Sakata la Bandari: Je, ni serikali ilimtafuta mwekezaji au mwekezaji aliitafuta serikali ya Tanzania?

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
Habari,

Waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano ameonekana akiongea bungeni na kumbi zingine nje ya Bunge akiwataka Watanzania wafungue moyo kupokea neema kutoka kwa Mwekezaji sijui anaitwa D World.

Swali la wananchi kwa serikali liko hivi:

Je, ni serikali ilimtafuta Mwekezaji au mwekezaji aliitafuta serikali ya Tanzania?

Tukijibiwa hili swali ndipo tutapata mpenyo wa kuuliza maswali mengine au tutaanza kufurahia hizo neema.
 
Hawa CCM hadi wanaondoka madarakani watauza kilakitu cha nchii, pamoja bandari zetu kutoa huduma kwa bei gharama kubwa charges nyingi ukilinganisha na bandari nyingine Duniani bado tunaambia zimeishindwa kujiendesha wale wanaiba ndio hawa wauzaji Kisha wanatuambia tumeshindwa kuziendasha na mimi wananiweka kwenye mamuzi yao.
 
Who bewitched this country?
 
Mwacheni Mama afurahie maisha na Wajomba zake!
 
Za chini ya kapeti zinasema walioleta hii kampuni ni Mtoto wa Mama Samia,Mkwe wa Kikwete na Mr Patel.Huyu Patel ndiye yule anayejenga Hotel kule mbugani Serengeti kwenye mazalia ya Wanyama.
 
Wee vipi! Mbona tumelimaliza tayari na wabunge wenu mliowachagua wameridhia.
 
Kwenye ule mkataba wameeleza kua mkulu alipoenda kuwatembelea wajomba zake ndio kwenye mazungumzo yao swala la Bandari likaibuka.
 
Ni kwamba huko uarabuni kulikuwa na mnada au tuite maonesho badala ya gulio, hapo katika pitapita tukagongana mabega ukawa mwanzo wa kujuana na kuelezeana kilichotupeleka gulioni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…