Safari yangu ya kwanza na Air Tanzania

Safari yangu ya kwanza na Air Tanzania

GwaB

JF-Expert Member
Joined
Mar 19, 2014
Posts
4,291
Reaction score
5,786
Amani iwe kwenu wadau wa JF.

Leo ndio siku niliyopanga kuanza kuiunga mkono Air Tanzania katika safari zangu zote za anga nitakazofanya katika maisha yangu yaliyobaki. Leo naelejea Geita, pamoja na kwamba naenda kwenye msiba, nimepata nafasi ya kujaribu ufanisi wa Shirika letu na kuliunga mkono na sitaki kusikia wanapata kingine zaidi ya mafanikio.

Hadi kufikia muda huu mambo yote naona yanaenda sawa, tiketi nimenunua mtandaoni na hivi ninapoandika nasubiri kupanda TC 131 na abiria wako wengi kiasi,lakini nitaangalia kama imejaa na safari yote nitaleta mrejesho.

Nina mipango zaidi ya kuruka na Air Tanzania kuelekea Entebbe, Lusaka, Moroni na Harare lakini zaidi najipanga na Guangzhou ambayo inaahirishwa labda kuningoja mimi.

Muda wa kupanda ndege umewadia.... Nitaleta mrejesho baada ya kuruka Czesc!.

1620649274126.png

 
Kwa vitu vizuri kama hivi mtu mwenye akili ndogo anasimama kumtukana jpm.

Jina jpm halisahauliki leo. Msisahau mnaishi kwenye matunda ya jpm.

No one like jpm.
Ni lini Tanzania ilikosa ndege angani?..Fastjet na Precision si walikuwa wanakimbiza fresh tu..alishofanya JPM ni kuwakimbiza fastjet na kujitengenezea monopoly mfu na hii Atcl inayoleta hasara kibao.
 
Kwa vitu vizuri kama hivi mtu mwenye akili ndogo anasimama kumtukana jpm.

Jina jpm halisahauliki leo. Msisahau mnaishi kwenye matunda ya jpm.

No one like jpm.
Tunaelekea njia ya kuruka na mambo ni bam bam! Nikiishatua Charo nitakwenda kuona kaburi la JPM. Mungu ibariki Tanzania .... Mashine inavuta Kasi na tuko angani sasa.
 
Kwaiyo kama unaenda Geita unashukia Chato au Mwanza?
 
Oohh ok vip hapo ﹰChato kunakuwa na abiria kweli?
Wapo kiasi chake. Huenda wakaongezeka,lakini kwa watu wa Magharibi kwa maana ya Biharamlo Geita Ngara Runzewe Kakonko na Kibondo ni poa sana kwani itapunguza masaa ya kusafiri kutoka 24 hadi 12 au chini yake.
 
Back
Top Bottom