kifupi kirefu
JF-Expert Member
- Oct 29, 2018
- 539
- 3,507
Katibu mkuu wa CCM pamoja na Mwenezi ni baadhi ya viongozi wa juu wa CCM ambao tuseme tu ukweli walipaswa kuwa viongozi wa Jimbo au Wilaya lakini siyo viongozi wa Kitaifa. Tukumbuke Mwenyekiti naye hana ushawishi kwenye jamii so viongozi wote wa juu ni vigumu kufanya siasa za majukwaani kwa sababu wanakosa ushawishi.
Ukiona chama kikuu kina safu ya aina hii tambua kimefilisika, hakuna mapambano ya hoja ndani yao na hakuna njia unaweza wategemea wakakuvusha. Hi nadhani ndiyo sababu iliyovifanya vyombo vya dola kuingia mtaani kupambana na Chadema baada ya kuona chama Tawala kimekosea kwenye safu ya uongozi.
Kufikia 2025 wasipobadilisha Hawa viongozi tusitegemee kufanyika kwa uchagizi labda turudi kwenye uchaguzi kama alivyofanya JPM last time. Ila Hawa watu ukiwaambia wakakitangaze chama sidhani Kama wataambulia kitu. Ni viongozi wamekaa katika Hali yakuelekezwa chakufanya na siyo kupanga chakufanya. Ni viongozi ambao Wapo hapo walipo kwa kubebwa Kama ilivyokuwa kwa Polepole na Bashiru kwamba walichukuliwa na mwenyekiti wakawekwa hapo juu bila hata wao kujua.
Kwa safu na nguvu waliyonayo Chadema ambayo wanaharakati wote na wasomi wanasimama nao sikutegemea kuona viongozi wakuu wa CCM kupooza kiasi hiki. Sikutegemea kuona wakilala nakuamka na press za ajabu ajabu ambazo hata hazikai kwenye front page za magazeti, sikutegemea tuwe na viongozi wanaosikiliza Polisi wanachosema na wao waje kukazia, nilitegemea wawe bold kutekeleza majukumu yao na wawe n nguvu inayoonekana. Hata mzee Mkama alikua na afadhali kuliko chongolo.