Saida Karoli apigiwa simu ya kutishiwa maisha

Saida Karoli apigiwa simu ya kutishiwa maisha

Kwa ninavyozijuwa FITNA za walioandaa Tour yake hii ni KICK.Na wameahirisha kwa kuwa wanasubiri muda muafaka wa yeye kuzifanya Hizo Show
Mfano;
1.Wanasubiri Tarehe za mwisho wa mwezi.
2.Msimu wa Mavuno
3. Wameahirisha ili waunganishe na lile tamasha lao walilodai siku likifanyika Dar liwe Public Holiday.waweze kuua ndege wawili kwa jiwe moja.
 
Wamemuambia ukitaka kurudi kwenye peak, tengeneza kiki...jifanye wanataka kukuua

Sasa mtu amuue Saida Kalori ili apate nini? Sasahv ana umaarufu upi mpaka watu wamuue?

Uongo mtupu [emoji23] [emoji23] [emoji23] !!!
 
Bongo fleva ushirikina upo tena kwa sana tu.....we umeona wapi mtu anayejitambua na kupiga mzuri hawiki ila mbabaishaji ndiyo anayewika?
 
Mkuu alitaja na hizo show zake alipanga afanye lini na wapi?

Maana hawa wasanii wa siku hizi wamekuja janja janja sana
 
Halafu mnataka Africa iendelee; Haiwezi kuendelea kwa huu upumbafu wa kurudishana nyuma kimaendeleo... Ukisha muuwa whats next???


Yaaani kuna matumbo ya wamama wengine yalibeba viumbe vya ajabu sana.....


Poleni sana wanawake wote duniani....
😀 mbavu zangu hatari saana
 
Kuna watoto wengi sana humu JF kumbe ,kama si watoto basi wengi wamakulia mjini na hawajaona matukio kama haya. Saida anasema hapo kuna kaka yake alitishiwa hivyohivyo na baada ya siku tatu alichinjwa, nadhani naye angekuwa msanii mngesema ni kiki. Unashangaa saida kutishiwa kifo eti kwa lipi, mbona watu wanauwawa kila kukicha pasipo sababu kabisa, kila siku tunasikia mara mtoto kauwawa kwa kula mboga, watu wameuwawa kwa kulipiza kisasa, na wanaokufa kwa kufanyiwa uchawi ndiyo usiseme hasa wanapotaka kunyanyuka, wanaopotea kabisa wamejaa halafu mtu na akili zake anasema anatafuta kiki. Tuwe tunajipa muda kusikiliza kwa akili pia siyo masikio halafu haraka haraka tunajibu. Hamjifunzi kwa Roma , watu walimkebehi humu sana lakini leo hao hao wanaamini kweli jamaa alitekwa na kuumizwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
huyo anayemtishia na yeye ni mwehu...kwa huo wimbo mmoja ambao unapigwa clouds tu!!!

labda kama kuna lingine....lakini kwenye mziki hajarudi chochote!!
Kasha kula hela ya watu analeta longo longo la kujidai katishwa..
 
Back
Top Bottom