Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Said Issa Mohammed, aliyefukuzwa uanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa madai ya kukiuka katiba, kanuni na miongozo ya chama, amesema uamuzi huo ni kinyume na katiba ya chama hicho.
Hatua ya kumfukuza ilipitishwa na Kamati Tendaji ya Kanda ya Pemba baada ya kuhusishwa na kufungua kesi dhidi ya bodi ya wadhamini na Katibu Mkuu wa CHADEMA, shauri ambalo baadaye lilitupiliwa mbali na Mahakama Kuu kutokana na kasoro zilizobainika.
Soma: Said Issa Mohamed aliyeishtaki CHADEMA atimuliwa rasmi Uanachama kwenye chama hicho
"Kwa sababu katiba ya chama inaeleza utaratibu mzima wa namna ya wanachama kuvuliwa uanachama, ikiwemo haki ya kuitwa kwenye kikao halali ambacho tuhuma zitasomwa na inatakiwa tuhuma hizo ziandikwe ili ajipange kuzijibu, na kikao hicho kitampa fursa ya kujieleza na kujitetea juu ya tuhuma ambazo zimetuhumiwa kwake. Na pale kitakapokuwa chama kimeona kinadhibitisha juu ya tuhuma hiyo, basi chama kinaendelea na mchakato mwingine ukiwemo wa kumtaka mtuhumiwa ama aombe radhi au kutoa maamuzi mengine ya kumfukuza chama. Taratibu hizi zote hazikuchukuliwa."
Via: Azam TV