Sakata la Bandari: Spika Tulia atoa ufafanuzi

Sakata la Bandari: Spika Tulia atoa ufafanuzi

Sana tena.
. Wewe ukimuamini usimuamini ndiye Spika wa bunge kwa sasa na ametowa ufafanuzi.

Mwenye wivu ajinyonge.

1. Kwanini DP imeteuliwa bila mchakato wa wazi wenye ushindani?

2. Je, DP ndio wanachukua nafasi ya TICTS?

3. Kwanini mkataba wa DP unapitia bungeni wakati wa TICTS haukupitia bungeni?

4. Je, mkataba wa DP ni wa muda gani?
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Hio bandari na jamaa wakome,na afadhali wapewe watu/kampuni yenye tija na nchi ipate mapato inayostahili, na sio kuendelea na wizi tu miaka yote pasipo tija yoyote.
"mifisadi ya bandarini"....

Mfano hai ni leo hii asubuhi....

Nilikuwa nakunywa kahawa pale kwa DIWANI njia ya kwenda bomba mbili....yuko mshkaji anafanya kazi TPA Dar....kwa zaidi ya nusu saa alikuwa anamponda mh.Rais SSH na huu uamuzi....akisema anauza nchi....huyu kijana mwenzetu "anakoga" tu Fedha huko TPA....machoni alikuwa anaonyesha hasira ya dhahiri kabisa [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Itapendeza Kama wawakilishi wetu,watapendekeza hili suala liletwe kwa wapiga kura kwa majadiliano zaidi au wabunge wetu,warudi kwenye majimbo yao kutoa elimu na ufafanuzi,ña sisi tutoe maoni yetu. Kuhusu hoja ya kuwa ,hili suala siyo geni au mara ya kwanza,ni vema wawakilishi wetu wakatuambia hao walio tangulia au wanao endelea kutoa huduma bandarini imepata faida au gawio kiasi gani kwa kipindi ambacho walikabidhiwa. Kama wawakilishi wetu watang'ang'ani kuridhiria mswada huo,Ni vema masuala ya tax holiday yakaangaliwa,vinginevyo mwekezaji atafanya kazi akiona kipindi cha kupata tax holiday kinakaribia kumaliza, biashara anahamishia kwenye kampuni nyingine au anauza.
 
"Narudia kusema kwamba, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania litaendelea kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na (anatajwa wadhifa na jinale) Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kukuza uchumi na maendeleo ya Watanzania ..."

Kwa matamshi hayo, ikichukuliwa kwamba sekta ya bandari ni sehemu ya maendeleo ya nchi...
The Guardian na Nipashe wanajua walichokichapisha.. tofauti ya spika na vyombo hivyo ni kuwahi kuchapisha kitakachotokea.
 
Nimuamini huyo spika anayewang'ang'ania covid 19 wawe Bungeni kinyume cha sheria!!?--- nimuamini Spika mvunja sheria??
Mtu asiaminike kwa lolote/yoyote mengine kwa kuwa tu hukumuamini kwa jambo 1 lilokuchusha?!!! Duuh [emoji15][emoji15][emoji1787][emoji1787]
 
Mtu asiaminike kwa lolote/yoyote mengine kwa kuwa tu hukumuamini kwa jambo 1 lilokuchusha?!!! Duuh [emoji15][emoji15][emoji1787][emoji1787]


Jambo hilo linatosha kumjua huyo spika ni CCM stooge.--- haaminiki tena.
 
Kupotosha kupi wakati Mkataba Kati ya Serikali ya Tanzania na kampuni ya DPW ya Emirates Dubai unaacha maswali mengi.

Ni mkataba ambao ulisainiwa kwa mwendokasi bila kuchukua tahadhari juu ya madhara yake yaliyo dhahiri. Mkataba huu haukubaliki kwa sababu nyingi Sana.

1. Mkataba ni wa milele kwa sababu hauna ukomo. Najua wapo waliosema ni wa miaka 100 na wapo waliosema ni wa miezi 12.

Hawa wote sijui wametoa wapi huo muda wa mkataba. Ibara ya 23 ya mkataba na randama zake (appendixes) hakuna popote zinaonyesha mkataba huu ni wa muda gani. Hii inaweza kutafsiriwa kuwa ni mkataba wa kudumu.

Ni kweli unaweza kuwa miaka mia lakini pia hakuna Cha kuzuia uwe wa miaka 1000.


2. mkataba huu una nguvu kuliko Sheria za Tanzania pamoja na Sheria za kimataifa (Takes precedent over national and international law)

Mathalani Ibara 23(4) hairuhusu kuvunja mkataba huu hata pakiwa na ukiukwaji mkubwa (material breach) au kukitokea hali inayopelekea mkataba usitekelezeke (fundamental change of circumstances) ambalo ni Takwa la mkataba wa kimataifa uitwao Vienna Convention on the Law of Treaties,1969 ambao Tanzania imejifunga nao.

Sasa hii tafsiri yake ni kwamba baada ya kusaini mkataba huu hata Dubai wakikiuka kabisa hatuwezi kujitoa. Hicho ni kitu Cha ajabu mno dunia itatushangaa.

Mbaya zaidi mkataba hausemi je una nafuu ili mbadala ukiachilia mbali kuvunja mkataba.

Kifungu Cha 23(4) kinaenda mbali zaidi na kusema ikitokea sababu yeyote inayotambulika kwenye Sheria za kimataifa ya kupelekea kuvunja mkataba bado mkataba huu hautavunjwa.Tafsiri yake ni kwamba tumeingia kwenye shimo ambalo halina pa kutokea (coup de sac) .

3. Mawanda (scope) ya mkataba pia ni mapana, ni Kama hayana ukomo. Ibara ya 2(1) itaruhusu muwekezaji kujenga na kuendesha miradi ya bandari za Bahari na maziwa yote.

Mkataba unakwenda mbali zaidi hata kwenye kile kinachoitwa logistic parks na trade corridors ambazo bahati mbaya hazijatafisiriwa kwenye mkataba.

Kwa namna mkataba huu ulivyo sisi tutakuwa tumepoteza udhibiti wa bandari zote za bahari na maziwa yote.

Mkataba ungeweka wazi ni bandari zipi hasa kwa sababu kwa namna ya Sasa hata usalama wa nchi unaweza kuwekwa rehani.

4. Mkataba hausemi sisi tutapata nini (consideration) kwa maana ya faida za mradi. Je, sisi tutakusanya Kodi tu? Au tutakuwa wabia?

5. Mkataba hauonyeshi nafasi ya mamlaka ya bandari (TPA) ni ipi katika uendeshaji wa mkataba. Kumbuka kwa mujibu wa sheria TPA ndo chombo chenye mamlaka ya kuendesha bandari zote. Sasa je mkataba huu umefuta sheria hiyo? Kwa mamlaka gani?

Mkataba hauelezei kuhusu usalama wa mapato yetu bandarini na nafasi ya vyombo vya ulinzi na usalama kwaajiri ya usalama wa nchi yetu hasa kwenye marine.

Nafasi pekee ya TPA kwa mujibu ya randama ya kwanza imeachiwa kuendesha na kusimamia " DHOW AND WHARF TERMINAL" ya bandari ya Dar es Salaam.

6. Pamoja na kuweka kipengele Cha local content ili kunufaisha wazawa kwenye ajira na manunuzi kwenye Ibara 13( 2) ambayo haina maana yoyote.
•Kwanza kwa sababu haiweki wazi kwamba "threshold" ya wazawa kwenye ajira itakuwaje.
• Pili hata procurement (manunuzi) ya vitu au "items" au huduma zinazopatikana ndani hailindwi na mkataba kwa sababu kwa mujibu wa bara ya 6(2) ya mkataba huu serikali yetu hauruhusiwi kufanya usumbufu wowote (interference) hata kwenye manunuzi yanayokiuka Sheria isipokuwa tu Kama yanahatarisha usalama (safety and security).

Sasa je wakiamua kuagiza mbao Dubai wakati hapa nchini zipo utawazuia kwa kigezo Cha usalama?

7. Mkataba hausemi nani atawajibika kulipa fidia yoyote inayotokana na utekelezaji wa mradi pamoja na watumishi ambao ajira zao zinaweza athiriwa na mradi.

8. Pamoja na kwamba Ibara ya 26 ya mkataba inaelekea kuruhusu "reservation" utagundua kwa namna Ibara ya 24 ilivyo imepoka kwa mkono mwingine haki ya "reservation" iliyopo kwenye Ibara ya 26 hivyo sioni uwezekano wa nchi yetu kufanya "reservation" kwenye makubaliano bila kukwaza mkataba.

Kwa namna ya mkataba huu tukifanya "reservation" sasa hivi inaweza kupelekea nchi iingie kwenye mgogoro wa kukiuka mkataba.

9. Hata kuridhiwa kwa mkataba huu na Bunge tayari umefanyika nje ya muda. Ibara ya 25(2) ilitaka mkataba uridhiwe ndani ya siku 30 tu na leo ni zaidi ya miezi Saba.

10. Kwa mujibu wa Ibara ya 8(3) (c ) mkataba huu ni kama unatoa umiliki wa ardhi kwa mwekezaji kinyume na Sheria ya ardhi. Kwa mujibu wa sheria ya Ardhi Sura ya 113 Kampuni ya kigeni hairuhusiwi kumiliki ardhi Tanzania. Tulitegemea mkataba useme ardhi zitakuwa chini ya TPA au mamlaka nyingine za serikali na wao watapata "derivative rights" badala ya kuwapa ardhi kwa mgongo wa "lease hold".
Sasa useme, mkataba huo una tatizo. Lipi?
Rejea Ibara (Articles) na vifungu nilivyonukuu katika wasilisho langu la awali na maelezo yake
 
Rejea Ibara (Articles) na vifungu nilivyonukuu katika wasilisho langu la awali na maelezo yake
Sijaona tatizo baada ysa kupitia vifubgu vyote.


Ninachokiona ni unoko tu.
 
Yaani serikali ndiyo inalisimamia Bunge,!
 
Sijaona tatizo baada ysa kupitia vifubgu vyote.


Ninachokiona ni unoko tu.

Ningekuelewa kama ungejadili huo unoko.

Nasita kutumia lugha isiyo staha kujibu sentensi yako ya mwisho.

Bandari siyo "Club" ya mpira ambayo mwekezaji anakuwa mmiliki na "exclusive rights". Msikilize Mwanasheria mwingine
 
Back
Top Bottom