Safari yangu ya utafiti Dodoma, nakukaribisha tuijue Dodoma kwa undani

Safari yangu ya utafiti Dodoma, nakukaribisha tuijue Dodoma kwa undani

Joined
Jul 4, 2025
Posts
15
Reaction score
54
Kupitia hapa nitaeleza kila kitu kuhusu Dodoma, picha linaanza kama fundi rangi nimekabidhiwa kufanya finishing jengo moja Chamwino

Aiseee msiichukulie simple Dodoma uchawi upo, ni nyumba ya brother mmoja kutoka Mbeya (Ngoja nimpe jina, naomba tumuite brother Imma)

Huyu Imma bwana kajenga bonge moja la jumba huko Chamwino ya Ikulu, akiwa katika harakati za kupaua anajitokeza mdada (Huyu tumpe jina la Mama Mussa)

Huyu Mama Mussa anakuwa akiwapikia mafundi wa Imma wakiwa kwenye harakati za kujenga na kupaua, anazoeana na Imma, mwisho wa siku akamuelezea matatizo yake, kuwa anadaiwa kodi alipopanga, anamuomba Imma amsaidie hifadhi akiwa bado anajipanga, Imma bila kujali (tumeumbwa na huruma so hata Imma ana hiyo huruma pia)

Imma akampatia Mama Mussa hifadhi, lakini toka siku Mama Mussa kaingia kwenye jengo la Imma (kumbuka Mama Mussa ameingia jengo likiwa bado halijafanywa chochote zaidi kupauliwa tu) lilikuwa halina hata madirisha

Mama Mussa alijimilikisha jengo siku hiyo hiyo, kamchezea vya kutosha Imma mpaka mda huu tunaongea Imma katumia pesa nyingi sana kwenye jengo lake na halijakamilka, kapeleka mafundi wa kila aina pale


Imma amekuwa wa kufanya marekebisho yasiyoisha kwenye nyumba yake, akitoka fundi huyu, anamleta fundi mwingine kurekebisha

Mbaya zaidi Mama Mussa katunukiwa cheo uchawini, hivyo anamiliki mpaka misukule ya wengine kwenye jengo la Imma

Ngoja tufupishe story nisiwachoshe, nilipelekwa kufanya marekebisho ya skiming kuna ukuta ulikuwa una mawimbi, baada ya kufika site kama fundi nikakagua jengo nikaona mapungufu mengi sana

Kazi ya jengo la Imma kuanzia kujenga boma imekosewa sana kazi ni chafu, mpaka naanzakuifanya kazi Mama Mussa ni kama alikuwa ananiandaa kisaikolojia, maana alikiwa haishi kunielezea changamoyo za Imma na idadi ya mafundi waliopita kwenye jengo hilo

Na mimi nikamhakikishia Mama Mussa kuwa basi asihofu kwa kuwa mimi ni bonge moja la fundi matatizo ya Imma yangeishia pale


Ajabu nlivyoanza kuifanya kazi ilee kadri siku zilivyokuwa zinaenda ari ikawa inapungua najisikia kuchoka bila sababu, ikabidi nirudi maabara kucheki ni nini changamoto, majibu yakatoka yakijieleza kuwa tatizo ni Mama Mussa

Mama Mussa ametia kigingi kwa Imma asikamilishe jengo, kamfanya Imma awe ni mtu wa kurekebisha miaka yote na huenda mpaka kifo kitamkuta bila jengo lake kukamilika na hii inaweza kumfanya Mama Mussa kuwa mmiliki wa kudumu wa jengo lile

Mafundi wakifika pale wanapoteza dira fundi anafanya makosa na hayaoni kwa mda huo, na bahati mbaya wanafanywa kuwa ni watu wa kupuuzia mambo, lengo ni lile lile Imma asihamie uungwana wake wa kumpa hifadhi bure Mama Mussa umegeika mkuki unaommaliza taratibu Imma

Kwa leo wacha tuishie hapa lkn naahidi kukuelezea kila kitu nilichokiona Dodoma hasa hasa fursa za kuichumu, nimeamua kuanza na hili la ushirikiana ili ukija ujue utaanzia wapi kwa imani yako
 
Wagogo noma ni wavivu wana penda kula bila kufanya kazi ,
 
katik makosa ni kumpa mtu ntumba bujamaliza akae eti akuangalizie.
nachoshauri. dodoma wenye vinyumba miin waingie joint venture wapige gorofa sio kuacha vinyumba kama vile mjin kati.na lami ziwekwe maeneo yote na pavement kama Burkina faso wana project yao faso mebo hiv sisi wa kushindwa na Burkina faso kweli ambao miaka miwil.mitat ugaid unawssumbua ila angalia faso mebo wanaweka pavement kila kichochoro cha ouagadugu kupunguza vumbi. dodoma nayo tukajifunze Burkina faso
 
Uchawi ni science ya Asili ambayo haina faida yoyote .
Zamani hata ukiwa mnene ukafa ghafla watu wars conclude umelogwa umechezewa

Ila siku ukifa hivyo vipimo hospitalini vitabainisha ulikuwa na pressure au heart attack
Si uchawi=ujinga

Mjinga hata chemical changes yenye kubadili rangi ataona NI uchawi
 
Zamani hata ukiwa mnene ukafa ghafla watu wars conclude umelogwa umechezewa

Ila siku ukifa hivyo vipimo hospitalini vitabainisha ulikuwa na pressure au heart attack
Si uchawi=ujinga

Mjinga hata chemical changes yenye kubadili rangi ataona NI uchawi
Uchawi
Kukaa mazingira machafu
Kelele
Kuwa mzinzi
Kuwa mlevi
Kuwa mwizi


Yote hayo ni matatizo ya akili yanachagizwa na ujinga
 
Back
Top Bottom