Sakata la Bandari: Spika Tulia atoa ufafanuzi

Spika anasema wacheni kupotosha:

--
Spika wa Bunge, Dr Tulia Ackson ametoa ufafanuzi kuhusu taarifa zilizosambaa zikidai kuwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tayari limesharidhia Azimio la Bunge kuhusu pendekezo la mkataba wa bandari kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Dubai ambapo amesema Bunge bado halijaridhia.

Spika Dr. Tulia amesema taarifa zilizotolewa na vyombo vya habari na mitandao kuwa azimio hilo limesharidhiwa na Bunhe si za kweli kwani azimio husika kwa sasa bado lipo katika ngazi ya kamati ya pamoja kwa mujibu wa kanuni na mara baada ya kamati kumaliza kazi yake azimio hilo limepangwa kuingia Bungeni tarehe 10 June 2023 kwa ajili ya mjadala.
I think it s another Richmond,

Kama si plan ya sababisha tatizo solve tatizo basi its total another Richmond, na ule msemo wa yuleee jamaa unatimia, japo sikutarajia iwe mapema hivi..

Kama kwa miaka 2 pesa zote za kigeni hatuna its means our leaders wana mesup nyingi za wazi, na sasa tu overcome hilo bonde wanakuja na second Richmond....

B
 
Kupotosha kupi wakati Mkataba Kati ya Serikali ya Tanzania na kampuni ya DPW ya Emirates Dubai unaacha maswali mengi.

Ni mkataba ambao ulisainiwa kwa mwendokasi bila kuchukua tahadhari juu ya madhara yake yaliyo dhahiri. Mkataba huu haukubaliki kwa sababu nyingi Sana.

1. Mkataba ni wa milele kwa sababu hauna ukomo. Najua wapo waliosema ni wa miaka 100 na wapo waliosema ni wa miezi 12.

Hawa wote sijui wametoa wapi huo muda wa mkataba. Ibara ya 23 ya mkataba na randama zake (appendixes) hakuna popote zinaonyesha mkataba huu ni wa muda gani. Hii inaweza kutafsiriwa kuwa ni mkataba wa kudumu.

Ni kweli unaweza kuwa miaka mia lakini pia hakuna Cha kuzuia uwe wa miaka 1000.

2. mkataba huu una nguvu kuliko Sheria za Tanzania pamoja na Sheria za kimataifa (Takes precedent over national and international law)

Mathalani Ibara 23(4) hairuhusu kuvunja mkataba huu hata pakiwa na ukiukwaji mkubwa (material breach) au kukitokea hali inayopelekea mkataba usitekelezeke (fundamental change of circumstances) ambalo ni Takwa la mkataba wa kimataifa uitwao Vienna Convention on the Law of Treaties,1969 ambao Tanzania imejifunga nao.

Sasa hii tafsiri yake ni kwamba baada ya kusaini mkataba huu hata Dubai wakikiuka kabisa hatuwezi kujitoa. Hicho ni kitu Cha ajabu mno dunia itatushangaa.

Mbaya zaidi mkataba hausemi je una nafuu ili mbadala ukiachilia mbali kuvunja mkataba.

Kifungu Cha 23(4) kinaenda mbali zaidi na kusema ikitokea sababu yeyote inayotambulika kwenye Sheria za kimataifa ya kupelekea kuvunja mkataba bado mkataba huu hautavunjwa.Tafsiri yake ni kwamba tumeingia kwenye shimo ambalo halina pa kutokea (coup de sac) .

3. Mawanda (scope) ya mkataba pia ni mapana, ni Kama hayana ukomo. Ibara ya 2(1) itaruhusu muwekezaji kujenga na kuendesha miradi ya bandari za Bahari na maziwa yote.

Mkataba unakwenda mbali zaidi hata kwenye kile kinachoitwa logistic parks na trade corridors ambazo bahati mbaya hazijatafisiriwa kwenye mkataba.

Kwa namna mkataba huu ulivyo sisi tutakuwa tumepoteza udhibiti wa bandari zote za bahari na maziwa yote.

Mkataba ungeweka wazi ni bandari zipi hasa kwa sababu kwa namna ya Sasa hata usalama wa nchi unaweza kuwekwa rehani.

4. Mkataba hausemi sisi tutapata nini (consideration) kwa maana ya faida za mradi. Je, sisi tutakusanya Kodi tu? Au tutakuwa wabia?

5. Mkataba hauonyeshi nafasi ya mamlaka ya bandari (TPA) ni ipi katika uendeshaji wa mkataba. Kumbuka kwa mujibu wa sheria TPA ndo chombo chenye mamlaka ya kuendesha bandari zote. Sasa je mkataba huu umefuta sheria hiyo? Kwa mamlaka gani?

Mkataba hauelezei kuhusu usalama wa mapato yetu bandarini na nafasi ya vyombo vya ulinzi na usalama kwaajiri ya usalama wa nchi yetu hasa kwenye marine.

Nafasi pekee ya TPA kwa mujibu ya randama ya kwanza imeachiwa kuendesha na kusimamia " DHOW AND WHARF TERMINAL" ya bandari ya Dar es Salaam.

6. Pamoja na kuweka kipengele Cha local content ili kunufaisha wazawa kwenye ajira na manunuzi kwenye Ibara 13( 2) ambayo haina maana yoyote.
•Kwanza kwa sababu haiweki wazi kwamba "threshold" ya wazawa kwenye ajira itakuwaje.
• Pili hata procurement (manunuzi) ya vitu au "items" au huduma zinazopatikana ndani hailindwi na mkataba kwa sababu kwa mujibu wa bara ya 6(2) ya mkataba huu serikali yetu hauruhusiwi kufanya usumbufu wowote (interference) hata kwenye manunuzi yanayokiuka Sheria isipokuwa tu Kama yanahatarisha usalama (safety and security).

Sasa je wakiamua kuagiza mbao Dubai wakati hapa nchini zipo utawazuia kwa kigezo Cha usalama?

7. Mkataba hausemi nani atawajibika kulipa fidia yoyote inayotokana na utekelezaji wa mradi pamoja na watumishi ambao ajira zao zinaweza athiriwa na mradi.

8. Pamoja na kwamba Ibara ya 26 ya mkataba inaelekea kuruhusu "reservation" utagundua kwa namna Ibara ya 24 ilivyo imepoka kwa mkono mwingine haki ya "reservation" iliyopo kwenye Ibara ya 26 hivyo sioni uwezekano wa nchi yetu kufanya "reservation" kwenye makubaliano bila kukwaza mkataba.

Kwa namna ya mkataba huu tukifanya "reservation" sasa hivi inaweza kupelekea nchi iingie kwenye mgogoro wa kukiuka mkataba.

9. Hata kuridhiwa kwa mkataba huu na Bunge tayari umefanyika nje ya muda. Ibara ya 25(2) ilitaka mkataba uridhiwe ndani ya siku 30 tu na leo ni zaidi ya miezi Saba.

10. Kwa mujibu wa Ibara ya 8(3) (c ) mkataba huu ni kama unatoa umiliki wa ardhi kwa mwekezaji kinyume na Sheria ya ardhi. Kwa mujibu wa sheria ya Ardhi Sura ya 113 Kampuni ya kigeni hairuhusiwi kumiliki ardhi Tanzania. Tulitegemea mkataba useme ardhi zitakuwa chini ya TPA au mamlaka nyingine za serikali na wao watapata "derivative rights" badala ya kuwapa ardhi kwa mgongo wa "lease hold".

Hatuhitaji ufafanuzi wenu,tunachojua mnaiuza nchi kwa waarabu. Ee Mungu Mwenyezi ikupendeze utufute machozi haya. Tupo tayari kuomboleza.
 
Sana tena.
. Wewe ukimuamini usimuamini ndiye Spika wa bunge kwa sasa na ametowa ufafanuzi.

Mwenye wivu ajinyonge.
Faiza, siku hizi hata Kiswahili kinakupiga chenga.

Siyo, "ametowa"
Sema, "ametoa"
 
Hatuhitaji ufafanuzi wenu,tunachojua mnaiuza nchi kwa waarabu. Ee Mungu Mwenyezi ikupendeze utufute machozi haya. Tupo tayari kuomboleza.
Nchi imekwishauzwa, msikilize Mwanasheria kwa umakini

Aseee unaweza kutoa machozi, hiv kweli tuna uongozi au tunaongozwa na wanao ongozwa? Idara ya ulinzi na usalama wa nchi yetu mpo wapi? Nchi inaingia mkataba wa bogaz kama wa ule mto eti maji yote yao, nasi tunakubali,

kama madam president hawajamset kwenye plan yao basi wanampango wa kumchafua mpka akose confidence ya kusimama mbele ya watz.

Anayo nafasi ya kusituka.

Pili kama si ule usemi wa tengeneza tatizo tatua tatizo, basi hili will be the biggest contract fullish ness ever in around the world, vizazi vitakuja kujutia kuwa ktk nchi ambayo kila kitu kimeuzwa.

Hili jambo lingetukia mwaka 1980 haingekuwa shida maana wasomi na teknologia ilikuwa down, lakini 2023? Kila kitu kipo waziii? Hapana hapna hapa na!

Msijizime data.
 
Tupe hiyo taarifa kama unayo. Kama huna unabaki kuwa ni mpotoshaji tu.
Ni kitu gani kilikufanya juzi useme Mwigulu ni waziri wa fedha mbovu kuwahi kutokea kwanini hukubali stratergy zake kwa kigezo kile kile cha kuwa yeye ndiye sasa ni waziri wa fedha kama ambavyo unataka kutuaminisha hapa kuwa kwa kuwa tulia ni speaker basi kila asemacjo ndio ukweli?
 
Hio bandari na jamaa wakome,na afadhali wapewe watu/kampuni yenye tija na nchi ipate mapato inayostahili, na sio kuendelea na wizi tu miaka yote pasipo tija yoyote.
Hakuna anayepinga uwekezaji bali vipengrle vya mkataba haiwezekani kisa wazawa walikuwa wanaiba basi ukaitupe tu kwa wengine wajichotee kabisa na hata wakiiba kuliko wazawa ushinde vunja nao mkataba.
Kilichowatisha watu ni vipengele vya mkataba kama story za kuibinafsisha bandari mbona zimeanza toka mwaka jana na hukiona watu wakipiga kelele mpaka mkataba ulipoonekana
 
Ni kitu gani kilikufanya juzi useme Mwigulu ni waziri wa fedha mbovu kuwahi kutokea kwanini hukubali stratergy zake kwa kigezo kile kile cha kuwa yeye ndiye sasa ni waziri wa fedha kama ambavyo unataka kutuaminisha hapa kuwa kwa kuwa tulia ni speaker basi kila asemacjo ndio ukweli?
Sitaki kukuaminisha chochote, hapa kika mtu na fikra zake, kitachotuweka huru ni ukweli tu.
 
Back
Top Bottom