Sakata la bandari ya Bagamoyo kuuzwa kwa Waarabu latua Bungeni. Prof. Kitila asema Serikali haijaingia makubaliano yoyote ya uwekezaji

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo amekanusha taarifa zilizozagaa mtandaoni kuwa serikali imeingia mkataba na kampuni mojawapo ya Saudi Arabia, kuwekeza eneo maalum la uchumi la Bagamoyo ikiwemo Bandari.

Profesa Kitila Mkumbo ametoa ufafanuzi huo leo, Ijumaa 14 Februari katika Bunge la 12, Mkutano wa 18, Kikao cha kumi na nne, baada ya Naibu Spika wa Bunge Mussa Azzan Zungu kumtaka atoe tamko kuhusiana na habari hizo zinazosambaa mitandaoni kuhusiana na uwekezaji Bandari ya Bagamoyo.

“Mheshimiwa Waziri kabla ya yote toa tamko kuhusiana na habari zilizosagaa mtandaoni kuhusiana na no maalum la uchumi ikiwemo Bandari ya Bagamoyo” alisema Naibu Spika Zungu.

Profesa Kitila alianza kwa kueleza vipengere sita ambavyo ni lazima vifuatwe ili kukamilisha uwekezaji na kubainisha kuwa taarifa zinazosambazwa hazina ukweli wowote.

“Hatuna makubaliano wala mkataba wa eneo hilo maalum la kiuchumi na kampuni yoyote na taarifa kuwa tumeingia mkataba na kampuni ya Saud Arabia eneo la Uchumi la Bagamoyo hayana ukweli” alisema.

Bunge limeahirishwa hadi 8 Aprili mwaka huu 2025 na litadumu hadi 25 Juni 2025 litakapohutubiwa na kuvunjwa rasmi na Rais Dk Samia Suluhu Hassan.
 
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TAARIFA MUHIMU KUHUSU UENDELEZAJI WA ENEO MAALUM LA KIUCHUMI LA BAGAMOYO (BAGAMOYO SPECIAL ECONOMIC ZONE-BSEZ)

Dodoma, Ijumaa, 14 Februari 2025

1. Serikali ipo katika hatua mbalimbali za kutekeleza programu ya ujenzi wa Eneo Maalum la Kiuchumi la Bagamoyo (Bagamoyo Special Economic Zone BSEZ), ikiwa ni moja ya miradi 17 ya kielelezo iliyopo katika Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Miaka Mitano 2021/22-2025/26.

2. Pamoja na mambo mengine, programu ya ujenzi wa Eneo Maalum la Kiuchumi la Bagamoyo (BSEZ) itahusisha ujenzi wa Bandari, Kongani za Viwanda, Kongani za TEHAMA, Ukanda huru wa Biashara, na Kituo cha reli.

3. Utekelezaji wa programu hii utafanywa na sekta binafsi kwa kushirikiana na serikali kupitia mpango wa ubia kati ya Sekta Binafsi na Sekta ya Umma (Public-Private Partneship-PPP).

4. Wakati wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi wameonesha nia ya kuwekeza katika ujenzi wa miradi mbalimbali iliyopo katika programu ya BSEZ, na wapo katika hatua mbalimbali za mazungumzo na taasisi mbalimbali husika za serikali, Serikali haijaingia makubaliano (commitment) yoyote na mwekezaji yeyote kwa sasa.

5. Hivyo, taarifa zinazosambaa katika mitandao ya kijamii kwamba kampuni moja kutoka Saudi Arabia imepata mkataba wa uwekezaji wa kujenga na kuendesha Bandari ya Bagamoyo sio za kweli.

6. Kutokana umuhimu na ukubwa wa programu ya BSEZ, umma utajulishwa kikamilifu katika kila hatua ya utekelezaji wake.

Kitila Alexander Mkumbo (Mb.),

WAZIRI WA NCHI,

OFISI YA RAIS, MIPANGO NA UWEKEZAJI. Dodoma, Ijumaa, 14 Februari 2025.
 
Inaweza kuwa wachezaji
Inaweza kuwa wasemaji
Inaweza kuwa team mzima itakayo shinda
Ila itakuwa bomba sana raia tukihusishwa zaidi kwenye mgao: Tupewe ticket za bure tukamuona triple C akicheza derby yake ya mwisho nchini. Au nyie wenzangu hamtaki?

Watu wa Chuga mtakuwa na matamasha kadhaa pia msijali.

Asanteni
 
Nimeipenda hii ya prompty answer kwa serikali yetu, kukanusha uongo wa mitandaoni kwa majibu ya kweli.
P
 
Wabunge wa bara amkeni

*Mods acheni kufuta comments kama hizi
Nchi yetu ni urithi wa watoto wetu na wajukuu sio wageni!*

Jitengeni na Uovu!
 
Profesa kabisa anakuwa na majibu mepesi rojorojo namna hii? Ccm akili za watu kama hawa huwa inazipeleka wapi jamani au huwa naona mimi tu?
 
Watufafanulie yale makaratasi walikua wameshkaa wanapga nayo picha na wasaudia ni kwaajili ya nini🤨🤨

Kweli kabisa, maana (digital footprint) nyayo za kidigitali zilizoachwa na mapichapicha ya makabidhiano ya nyaraka zipo mtandaoni hazifutiki au kufichika kirahisi. Unyayo wa kidigitali haufutiki hata mchawi akijaribu kuchota mchanga wa unyayo.

Hivyo ni muhimu watuelezee picha hizo walikuwa wanabadilishana hati za makubaliano MoU au kupeana hati miliki yaani acquisition ya bandari ya Bagamoyo na ilikuwa kwa bei gani ?


SAUDI ARABIA SECURES RIGHTS TO OPERATE TANZANIA’S BAGAMOYO PORTSaudi Arabia has officially secured rights to operate Tanzania’s Bagamoyo Port, one of the largest in East and Central Africa, in a move set to boost trade, logistics, and investment in the region.

The agreement was finalized during a visit by a Saudi trade delegation to Tanzania, aimed at strengthening economic ties between the two nations.

The Tanzanian government granted the Saudi African Investment and Development Co. (SADC) concession and acquisition rights for the port as part of the 'East Gateway Project,' which focuses on expanding trade in East Africa.
 
🙏 Kwahzo picha mkuu kuziweka.sasa manyanga'u watwambie zlikua zanini?
 
Kuna kipindi tulikuwa tunadanganywa nafasi aliyoshika Miss Tanzania kwenye miss world na watanzania tuliendelea tu na maisha, siku hizi hatudanganywi tena maana siku hizi kuna mitandao.

Hili la SAUDIA watu wameshabutua account zimenona mengine yaliyobaki mtajuana wenyewe.
 
Saudi Arabia acquires Bagamoyo Port in Tanzania as part of the “East Gate” project

ByAkram Bin Khalid

12 February، 2025

News Projects

Home » News » Saudi Arabia acquires Bagamoyo Port in Tanzania as part of the “East Gate” project

In a major strategic move, the Kingdom of Saudi Arabia announced its acquisition of Bagamoyo Port in Tanzania, as part of the “East Gate” project, which aims to enhance the region’s position as a global trade hub.

This huge investment comes within the framework of the Kingdom’s efforts to open new investment horizons for Saudi companies in vital sectors, and provide marketing outlets for exporting Saudi products to African markets.
 
CCM wajinga sana wao kila kitu kinacho fanywa na serikali ni kuunga mkono hata kama kina madhara kwa taifa na kwa vile wamejishika kwenye dola basi dola ina saidia nchi kuharibika
 
Ukisikia uhaini ndio huu sasa.

Mwenye macho haambiwi tazama.
Acquire...kupata umiliki au uthibiti wa kitu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…