PostGE2025 Said Issa: Uamuzi wa kunifukuza CHADEMA siyo halali

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Said Issa Mohammed, aliyefukuzwa uanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa madai ya kukiuka katiba, kanuni na miongozo ya chama, amesema uamuzi huo ni kinyume na katiba ya chama hicho.

Hatua ya kumfukuza ilipitishwa na Kamati Tendaji ya Kanda ya Pemba baada ya kuhusishwa na kufungua kesi dhidi ya bodi ya wadhamini na Katibu Mkuu wa CHADEMA, shauri ambalo baadaye lilitupiliwa mbali na Mahakama Kuu kutokana na kasoro zilizobainika.

Soma: Said Issa Mohamed aliyeishtaki CHADEMA atimuliwa rasmi Uanachama kwenye chama hicho

"Kwa sababu katiba ya chama inaeleza utaratibu mzima wa namna ya wanachama kuvuliwa uanachama, ikiwemo haki ya kuitwa kwenye kikao halali ambacho tuhuma zitasomwa na inatakiwa tuhuma hizo ziandikwe ili ajipange kuzijibu, na kikao hicho kitampa fursa ya kujieleza na kujitetea juu ya tuhuma ambazo zimetuhumiwa kwake. Na pale kitakapokuwa chama kimeona kinadhibitisha juu ya tuhuma hiyo, basi chama kinaendelea na mchakato mwingine ukiwemo wa kumtaka mtuhumiwa ama aombe radhi au kutoa maamuzi mengine ya kumfukuza chama. Taratibu hizi zote hazikuchukuliwa."

Via: Azam TV
Ila Mbowe naye kwa kuzoa zoa sasa hii takataka aliiokotea wapi?
 
Mkuu hata wewe unashangilia hili unahisi Maalimu yuko sahihi?
tukiacha uchama kabisa
kafutwa uanachama isivyo sahihi gentleman,

in fact,
natamani utaratibu ufuatwe kwa mujibu wa Katiba ya chadema na itapendeza zaidi, otherwise tutashuhudia vichekesho zaidi kwa jambo hili dooogo tu, la mtu moja dhidi ya chama kizima 🐒
 
nimeandika hapa mkuu nenda kaangalie
 
Wakina Halima mpaka sasa ni wanachama wa Chadema kwa sababu Chadema haikufuata utaratibu katika kuwanyang'anya uanachama.

Na je Katiba ya Chadema inakataza mwanachama wake kukishtaki chama chake?

Amandla...
 
nimeandika hapa mkuu nenda kaangalie
nimeipenda hiyo,
but ukweli unabaki palepale kwamba kwenye suala la kuwasimamisha au kuwafuta uanachama wanachama wake,

chadema imekua ikikurupuka na kurudia kufanya makosa yaleyale waliyoyafanya wakati wa kumfukuza zito kabwe na wenzake, lakini pia hata ilipojaribu kuwafukuza uanachama wabunge wake wa viti maalumu.

Na katika kumfuta huyu muungwana, dosari na makosa ya utaratibu ya ufukuzaji yamerudiwa villevile, ni bahati tu muungwana sio mbunge na hana cheo chenye maslahi mapana ndani ya chadema.

In short,
atawasimbua mno chadema mahakamani, just kuwasumbua tu coz wamezoea usumbufu wa kujitakia wenyewe 🐒
 
Said Issa Mohammed, aliyefukuzwa uanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa madai ya kukiuka katiba, kanuni na miongozo ya chama, amesema uamuzi huo ni kinyume na katiba ya chama hicho.

Hatua ya kumfukuza ilipitishwa na Kamati Tendaji ya Kanda ya Pemba baada ya kuhusishwa na kufungua kesi dhidi ya bodi ya wadhamini na Katibu Mkuu wa CHADEMA, shauri ambalo baadaye lilitupiliwa mbali na Mahakama Kuu kutokana na kasoro zilizobainika.

Soma: Said Issa Mohamed aliyeishtaki CHADEMA atimuliwa rasmi Uanachama kwenye chama hicho

"Kwa sababu katiba ya chama inaeleza utaratibu mzima wa namna ya wanachama kuvuliwa uanachama, ikiwemo haki ya kuitwa kwenye kikao halali ambacho tuhuma zitasomwa na inatakiwa tuhuma hizo ziandikwe ili ajipange kuzijibu, na kikao hicho kitampa fursa ya kujieleza na kujitetea juu ya tuhuma ambazo zimetuhumiwa kwake. Na pale kitakapokuwa chama kimeona kinadhibitisha juu ya tuhuma hiyo, basi chama kinaendelea na mchakato mwingine ukiwemo wa kumtaka mtuhumiwa ama aombe radhi au kutoa maamuzi mengine ya kumfukuza chama. Taratibu hizi zote hazikuchukuliwa."

Via: Azam TV
hili jamaa lofa nini
kwa ni lazima awe
mwanachadema
si ajiunge hata udp
 
nimeipenda hiyo,
but ukweli unabaki palepale kwamba kwenye suala la kuwasimamisha au kuwafuta uanachama wanachama wake,

chadema imekua ikikurupuka na kurudia kufanya makosa yaleyale waliyoyafanya wakati wa kumfukuza zito kabwe na wenzake, lakini pia hata ilipojaribu kuwafukuza uanachama wabunge wake wa viti maalumu.

Na katika kumfuta huyu muungwana, dosari na makosa ya utaratibu ya ufukuzaji yamerudiwa villevile, ni bahati tu muungwana sio mbunge na hana cheo chenye maslahi mapana ndani ya chadema.

In short,
atawasimbua mno chadema mahakamani, just kuwasumbua tu coz wamezoea usumbufu wa kujitakia wenyewe 🐒
zitto alikuwa anajua sheria sana na katiba na ndo maana alivoona amefukuzwa hakutaka kuanza kubishana kama huyu jamaa anachotaka nakuhakikishia kuwa atashindwa maana katiba inaruhusu kufukuzwa bila natural justuces kwa baadhi ya makosa wanatakiwa wao wabadilishe katiba yao kwanza
 
Okay let's wait and see,

but mule mule chadema kuna wangwana wanamsaidia kwa kiasi kikubwa sana huyo jamaa kuiangaisha chadema,

but pia,
kuna watu pale chadema taifa, wanawachochea na kuwashauri viongozi wa kitaifa wafanye makosa ili hatimae waonekane wabaya kwa wanachama, na kisha wao watumie fursa hiyo kujitwalia nafasi za kitaifa.🐒
 
100% nakubaliana na wewe ila alichokuja kushangaa wamemgeuka wale wa pemba ambao walimwambia kuwa watakuwa na yeye sasa sijui tayari wamepokea mgao hahahaha

maana nakumbuka mwanzoni alisema uongozi wote wa Zanzibar uko na yeye kwenye hilo swala nashangaa wamemtoa chambo maybe wameona hana tena thamani kwenye game yao..

si unafahamu mchezo wa Chess angalia matumizi ya Knight na Pawn..
knight huwa inaanza ikwa na nguvu sana ila baadae nguvu yake inapotea
ila pawn anaanza akiwa dhaifu ila baadae anaweza akawa na nguvu saaana

so huenda kuna mwingine anaandaliwa na amekwisha iva kufanya maangamizi
 
Akate rufaa... Kikubwa ni kwamba hatakiwi.. Kifo ni kifo tu.. Ufe kwa risasi, panga, au Malaria.. Ukifa umekufa... Hautakiwi hata ukitaka kuchagua style ya kutokukutaka.
 
CHADEMA wamechelewa sana kufanya haya maamuzi alitakiwa kufukuzwa kipindi alipofungua ile kesi
 
Wakina Halima mpaka sasa ni wanachama wa Chadema kwa sababu Chadema haikufuata utaratibu katika kuwanyang'anya uanachama.

Na je Katiba ya Chadema inakataza mwanachama wake kukishtaki chama chake?

Amandla...
Hoja hiyo ya mwisho ni kweli, ukishitaki Chadema Mahakamani uanachama wako umekwisha

Halima alifukuzwa na ndio maana ameomba upya uanachama kwenye Tawi

Kuhusu Ile kesi ya covid 19 ilikuwa Mpango wa Serikali tu, Matiko ni mwanachama wa ccm tangu 2022 lakini bungeni aliitwa mbunge wa viti Maalum Chadema hadi 2025 bunge lilipovunjwa
 
Kifungu gani kinasema hivyo.

Mahakama iliwaambia mfuate utaratibu ili kufukuzwa kwake kukamilike lakini hamkufanya hivyo. Kisheria alikuwa na bado ni mwanachama.

Ulikuwa kweli mpango wa CCM lakini CDM walichangia kuuwezesha kufanikiwa.

Sio Matiko peke yake. Nadhani hata Slaa aliwahi kusema kuwa kwa vile hakurudisha kadi ya CCM alikuwa mwanachama wake hata alipokuwa KM wa CDM.

Kuna mbunge mwingine alitangaza kujitoa CDM na kujiunga CCM lakini Ndugai akamwambia ataendelea kuwa mbunge wa Chadema mpaka kipindi chake kitakapoisha.

Yote haya ndio yananifanya nishangae mnarudia kosa lile lile. Hapo si kumpa upenyo wa kufungua kesi dhidi ya CDM ya udhalilishaji na kutotendewa haki? Na si anaweza kuomba zuio tena wakati kesi mpya inaendelea?

Huyu jamaa hana cheo chochote CDM, mngempotezea na kumtenga mpaka mwenyewe aamue kujitoa.

Kuhusu mipango ya Ndugai na Yule Mbunge na hata covid 19 ulikuwa uvunjifu wa katiba wa bunge, unajua ila unataka kunipotezea muda, uwe na siku njema
 
Back
Top Bottom