Yanga imekuwa katika wakati mgumu baada ya mtu asiyejulikana Hans Pope kumuweka kwenye mikono salama striker wa Yanga Saido.
Katika hali ya kushtua Saido amefuta picha zote akiwa na jezi za Yanga katika kurasa zake za Insta
Kama Simba wanataka kumsajili Ntibazonkiza wamepotea sana.
Kiwango chake hakimfikii mchezaji yoyote wa simba wanaocheza eneo lake, Saido hawezi kumuweka bench hata Miraji Athman Sheva hawezi kumweka benchi hata Cyprin Kipenye au Abdullazack Mohamed.
Kama anasajiliwa kuibomoa Yanga hata penyewe ni matumizi mabaya ya pesa kwani Saido ni injury prone na hana future kwenye kikosi cha Yanga.
Simba hatuna mapungufu eneo la attacking midfield tuna kila aina ya wachezaji wanaotupa dimension tofauti uwanjani.
Simba tunapaswa kujiandaa na kuzeeka kwa Wawa na Nyoni pendekezo langu nafasi ya Wawa.
1. Captain Solomon Banga wa Cotton Sports
2. Adrian Chama wa ZESCO United.
3. Timothy Awany sasa hivi yuko Uturuki alikuwa anacheza KCCA ya Uganda.
4. Mohamed Quattara wa Al Hilal ya Sudan.
Mabeki wote hao wanauzoefu mkubwa na ukiondoa Timothy Awany wengine wote ni good ballers hasa Adrian Chama
Captain Solomon Banga ana speed, mrefu kuliko Wawa na anafunga sana kwenye CHAN alifunga goli tatu na zote kwa set pieces