa nitafika niwndako Ingawa sijui kama nitarudi salama.
Kumbe ilikua ni faraja ya muda tu, Sasa tulikua yimeanza kuona dalili za uwepo wa Kijiji Kwa mbele. Hapo Kuna kijiji kimoja kinaitwa Kashuga. Hapo Kashuga ni sehem hatari kuliko zote Kwa ukanda huko, na angalau ndio sehem pekee tunaweza kusema ndipo kekee inapoishia hewa ya uhai na baada ya hapo hata mita 100 unakua imeingia kuzimu.

Tulianza kusunguka mlima Kwa kukata kulia na kushoto kote tukizunguka mlima. Mpaka tulipoanza kuona mabango ya UNHCR na UNICEF. Kwa mbele tulianza kuona vijumba juu kidogo ya mlima hapo Kuna mto katihati ya Kijiji. Tulizidi kusogea na kuona mabango ya COVID-19 wao wanai Kovide diznefu, au Konora virisi. Pia mabango ya kipindupindu yalikua mengi. Sasa tulikua timeanza kuingia kijijini. Hali ya hewa ya ukungu ulio funika milima na baridi Hali iliyo changiwa na upepo wa gari. Hapo angalau nilikua nimefanana naonkwa kiasi kikubwa na huku tayari midomo yangu imekauka mpaka kipasuka.Kwenye bagi nilikua na chipa la Maji lakini sikuweza kuyanywa hadharani sababu wangeanza kumiona wakuja.
Kijiji kilikua na nyumba za mbao tupu. Hakukua na gari lolote zaidi ya gari letu.
Tulipokua tukiingia kijijini, kundi kubwa la watoto walilikimbilia gari kama vile mapokezi ya wanasiasa, hio ikanipa picha kuwa huko gari ni adimu sana kwenda.
Tulifika mpaka maeneo ya sokoni na gari likasimama. Kuna kitu sikuwa makini nacho,wakati gari linasimama ni kwamba dereva alikeuza gari na kuangalia tulikotoka. Kumbuka wakati Wote nilikua naangalia mazingira ya Kila sehema ili ikitokiea lolote nijue wapi nakimbilia. Sasa kutokana na shangwe za wanakijiji kuona lile gari nilizama katika mshangao na gari lipo geuka sikujua. Sasa Mimi nikakalili uelekeo wa gari kama sehem ya mbele na huku Nyuma ndiko tulipotoka. Kumbe uelekeo wa gari ndio tulikotoka na nyumabya gari ndiko tunako elekea. Kijiji hicho Kiko katikati ya milima mitano yaani Kijiji kimekaa kama kwenye beseni au bakuli.
Baada ya kushusha mizigo yetu, Tulienda kwenye mgahawa kutafuta chakula. Yule mama alikua anajua migahawa miziri angalau. Pale tulikuta ugali wa Muhogo na Ngozi ya ng'ombe. Yes Ngozi inapikwa na inalainika kama maini, Kisha inachanganywa na Sombe huku tunapita kisamvu au majani ya Muhogo. Kiukweli nilitamani kula chakuta tofauti lakini nililetewa ndizi hizo sijui zilipikwa Kwa Maji gani, ndizi nyeusi balaa. Ikabidi nirudi kwenye ugali na Ngozi ya ng'ombe.

Katika kile kijiji nilishangaa kuona watoto Wana miguu imeliwa na funza sana mpaka kwenye vidole vya mikono. Kichwani Wana vibarango na mwilini ukurutu flani mweupe na mipasuko ya vidonda. Ilifikia hatua mpaka naogopa kugusana na mtu nikihogia kiambukizwa ukurutu. Wakubwa wamedhoofu sana na watoto Matumbo ya utapoa mlo. Ni Kwa mara ya kwanza naona watu wanakupa vumbi la dagaa lililo na mchanga waenda kupika.

Hapo Sasa nilianza kusahau madhila ya njiani na akili ikarudi kwenye lengo langu la kutafuta mawe.Kumbuka yule dada sikumwambia dhamila halisi ya safari yangu, Bali yeye alikua Mimi natafuta soko la Samaki na mguo. Hapo Sasa nilipunguza nguvu kwenye maswala ya samaki na Nguo na kuongeza umakini katika kuzisoma nyuso za watu ambao nahisi wanaweza kunipa ABC za kupata dealers. Baada ya muda kupita soko lilikua limechangamka sana na uuzaji wa samaki ukapamba moto hivyo nikawa sina hudi kurudisha umakini hapo. Wakati tukiendelea kuuza nilimuuliza yule dada kuhusu akinamama wanaonkuja na dhahabu kubadilisha na Samaki. Alinijibu kuwa anawafaham na wakifika atanionesha. Hapo nilifarijika nikajua Sasa nimefika kwenye chimbo la Uhakika.Muda ilizidi kusonga bila kuona mtu akileta dhahabu.

Kile kijiji baada ya kuuliza zaidi kwanini watu wako dhoofu sana, niliambiwa kuwa hapo ilikua Kambi ya wakimbizi ambayo ni kama walitelekezwa kulingana na Hali Tete ya usalama na maofisa wengi walirudi kule Kijiji Cha Nyuma Cha Mweso. Hivyo watu ilibidi waanze kijitafutia chakula na ndio huko hata yake makundi ya uasi na ujambazi ni watoto wa huko.
Sasa hiyo habari haukunipendeza na hata ule uchangamfu ulipotea. Nilijilaumu kwanini nilipofika nilipunguza umakininwa kujifulicha ilihali sijawahua hao wakazi ni watu wanamna gani.
Milihisi tayari watakua wameshanishtukia.
Tuliuza sana samaki mpaka yule dada akawa anaacha kazi yake nakuja kunisaidia kurudisha chenji. Tatizo nikuwa Pesa ya Congo ni Chafu sana yaani noti imechakaa mpaka inanuka. Noti imechafuka mpaka maandishi yamepotea, Sasa ikawa inanisumbua kurudisha chenji. Pia nilikua naogopa hata kukamata pesa zilizotoka kwenye mikono Yao iliyojaa ukurutu.

Hivyo vijiji vyote kuanzia KITCHANGA kwenda mbele vimejaa watu waliotoka Rwanda. Na hata Lugha hapo ni Kinyarwanda na Kiswahili kidogo. KITCHANGA hii iliyotekwa na M23 pamoja na hapo Kashuga ni maeneo ya Wahutu na hapo katikati Mweso ni maeneo yaliko na mchanganyiko wa hahutu na Watusi wengi, Sishangai kuona ofisi za UN na Mashirika ya Misaada yaliwekwa hapo sababu inaaminika hayo Mashirika yako Kwa maslahi ya Watusi ndio maana unaona M23 wanapata Nguvu. Tuachane na huko sio lengo letu Kwa Leo.

Sasa yule mama ilipofika mida ya saa kumi alasiri nikamuuliza tena kuhusu wale wamama wa dhahabu za kubadili na Samaki. Akasema kuwa amepata taarifa kuwa hawakuja sokoni sababu njia imechafuka, Kisha akajifanya kama Amekua bize nammambo mengine. Huku Mimi nikiwa Bado na kiu ya kujua njia imechafukaje lakini hakuonesha kunipa umakini, nikamuacha.
Tuliuza samaki mpaka zikaisha, haku Mimi nikiwa shingo upande maana sijaona wadau wangu wa kuleta dhahabu.
Hiyo ilikua ni Desember 30 yaani Bado siku Moja kufika mwaka mpya. Kwa desturi ya Wakondo ni kwamba mwakampya wanaoita Bonanee au Fete, ndio sikukuu inayopewa heshima kuliko Christmas. Sasa ni kama ilikua maandalizi ya fete yanapamba moto, Sasa Kwa ila biashara ya Nguo nayo ilikua kuafaka sana.

Ilipofika jioni mvua ilianza kunyesha sana ikabidi tujikinge kwenye Banda kubwa la hapo sokoni. Tulibanana sana na watu wenye ukurutu ulio lowana na amani ikaniisha. Hapo nikapata nafasi ya kumdadisi zaisi yule dada. Sasa ilibidi aniweke wazi
"Unajua hapa tulipo ndio sehem ya mwisho yenye amani, unaona huo mlima Kwa Nyuma kuna mapigano makali sana na hata lile gari letu limepelekwa kubeba maiti na majerudi. Sasa wake akinamama wanatoka Kwa mbele kidogo ya huo mlima, wameshindwa kuja sababu ya vita"
Sasa leo tunalala wapi? Niliuliza Kwa sauti ya kutetemeka huku nikisikia machizi yanadondokea tumboni.
" Huwa Kuna rafikiyangu naendaga kulala kwake lakini Leo hayupo, kwahiyo tutaangalia mgahawa flani tuombe kulala hapo"

Mvua iliendelea kunyesha mpaka Giza likaigia. Watu Wote akiondoka makwao wakiwa wananyeshewa na hakukua na dalili ya mvua kukata. Tulijipenyeza pole pole huku tukitumia mwanga wa radio kuona sehem ya kukayaga. Tiliingie sehem ya kwanza wakasema hakuna nafasi ya kulaza wageni. Ile mizigo yetu tulikua tumeiweka kwenye stoo flani pale sokoni. Yaani ilikua inalinda na Mungu tu. Stoo ya mbao zimeliwa na mchwa na mchana kulikuwa na Stori kuwa Kuna wezi waliiba mizigo hapo lakini walikamatwa na kundi flani la waasi waliokua wamejikusanya hapo kama siku tatu zilizo pita.
Sasa baada ya kukosa nafasi ikabidi tuelekezwe sehem nyingine. Tulipenyapenya Kwa shida gizani mpaka kufika pale. Kisha tukaingia ndani.

- Tulipofika mle ndani yule dada alisalimia, kilikua na vijana watatu huku Mmoja akionekana kulewa sana na wawili wakiwa hawajalewa lakini walikua wanakunywa Gongo. Sasa yule kijana mlevi alikua naongeaongea sana Kwa kuropoka na maongezi yake nikama yaliwakera wake wengine, wakaamua kunywa Kwa haraka na kuondoka. Yule mlevi alikua anatukana Kwa kutaja majina ya vikundi vya waasi kama FDLR na mengine ambayo alikua anatukana wakuu wa Yale makundi.

- Sasa wake vijana wakati wanainuka tu, lahaulaa!!! Kumbe jamaa wako na bunduki mbili Kila Mmoja yakwake. Waliondoka Kwa ghadhabu na hawakulipa labda walilipaal mapema sijui. Hali Ile iliniacha katika maswali mengi ambayo sikuweza kumuuliza yeyote. Kwanza sikujua yule mlevi ni nani na kwanini wale jamaa ambalo baadae niliambiwa ni waasi wa FDLR waliinuka bila kumdhulu yule jamaa!! Hiyo ilinifanya nimuogope naye yule mlevi.

- Alikuja dada Mmoja MWENYE kitoto kidogo mgonhoni nabkutuonesha chumba ambacho unaingilia hapohapo sebuleni wanaponywea pombe.

Baadae tulimuomba chumba kingine, baada ya kumueleza kuwa sisi sio wapenzi ndipo tupatia kingine chapil. Yule dada mwenyeji wangu alienda kicho chumba nami nikaingia hicho Cha sebuleni.Yule dada aliomba Maji akaenda kuoga. Lakini Mimi hata sikuona haja ya kuoga maana Mwili ulishakufa ganzi.
Baada ya muda yule mlevi aliondoka na yule dada wa mgahawa naye akatueleza choo na bafuni Kisha anaye kaondoka.

Niliingia chumbani kwangu kulala na yule dada kaenda kuoga Kisha akarudi kulala." Mulale bye..Merci! Tulitakiana usiku mwema.Niliingia chumbani na kufunga pesa nilouza samaki katika mfuko wa nailoni. Pesa za Congo, pesa kidogo tu unakua Mzigo, Alafu noti za miatano ni nyingi sana. Unaweza kuwa na Milioni za jerojero, yaani inakua furushi. Baada ya hapo nikajilaza.

Usiku ilikua tulivu sana sana. Zaidi ya matone ya mvua ya mwishomwisho hakuna sauti hata ya ndege iliyo sikika. Utulivu ilikua mkubwa sana nikama watu Wote walikua wafu. Sikutilia mashaka kwakua ni kawaida usiku watu kulala pia utulivu kuanza mapema vile nilijua ni sababu ya mvua Ile ya jioni na baridi.
"Mikononi mwako naliweka roho yangu bwana"...nikalala.

*** Usingizi ilikua mzito sana ukizingatia uchovu wa safari za kuuza samaki sokoni, nililala kama mfu.
Muda uliyoyoma Giza likazidi kuwa zito na ukimya uzidi. Huku usingizi ukiwa umekolea, ama Kwa hakika Sasa ni usiku wa manane au wengine husema ni mida ya wanga.
- Gafla nikiwa katikati ya usingizi mzito, kwambali nilisikia kama sauti ya mpasuko wa kitu. Kwakua nilikua na usingizi mzito haikunishuulisha sana, nikazidi kulala. Ikarudia tena "Pwaaaa, Pwaaaaa.....". Gafla mishindo ikawa ya kupokezana. Nilishtuka toka usingizini kama mwehu. Sasa nilikua nimetambua Kuna ni mlio wa bunduki. Milio ilikua inapiga Kwa kupokezana kama watu wanajinishana Kwa zamu.

  • "Pwa Pwa Pwa pwaaaa..." Alafu inajibiwa Kwamshindo ambao ni mzito zaidi "Gi Gi Gi Gigi giiii ...."
  • Kumbuka Kijiji kipo katikati ya milima hivyo mshindo wa bunduki ulipokelewa na mwangwi Toka milima ile. Nikiri kusema katika dakika mbili tu nilikua sina ufaham wa kibinadami nilikua kama nimerukwa na akili. Niliwaza kuwa Sasa Mimi nakufa hakuna namna, Sasa kilichobaki ni kujaribu kujiokoa angalau nife nimejaribu kufanya lolote.

- Huku mizinga iliendelea, haukusikika sauti ya binadam yeyote zidi ya bunduki tu. Nilikua kama vile watu Wote wameshakimbia ila Mimi tu ndio nimeachwa, nikawaza labda sababu ya ugeni wangu Kuna kitu nimechelewa kufanya. Nikawa nawaza chakufanya... Hakuna zaidi ya kukimbia. Sasa nakimbia kuelekea wapi? Maana sijui wale wanaopoligana walipo. Kumbuka wakati tumefika niliiweka alama yangu Kwa kuangalia ule uelekea wa gari ili nijue tulikotoka. Sasa huko ndiko ikawa uelekeo wangu. Usisahau dereva aligeuza gari bila kujua tayari ninapooanga kukimbilia ndiko kambini Kwa waasi lakini sijui, nimeshapotezwa.
Niliwaza nikimbie na pesa na passport lakini nikimbie bila utambulisho utakao nionesha kama mgeni. Hivyo lazima begi niliache. Sasa nilichofanya mi kuvaa ngo zote zilizo kwenye begi nikazivaa mwilini. Suruali mbili zote nikazivaa. Kikavaa tisheti mbili, Sweta na koti la juu. Mwili ilikua mzito na nikabeba pesa na passport.

Kabla ya kutoka nje ikabidi nijiridhishe kama yule dada Bado yupo hai wau risasi imempitia au tayari ameshakimbia. Nilijivuta Kwa kutambaa kama jongoo. Mpaka pale sebuleni, Kisha nikaelekea chumba Cha yule dada. Nikifika nikiwa kifua Kiko usawa wa kizingiti Cha Chini Cha mlango wake. Nilipenyeza sauti kwenye uwazi mdogo Chini ya mtango na kumuila. Kwa bahati kumbe yule dada alikuwepo Bado na tayari ameamka ila Bado naye ameshajilaza uvunguni mwa kitanda chake ...
"daadaaaa daadaaaa?...abeee! .. umesikiaaaaa? ...weye rudia ukalale Chini bitatuliyaaaaa!!!"
Niliona kumbe dada hakuwa na mpango wa kukimbia kama mimi, Sasa Niko njiapanda. Nisubiri nife bila hata kujaribu kujiokoa au nindelee na mpango wangu.
Kwa haraharaka nikaamua kufuata maelekezo ya dada yule. Nikatambaa kimyakimya mpaka uvunguni mwa kitanda changu.

Wakati huo tayari sauti za bunduki zilikua nzito zaidi kuashiria kuwa Sasa mpigajinyuko karibu. Kwa ufaham wa haraka ni kuwa mapigano yalianzia mlimani na yakawa yanakuja kijijini. Kumbuka hapo tulipolala ni atikati ya Kijiji na ndio baa ambayo waasi wanakuja kunywa hapo. Kwahiyo Kuna uwezekano mkubwa wa kuja kutake cover hapo au kuja kujificha kama wakizidiwa mapigo. Kwa fikra hizo, wazo la kutimua mbio likawa na nguvu zaidi, na Sasa nimeamua nikimbie porini angalau.
Wakati nikiwa Nawaza hivyo nilisikia sauti ya mtu Mmoja analia " Yoooooo oooo..." Kisha kuka ukimya kama dakika Tano hivi. Kukaanza kusikia vishindo vya watu wanao tembea pembeni mwa ule mgahawa tuliomo. Gafla jamaa wakaanza kufyatua risasi mfukukizo Pa pa pa pa pa..... No kama waliona adui Kwa kushtukizwa kwahiyo walikua wanampiga Kwa kubahatisha yaani walirusha risasi hovyohavyo.
Katikati ya mapigo Yao nao wakajibiwa Kwa risasi za havyo havyo, kumbuka nyumba Ile ni yambao nyepesi Cyprus. Risasi zilipiga ile nyumba. Nilisikia Vyombo kule jikomi viisambaa Kwa kupigw sisai. Kreti za bia zilisambaa Pwaaaaa. Kisha nikasikia wale jamaa kama wanakimbia huhu wakipiga risai Mojamoja. Waliendelea kuchapana kuanzia hiyo saa nane mapaka saa kumi. Kisha ukimya ukatawala sana. Niliendelea kulala palepale mpaka alfajiri.
Ilipofika saa 11, nikaanza kusikia suti za watu wakiongeankwa nje nawengine wanachekabna Stori kama kawaida.

Nikipata faraja kidogo. Lakini ukimya wa yule dada ukanipa maswali. Kumbe yeye amesinzia tu na ilipofika asubuhi tuliamka na kukutwa wale watu pale nje ni Makuli walikua wanapakia mbao ili Ile gari yetu irudi Goma.
Niliamsalimia yule dada na kusubiri kuche ili turudi sokoni.
Ilipofika mida ya saa Moja nikawa na kiu ya kujua nini kilitokea usiku na ni makundi gani Yale. Kuna Hali ya kushangaza niliona pale.Kinyume Cha Matarajio yangu ambapo nilitaka nione makundi ya watu wakipeana habari za vita ya usiku. Lakini Hali ilikua tofauti. Watu walikua na mishe zaso kama Kawa.
Hii Hali haikunipa amani, ilipofika mida ya saa tatu asubuhi, ndipo nikaanza kuzitafuta habari mwenyewe.
Nilipo uliza watu waliniambia kuwa hiyo ni kawaida na wao wamezowea kwani inatokea marakkwamara. Watu walikua wanampiga mishe zao kama Kawa.
Nizidi kumdadisi Kwa sauti ya chini ili kujua uhalisia wa hapo na nini kilitokea.
Nikaambiwa kuwa hii milima unayo Iona hapa huko juu Kuna Kambi za waasi . Kila mlima una kundi lake tofauti na hapa kijijini ndio makutanio na huja kupata mahitaji Yao hapa. Na wakati mwingine huja waasi na kuteka vijana ili waende kujiunga na jeshi lao au kuchimba Madini.
Kwahiyo lolote linaweza kutokea wakati Wotewote.

*** Safari Bado na Mzigo sijapata, lakini nimeshafika au nimekaribia kuufikia Mzigo...

*** Itandelea
 
.
Katika harakati zangu za kujikomboa na umasikini, niliamua kufanya ziara ya kusaka fursa Mpya nchini Congo. Nilikua tayari nimeshapata masimulizi mengi ya upatikanaji wa madini ya dhahabu na Rubi.
Ni mnamo mwaka Juzi mwanzoni nikiwa mji wa Uvira amabapo jilikutana najamaa Akiwa na jiwe alilo dai kuwa ni Rubi

View attachment 2497370
Baada ya mazungumzo marefu jamaa alikubali kunipa jiwe Moja ambalo alisema kuwa alishawahi kulipeleka Kigali Rwanda lakini katika vipimo ilitoa majibu yanayo Changanya. Ilisoma upande Moja ni Rubi na wakati mwingine inasoma Spinel. Sasa akanionesha ndoo imekaa mawe ya Kila namna. Kazi yangu nilitakiwa kwanza kwenda Tanzania kupima jiwe hilo ili tujue ni aina Gani ya jiwe Kisha nitafute mteja wa Uhakika ambaye tutakuwa tunampa Mzigo.
Kazi hiyo nikaichukua na kuanza safari, sikuhiyo nililala Bujumbura na keshoyake nikalala Kigoma. Asubuhi nilianza safari mpaka Arusha. Pamoja na kuzongwa na matapale na kashkash nyingi nilifanikiwa kufanya vipimo na bahati mbaya jiwe lilikua feki .
Pale Arusha nilikutana na wadau wengi sana na kupewa michongo nankutiwa moyo sana. Nilianza kuiona Dunia ya dealers. Sasa kazi ilaanza kutafuta connection ili nikasake Mzigo. Hapo ndipo safari wa Kivu kaskazini ikaanza.
Kiukweli sikuwa najua mawazo yangu ni hatari kiasi gani lakini laiti ningelijua pengine ningeanza kuungama dhambi zangu kwanza kabla ya kuanza safari katika ukanda wa damu mbichi.
Wakati ukawadia na safari ikaanza, niliambiwa nitafute biashara ya kwenda mayo ili nizugie kuingia mayo maeneo ya ndani na machimboni. Kwanza nikawaza kupeleka Nguo za kiume Jeans za masela na Viatu moka za Bakulutu na Kisha nikafikiria kupeleka Mchele. Baada tathmini jikapeleka Jeans Viatu na Samaki. Nilidhamilia kukutana na kamii ya Kila namna nanjinsia zote nilidhamilia kufa au kurudi na Mali. Militia taarifa za AWALI kujua hata mavazi ninayotakiwa kuvaa nikiwa huko. Nilihakikisha ninachukua kilataarifa Kwa uzito unao stahili.
Nilijifunza kuhisabu na kutaja pesa Kwa kifaransa, ndani ya wiki Moja nilijua kuhesabu Moja mpaka Milioni na kutaja pesa na maneno muhim ya kibiashara. Mfano Congo neno Kuuza wao linamaana ya kununua kuuu. Nipatie, kombola, mbasela na maneno mengine kama kutaja rangi na kusalimia. Bahati ni kwamba Kiswahili Cha Kivu kinafanana sana na Kiswahili Cha Tanzania Bara tofauti na hawachanganyi sana french kama wale wa Lubumbashi na Kinshasa.View attachment 2497368
Safari ilianza Kwa kupitia Burundi Kisha kuingia mji wa Uvira. Hapo nililala na kesho nikapanda Hiache kwenda Mji wa Bukavu. Nilikua na machaguo mawili aidha kupitia Barabara ya ndani ya Congo au kupitia Rusizi Kisha Rwanda na kurudi tena Congo. Barabara ya ndani ya Congo ni mbaya sana na hatari sana, wanapita watu wahalifu na wanao ogopa ukaguzi wa Rwanda na ukifika unafanyiwa sherehe yaani makorongo na magari kuanguka sio habari tena, kutekwa na kuuwawa ni kawaida kuliko kusaliklmiana. Hii inaitwa Barabara ya Ngomo(Kaburi wazi)
Changamoto ya kupitia Rwanda, ukiwa na Visa ya Dola 50 basi ukiingia Rwanda Visa ya Congo imeisha na ukitaka tena kuingia Congo Kwa kutokea Barabara mchepuko ya Rwanda basi utalazimika kulipia Visa tena, kwahiyo kupitia njia hiyo utalipa Dola 200 kwenda na kurudi. Suluhisho ni Visa ya Dolar100 ambayo unapewa miezi mitatu na unaweza kutoka Congo na kuingia kadili uwezavyo. Hilo nilisha lifuatilia mapemaa, nikawa na Visa ya Dola100 nikapita Rwanda. Kuna mengi hapa Rwanda lakini kwakua sio mada ya Leo itoshe kusema ni Dunia tofauti sana. Tuishi bongo tu, amani inatosha .
Sasa niliingia mjini Bukavu kupitia mpaka wa Rusizi. Pale Bukavu wakati nimeingia nikakuta watu wanafunga maduka na kukimbia kujificha, nilipojaribu kuuliza wakasema Kuna vita imetangazwa M23 wanaingia Leo. Hapo nilitetemeka sana, nikawaza nirudi Rwanda lakini ukaguzi na Mahojiano ya Rwanda yalinipa hofu, maana ilifika wakati nashuhswa kwenye gari nafanyiwa Mahojiano maalum . Nilishangaa Kila yulipopita nakuta askari wanajua Kuna Mtanzani Yuko kwenye gari. Nilikua nahojiwa Kwa muda mrefu mpaka abiria wanalalamika, abiria Wote walikua Wakongo na karoko mswahili Mimi, askari wa Rwanda hawamuelewi wanashangaa Mtanzani kupitia pale.
Sasa Hali Ile ilinipa hofu ya kurudi Rwanda na nikakumbuka adhima yangu Bado, safari yangu Bado na lazima nifike.
Hapo nilisajili lakini ya Simu na kuweka vocha niajiunga mitandao yote na kupata dakika 3 Kwa Buku...
Haraharaka nikapita mtu wa toroli wao wanapita shareti, nikapakia mizigo tukaelekea Bandarini. Kutoka Bukavu kwenda Guma Kuna ziwa Kivu hapo unapanda meli usiku Kucha unafika kesho Asubuhi. Lengo langu niondoka Bukavu na usiku niwe kwenye meli ili hata vita ikitokea Mimi nakua kwenye meli. Bandarini nilikuta Meli nyingi ila nikaamua kupanda "Emanele04" waniita Emauele katre, hii Bei yake Iko juu na wanapanda watu wenye uwezo na mabishoo. Lengo langu nilitaka kuanza kukutana na watu ambao wanaweza kunipa michongo ya machimbo au kupata connection za dealer wazuri. Katika safari yangu nilikua mkimya sana kwani Kila nilipo jaribu kuongea watu waligeuka kunitazama, nikagindua Kiswahili changu kinaniumbu jambo ambalo sikulitaka hasa kulingana na treatment ya Wanyarwanda. Usiku niliingia Club na kukaa Kwa muda Kisha nikarudi, mpaka wakati huo sikupata mtu wa kuanza mazungumzo naye. Tukiwa njiani upande Moja nchi kavu kulikuwa Giza huko ni Congo kisiwa kinaitwa Idjwi na upande mwingine Kuna mataa sana, huko ni Rwanda na mataa yale ni miji na vijiji.
Asubuhi tulifika Bandarini Goma. Hapo nilikuwa makini kuangalia watu wenye mizigo kama yangu hasa samaki ili nijue wanako wapeleka. Kuna dada Moja alikua na Samaki mwengi. Niliadhimia kujiweka karibu yake. Wakati anapakia kwenye gari kupeleka stoo ndipo nikasogea na kumuomba anipakilie Mzigo wangu nitachangia garama, dada yule alikubali na Alipo niuliza napeleka wapi nikamwambia Kuna mtu tutamkuta hapo mbele ndiye anajua stoo ilipo, lakini haikua kweli.. Tulienda mpaka nakoenda yeye, na tukiwa njiani nilikwambia ukweli kuwa sina stoo Bali nimekuja tujaribu biashara. Alipo niuliza Bei za Samaki Tanzania nilimdanganya nikamwambia Bei ya chini sana kiasi akawa anatamani nimpeleke huko chimbo. Leongo langu lilitimia na tulipo fika stoo kitu Cha kwanza alimueleza mume wake kuhusu Bei za Samaki Tanzania na kuanzia hapo hao wakawa weneji wangu. Kesho yake nilizunguka mjini Goma mpaka sehem inaitwa Bireree hapo ni mjini na ndipo mpakani na Gisenyi Rwanda, yaani border Ile Iko kama ilivyoisha Tunduma na Nakonde Zambia. Nyumba zimeungana za Rwanda na Congo. Soko na mishe nyingi ziko upande wa Congo . Asubuhi Wanyarwanda wanavuka kufungua biashara zao huko Goma ni jioni kurejea kwao.
View attachment 2497412
Hapo ni katikati ya mji wa Goma. Sanamu la Chukudu kama alama za vijana kuchapa kazi.
Nilitumia siku tatu nilizo Kaa hapo Goma ili kukusanya intelijensia muhim Kwa safari yangu. Nilioewa masimulizi ya vita na uharifu. Mji wa Goma mpaka Sasa uko Chini ya utawala wa Kijeshi. Pale hakuna mbunge wala mkuu wa Mkoa. Niuongizi wa Kijeshi, hii ni sababu mji wa Goma na wilaya zake ni ukanda wa Vita na machafuko Kila wakati. Pale nilishuhudia kusikia Simulizi za YouTuber wa Tanzania Denis Mpagaze zikipigwa redioni akisikuli mambo ya uzalendo Kwa Afrika. Pia Kuna redio ya watu wanajiita Kimbanguist hao wanarusha hotuba za Magufuli na kumtaja kama shujaa wa Afrika. Wakati huo Stori za Magufuli zilivutia sana na nikama ukimzungumzia vizuri tu, hapo niliwasoma mapema Wakongo nikawa namsifia Magufuli basi wakanipenda na kupata marafiki.
Nilianza kuoneshwa askari waasibwa maimai wakiwa mtaani kama raia wa kawaida tu.
Mji wa Goma umefimikwa na mawe ya Volcano na nyumba karibu zote zimejengwa Kwa mawe ya Volcano au mbao.
Nilifanya intelijensia yangu na kukamilisha Sasa safari ikawa ni kuelekea sehem inaitwa Walikale.
Mwanzo nilitaka kwenda semem inaitwa Beni au Butembo huko mnako sikia vita Kila siku lakini kilikua kumepigwa vita Kali sana na ADF wamechinja watu. Pia kilikua na taarifa za watanzania kukutwa kwenye jeshi la ADF na wakatekwa. Hii ilinipa hofu nikajua huku Watanzania hautuaminiki tena na kwakua ni ukanda wa Vita wanaweza kunikamata Kwa kushakia usalama wao tu. Pia ilitakiwa nipitie mji wa Rutchuru huko M23 waliko ondoka baada ya Kenya kupeleka majeshi. Niliambiwa tungepita Virunga na huko tunapata escort ya jeshi lakini kikinuka majeshi wanakimbia mnaachwa porini na kutekwa. Wanaume mnalazimisha kujiunga na jeshi la waasi na wanawake wanaolewa na ADF au M23. Hiyo ikatosha kiua mpango wangu. Sasa uslekeo ni Walikale na nisafari ya wiki Moja na Sio Chini ya siku Tano. Huko wakaniambia wanafanya butter trade yaani unawapa samaki. Pia masela wakipenda jeans hasa zile zenye mapichapicha basi wanakupa Madini hasa dhahabu na hapo mnakadiliaana tu.
Huko ikawa changua Bora. Kitu ambacho sikuzingatia ni usalama wa Barabara na aina ya usafiri. Mawazo yangu yalikua kwenye Madini tu. Safari ikawadia nikiwa na yule dada wa samaki mwenyeji wangu. Wakati huo Wote sikuwa nimemueleza lengo la safari yangu, yeye alikua anafurahi kuja Tanzania kuzoa samaki Kwa Bei Chee. Alinipa Kila msada ilimradi tu niwe na amani.
Siku ya safari Tulienda sehem inaitwa KwaAroxii , hapo tulikuta Maroli mengi aina ya Mercedes Benz Actros yakiwa yanapakia. Magari yalikua wazi Kwa Nyuma na hayana Bomba.
Hapo mizigo inapakiwa mapaka juuu, Kisha watu wanagombania kukaa juu ya mizigo. Nilijaribu kupya sehem nzuri lakini nilishindwa. Nilijibana Kwa mbele hapo nilikaa kwenye body huku miguu ukiwa juu ya Cabin juu ya dereva. Gari likinesa miguu inaning'inia na kutua juu ya Cabin, napo nimekalia tako Moja. Nilijibana sana nikakaa katikati. Safari ikaanza na hapo sikujua kumbe tulikua tunaingia Dunia ya wafu, huko kufa ni kawaida kuliko kuishi, Wanasema Zone rujhe yaani Red zone au Ukanda wa Damu.
Baada ya safari ya kama kilomita 50 tulikua nje ya mji wa Goma na hapo tulikuta Kuzuizi Cha jeshi. Hapo wanakagua Kila mtu kujua anakoenda na anaenda kufanya nini. Nilijaribu sana kukwepa lakini ilitoka amri ya wanaume Wote kushuka Chini.
Yule dada alinisogele na akasema ukiulizwa waambie Mimi ni mke wako tunakwenda kusalimia ukweni. Ikafika zamu yangu kupekuliwa, pesa nilikua na karobia Dola 500 nimezificha kwenye begi ambalo yukonalo yule dada.
"Peti yakawa,...... , Hapo ilimwagija lingala ya vitisho na walipooona sijibu Moja alikua pembeni alikoki silaha yake. Na kusogea pembeni, moyo ukienda mbio nikajua anataka kunifyatulia risasi. Niliamua kuongea Kiswahili Cha Tanzania pure, na hapo wakajua Mimi ni mbongo. Yule askari akamzuwia mwenzie nabkumuita. Jamaa alikua ananuka Bangi na pombe, gwanda zimechoka vibaya. Taarifa kuwa Kuna Mtanzani zikasambaa wakaanza kukusanyika. Dakika mbili mbele ikatoka amri nikaonane na Mkuu wako "Weye kuya hapa Kwa shefu" kilikua na Banda la turubai pembeni huko yupo boss wao. Nikaingia Kwa kuinama. Huko nilimkuta jamaa mstaaarabu Akiwa amezungukwa na walizi.
Pembeni kulikuwa na vijana wanne watusi na walikua wameshakiwa kuwa ni M23. Simu zao zilikiua Inapekuliwa nankukutwa picha zao wakiwa na kombati za jeshi la Rwanda. Gafla wakatolewa nje, nikiwa mle ndani nikihojiwa gafla ilisikika mlio wa risai. Yule boss aligundua hufu yangu, akaniuliza "weye mtanzania unaenda huko huyo bibi yako hayakuambia kama kule ni fasi ya mubaya?" Mikamwambia kuwa ninajua lakini titawahi kurudi haraka. Jamaa aliniomba Hela ya bia nikampa Franga 2000. Kitu inatakiwa kujua ni Askari wa Congo hawaombi Hela nyingi.
Nilipotoka nikakuta nasubiriwa Mimi peke yangu. Wale M23 sikujua nini kimewakuta zaidi ya ule mshindo wa chuma.
Safari ikaendea mpaka mji wa Masisi hapo ni kama mwisho wa kuona majumba, Sasa tunaanza milima na maporomoko ya msitumi. Huko utakuta vibanda vya Nyasi Kandi ya Barabara na askari wa Serikali wako hapo wanafanya doria. Baada ya kutembea kama kilomita 200 tulikua uwanda wa juu sana, baridi na upepo mkali. Nilianza kuona makundi makubwa ya ng'ombe wanao lindwa na walizi wa kitusi. Nilipo uliza nikaambiwa kuwa hao ni ng'ombe wa Raia Joseph Kabila. Wengine walisema ng'ombe wa Kagame. Tumesafiri zaidi ya kilomita 100 tukiwa katika ya makundi ya ng'ombe. Safari iliendelea mpaka kufika saa tatu usiku tulifika katika mji wa KITCHANGA, mji huu ambao M23 Leo wameuteka. Hao ni mji muhim sana kwani unaunganisha miji ya Goma na Bukavu Kwa upande wa magharibi na ni mji unao pitisha huduma ya chakula kwenda miji mingi sana. Mji huu ni kama roho ya maisha ya watu na uchumi.
Tulifika na kulala kwenye mgahawa wa mbao na wengine walilala nje. Hapo Kuna baridi Kali sana. Ilipofika usiku wa manane ilitoka amri ya kuzima mataa na kukaa kimya. Tulishangaa bila kujua kinachowndelea. Yule mama mmiliki wa mgahawa alijisahau kuzima taa chumbani mwake, kumbe wajuba waliona mwanga Kwa nje. Dakika chache baadae vilisikika vishindo vikumbwa sana na sauti za kiume ambazo ni kama walikua wakiimba huku wamefunga midomo. Wakiimba na kupiga vishindo Kwa pamoja na kuitikia Kwa kuunguruma. Tulipata hofu sana. Walikuja na kuzunguka Ile mgahawa wa mbao. Yule mama akatueleza kulala Chini sakafuni na tusikijitikise Kisha akajitosa yeye kuokoa maisha yetu. Wakamuamuru kuzima taa Kisha wakondoka naye kusikojulikana. Yulikaa mpaka asubuhi tukiwa na hofu sana.
Ilipofika asubuhi yule mama alikuja na kuomba tumchangie pesa ili anunue mbuzi wawili wa faini. Akatueleza kuwa wale walikua ni wazee wa Mila wanafanya tambiko la mji ule na kukutwa hajazima taa ni kosa na wangejua mule Kuna wageni basi tunguwawa. Anasema wale wajuba walikua na vichwa vya watu vimetungwa kwenye miti na kule walipo mpeleka alishuhudia wanazika mtu Akiwa hai inagwa hakumjua yule mtu. Yeye walimzuwia wakasema atakesha nao na kesho saa sita apeleke mbuzi wawili Kwa chifu wao. Tulipo muuliza akasema ni kawaida kufanya Tambiko Kila ifikapo mwisho wa mwaka. Na sikuile ilikua siku ya Tambiko.
Hapo KITCHANGA Kuna sananu la mwanamke linaabudiwa na linabadilishwa Nguo Kila mwaka.
Safari iliendelea na huko mbele kadili tulivyokua tukisogea ndivyo tulikua tunazidi kukiendea kifo. Hapo KITCHANGA ndio mwisho wa kupata internet na mpaka hapo sikuwa na mawasiliano na Ndugu zangu nilipiga simu za mwisho na kutoa malekekezo Kwa kina katika Kila jambo langu. Nilikua kama naaga au kutoa wosia wa mwisho bila ndugu zangu kujua. Nilikata tamaa ya kurudi hai, tulikua tayari katikati ya makundi zaidi ya 20 ya waasi na magenge ya watekaji. Wenyeji walionekana kuwa na hofu huku Mimi nikiwa hoitaabani. Masimulizi ya ujambazi na vita yalitawala, tulipita maeneo yenye Kila kumbukumbu ya mauaji. Jambo la kushangaza ni kuwa huko ni kama tulikua tumevuka mpaka na kuingia Rwanda, watu wanao ongea Kiswahili walizidi kupugua na wengi walibaki waliokua kwenye gari. Tulianza kupitia vijiji vya Watusi na vijiji vya wahutu Wote kutoka Rwanda. Hofu ilizidi kutanda.Tulifika sehem inaitwa Mweso, hapo ni Kambi wa wakimbizi wa Rwanda ambao wameshafanya Kijiji na Kuna Kambi ya Majeshi ya MUNOSCO na ofisi za nji nyingi zenye Operation zao Congo. Mabango ya UN,UNICEF , USaid na Japan aid na Kila shirika la kimataifa basi liko hapo. Pomoja na hivyo haizuwii kitu sababu hao Wote hawaingilii mapigano yoyote.
Tulipumzika hapo kidogo Kisha safari iliendelea.
Kabla ya kukiacha hiki Kijiji dereva alisisimama sehem watu wakashuka kuchimba dawa na Kisha wakakusanyika na kuanza kuomba Mungu. Kitendo hicho kilinipa hafu ambayo sijawahi kuipata na kwamara ya Kwanza nikatamani kurudi Nyuma , niliuliza kama naweza kupata usafiri lakini wakasema mpaka gari hilo lirudi hivyo hakuna kurudi Nyuma. Yake maombi sikutaka hata kuuliza maana waliomba Kwa Kiswahili na ni kama ilikua Sala ya toba na kukabidhi roho Kwa Muumba...
Itandelea
Duuh very Interesting
 
Back
Top Bottom