Saido Ntibanzokiza vs Benard Morisson, Manara alikuwa sahihi. Yanga tuna shida

Saido Ntibanzokiza vs Benard Morisson, Manara alikuwa sahihi. Yanga tuna shida

mdukuzi

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2014
Posts
20,925
Reaction score
51,688
Saidoo aliachwa na Yanga kwa mazingira sawa na yale aliyoachwa Morrison Simba.

Ila Saido anaonekana kuwa tegemeo kwa club yake tofauti na Morisson.

Ilikuwaje Morrison kupewa tena mkataba wakati mambo yake yanajulikana maana sisi ndio tuliomleta mjini.

Au ndio ule usemi wa Haji Manara kuwa Jangwani wenye akili wawili tu
 
Ukweli usemwe, Ntibanzokiza aache uchoyo na ubinafsi, kuna mabao anatukosesha wakati kama angetoa pasi inakuwa kambaa, ila yeye analazimisha afunge yeye anaishia kupokonywa na kuharibu movement.

Na ulengaji wake wa bao awee anatazama na angle sio kupiga tyuuh,

Mie ananikera kwa kweli. Khaaa
 
Mwacheni bwana kila mmchezaji ana faida yake kwa kipindi fulani
 
Mie ananiboa mnoo, mabao mengi anatukosesha sana huyu, ajue kuwa anaipambania team sio kujipambania yeye.

Km fame atapata tyuuh muda ukifika. Lol
Hilo swala linarekebishika tu kikubwa kipaji kipo
 
Umelinganisha katika nyanja ipi? Kinidhamu au kiuwezo uwanjani? Kama kinidhamu upo sahihi ila kama kiuwezo basi haupo sahihi. Morrison ni mchezaji anayefosi kukupa matokeu kwa namna yeyote ile.
Aaah we jamaa kumbe upo?

Aisee jana sijakusoma kabisa baada ya mechi na staki kujua sababu
 
Saidoo aliachwa na Yanga kwa mazingira sawa na yale aliyoachwa Morrison Simba.

Ila Saido anaonekana kuwa tegemeo kwa club yake tofauti na Morisson.
Ilikuwaje Morrison kupewa tena mkataba wakati mambo yake yanajulikana maana sisi ndio tuliomleta mjini.

Au ndio ule usemi wa Haji Manara kuwa Jangwani wenye akili wawili tu
Rage atakumbukwa daima. Yanga walishasema kuwa Saidoo ni mchezaji mzuri sana ila hawawezi ku-meet demands zake. Pia jamaa ana 'makuu'. Kukaa nae ni sawa na kutembea na nyoka mfukoni.

Wanamfaham vzr Morrison. Matatizo yake ni yake mwenyewe. Wengine wana sumu hadi kwa wachezaji wengine.

Anafananishwa na Zito Kabwe alivyokuwa CHADEMA. Pamoja na kuwa mwanasiasa mzuri sana na mwenye akili nyingi, walimkataa
 
Saidoo aliachwa na Yanga kwa mazingira sawa na yale aliyoachwa Morrison Simba.

Ila Saido anaonekana kuwa tegemeo kwa club yake tofauti na Morisson...
Kwani kuna kilichopungua kwa kutokuwepo saido? Timu aishindi? Au mnatafuta kichaka baada ya kushiba makande? Nani kawaambia yanga inatetereka ata asipokuwepo mchezaji mmoja?

Nani kakwambia yanga ina mchezaji muhimu? Mchezaji muhimu ndani ya yanga ni Timu nzima na sio mtu mmoja, ayo mambo ya kumtegemea mchezaji mmoja yako makolo uko acha wenge wewe
 
Back
Top Bottom