Mchambuzi wa siasa na mwanasiasa mkongwe Saidi Miraj amesema kuwa Bunge la Tanzania linapoteza maana yake halisi iwapo halina mijadala yenye upinzani wa kweli na mawazo mbadala yanayowakilisha matakwa ya wananchi.
Akizungumza katika mahojiano maalum na Jambo TV, Miraj amesema kuwa mijadala ya moto bungeni si dalili ya mgawanyiko, bali ni kiashirio cha ustawi wa demokrasia ya kweli.
Ameeleza kuwa katika mabunge yenye demokrasia imara duniani, wakati mwingine hata wabunge wa chama tawala husema wazi wanapopinga maamuzi ya viongozi wao ikiwa yanaenda kinyume na maslahi ya wananchi
Miraj amesisitiza kuwa kuheshimu mawazo mbadala na kuruhusu hoja zenye mitazamo tofauti ni msingi wa Bunge imara na lenye kuwakilisha wananchi ipasavyo, akiongeza kuwa umoja wa kitaifa haujengwi kwa kuficha tofauti za mawazo, bali kwa kuzisikiliza na kuzifanyia kazi kwa hoja