Said Salim Bakhresa akamata nafasi ya 30 katika orodha ya watu matajiri 40 barani Afrika – Forbes

Said Salim Bakhresa akamata nafasi ya 30 katika orodha ya watu matajiri 40 barani Afrika – Forbes

Utamuonea bure!Umeambiwa anaviwanda hadi nje ya nchi lakini collectively ndiyo anahela ndefu!Kwahiyo usikariri kuwa mapato yake yote yanatokea tanzania maana unawezakukuta kwa investment zake za bongo peke yake wapo wanaomburuza so siajabu kutokuwepo ktk orodha ya walipa kodi bora 20 hapa nchini.

Au kama una-data za kuthibitisha madai yako basi tuwekee jamvini na sisi tujionee.

Nijuavyo ana viwanda Tanzania, Zambia, Rwanda na Uganda, Sina uhakika kati ya Msumbiji kuina mojawapo ana viwanda huko pia. sasa mnaweza kuangalia kwa mtawanyiko huu kodi inakuwaje.. Ingawa uwekezaji mkubwa upo Tanzania.
 
Tajiri namba moja Bongo, namba 2 EA halafu bado anauza ice-ream kwenye vituo vya daladala na chapati za 500/= kama wajasiliamali wadogo wanawake!!
alafu kwenye walipa kodi 10 boran wa TRA hayumo, ndipo ujue sasa nani ni nani bongo!!

Huyu yuko kwenye ten ya walipa kodi?
hapana!!!
huko wapo wauza sigara, bia nk
 
HONGERA SANA, NI MFANO Mzuri sana wa kijasriamali kwa Watanzania
 
Huyu bwana amejitahidi sana tumpe pongezi,tuache majungu.:becky::becky:
 
Hongera sana SSB...hilo la ajira ndio muhimu zaidi kwa jamii yetu!
 
Watakuwa wanamuonea Mengi, nasikia ana pesa kama njugu. Tajiri wa Kaskazini.
 
Aliwahi kuichangia CUF kipindi fulani, mkono wa chuma wa CCM
ukateketeza baadhi ya bidhaa zake.............
Mkuu,nakumbuka wanaume walivyomshughulikia kwa kuteketeza ngano yake tani nyingi;kama mfano kwa wengine wasiige mfano wake;lakini Mzee Sabodo,amevunja mwiko huo leo,pamoja na majasiri wachache!
 
Kuna wafanyakazi wake kuna wakati wakikuwa wanalalamika hawajaajiriwa tangu waanze kazi pale kwake ni muda mrefu wako pale kama vibarua,sijui hilo limekaaje,kidini na kiutaratibu hapa duniani kwenye mapato,nahisi kama alikuwa anawanyima haki zao na pia serikali ilikuwa inanyimwa haki zake!
 
Hongera sana. Sasa jitahidi juisi utengeneze kwa matunda ya hapahapa na chapati kwa ngano ya hapahapa. Itafaidi wakulima na kuongeza ajira.
 
na pia anashika nafasi ya 30 kati ya matajiri 40 wa AFRICA kwa mujibu wa jalida la FORBES linaloelezeaga utajiri wa watu duniani...
 
HONGERA SANA, NI MFANO Mzuri sana wa kijasriamali kwa Watanzania
unaweza ukawa uko sahihi, swali: Je, analipa kodi sahihi?
maana kama kweli yeye ni milionea wa bongo tuone na kodi yake basi vinginevyo naye ni mwizi kama wengine tu!!!! kumbuka simuonei wivu
 
Yaani jamaa ana $520 mil. hapa bongo hiii imeniuma kweli -hivi wakina Kimuga,Lyimo,Masanja,Mapunda,Nnko,Nyange hivi mpo wapi mbona uchuuzaji mmeanza zamani-mikakati yoote mara MKUKUTA na ile nyingine MKURABITA imefanya nini-haya jamani ngoja nikae kimya na wivu wangu!

Ni utajiri unaoletwa na majini, hali akazifurahia pesa zake. Masharti kibao
 
Yaani jamaa ana $520 mil. hapa bongo hiii imeniuma kweli -hivi wakina Kimuga,Lyimo,Masanja,Mapunda,Nnko,Nyange hivi mpo wapi mbona uchuuzaji mmeanza zamani-mikakati yoote mara MKUKUTA na ile nyingine MKURABITA imefanya nini-haya jamani ngoja nikae kimya na wivu wangu!
je na wa kwanza ni nani EA?anamiliki kiasi gani?ningefurahi pia kuwajua wa 3,4,5.
 
Kuna wafanyakazi wake kuna wakati wakikuwa wanalalamika hawajaajiriwa tangu waanze kazi pale kwake ni muda mrefu wako pale kama vibarua,sijui hilo limekaaje,kidini na kiutaratibu hapa duniani kwenye mapato,nahisi kama alikuwa anawanyima haki zao na pia serikali ilikuwa inanyimwa haki zake!

mkuu kwenye capitalism ili uwe tajiri lazima uwanyonye wafanyakaz wako ili ujilimbikizie zaidi,hakuna tajiri ambaye awanyony wafanyakaz wake,ukiwanyonya ndio unajilimbikizia zaidi na awawez chomoka sababu ya ukosefu wa ajira uliopo duniani
 
Nakumbuka Former president Benjamin William Mkapa aliwahi sema kwamba Waislam ndio wanaongoza kwa utajiri nchini Tanzania na ndio wenye number kubwa ya wafanyabiashara.
Katika nchi ya mfumo-kristu, Muislaam anaongoza kwa utajiri!
 
Back
Top Bottom