DOKEZO Sakata la binti wa Yombo lilishatokea kama hilo Kilindi -Tanga

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Rigidity

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2024
Posts
391
Reaction score
482
Habari zenu wanajukwaa. Nimatumaini yangu kwamba mmeamka salama salmin.

Moja kwa moja kwenye mada ni kwamba lipo sakata linalofanana na la binti wa Yombo ambapo limetokea wilayani Kilindi mkoani Tanga. Ni zaidi ya wiki kama tatu hivi tangu tukio hilo lifanyike lakini rushwa ndio inatembea.

Tukio hilo limetokea jirani na mji wa Songe Kijiji kiitwacho Kwamwande ambapo binti huyo aliitwa na jamaa aliyekuwa amezaa nae kwamba eti akachukue matumizi.

Baada ya msichana huyo kufika kumbe walijiandaa vijana nane kumuingilia dada huyo ambae alikuwa amejifungua hata siku arobaini hajamaliza.

Inasemekana vijana waliofanikiwa kumuingilia walikuwa watano. Ingawa baadhi walikamatwa na polisi pia walipewa dhamana kwa sharti la kila mmoja kutoa laki tano. Kilichopo ni ukimya usiokuwa na majibu.
Rushwa imetumika kumkosesha binti huyu haki yake.

OCD Songe achunguzwe kwa kulikalia kimya suala hili na kutowafuatilia wabakaji wengine Ili kumpatia haki msichana huyo.

Hata baada ya kutoka hospitalini msichana huyo aliendelea kupata tabu maumivu makali ya kubakwa na watu watano huko akiwa bado alijifungua siku sio nyingi.

Natoa rai kwa makundi mbalimbali wasaidie haki ya mtanzania huyo.
 
Akina Mwamposa na wenzake badala wakemee haya mapepo kwenye madhabahu yao wao kila siku ni matamasha. Leo ya kuwasha mishumaa, kesho tochi za simu mara sijui komboa nyota. Vitu vya ujingaujinga tu mradi wapige hela. Haya mapepo ya ukatili yaliyoibuka ndo ya kudili nayo kama huo uwezo wanao
 
Sasa hapo wakina mwamposa wameingiaje? wao ndo wanatuma watu wabake au wahusika wa vyombo vya dola kukaa kimya. myonge nmyongeni haki yake mpatie. hapa lawama ni kwa wahusika wanaosaababisha kupindishwa kwa sheria.
 
Akina mwamposa wanahubiri neno LA Mungu - kuacha dhambi. Matendo mabaya kama kubaka, kulawiti ni miongoni mwa dhambi.
 
Akina Mwamposa na wenzake badala wakemee haya mapepo kwenye madhabahu yao wao kila siku ni matamasha. Leo ya kuwasha mishumaa, kesho tochi za simu mara sijui komboa nyota. Vitu vya ujingaujinga tu mradi wapige hela. Haya mapepo ya ukatili yaliyoibuka ndo ya kudili nayo kama huo uwezo wanao
Ukisubiri maombi/miujiza ya hao matapeli ni sawa na kusubiri meli ubungo. Dawa ni kujichukulia sheria mkononi
 
Kama wale wakipata hukumu basi watakamatwa wengi sana , hiyo michezo ya kijinga wanaita ''mtungo'' wanafanyia sana mabinti za watu , halafu wanajisifu kabisa kwenye maskani zao .

Hawa vijana wenye vyumba wanaita ''geto" wengi ni wajinga sana kweny kutesa mabinti za watu.
 
Habari zenu wanajukwaa. Nimatumaini yangu kwamba mmeamka salama salmin
Moja kwa moja kwenye mada ni kwamba lipo sakata linalofanana na la binti wa Yombo ambapo limetokea wilayani Kilindi mkoani Tanga. Ni zaidi ya wiki kama tatu hivi tangu tukio hilo lifanyike lakini rushwa ndio inatembea.

Tukio hilo limetokea jirani na mji wa Songe Kijiji kiitwacho Kwamwande ambapo binti huyo aliitwa na jamaa aliyekuwa amezaa nae kwamba eti akachukue matumizi.

Baada ya msichana huyo kufika kumbe walijiandaa vijana nane kumuingilia dada huyo ambae alikuwa amejifungua hata siku arobaini hajamaliza.

Inasemekana vijana waliofanikiwa kumuingilia walikuwa watano. Ingawa baadhi walikamatwa na polisi pia walipewa dhamana kwa sharti la kila mmoja kutoa laki tano. Kilichopo ni ukimya usiokuwa na majibu.
Rushwa imetumika kumkosesha binti huyu haki yake.

OCD Songe achunguzwe kwa kulikalia kimya suala hili na kutowafuatilia wabakaji wengine Ili kumpatia haki msichana huyo.

Hata baada ya kutoka hospitalini msichana huyo aliendelea kupata tabu maumivu makali ya kubakwa na watu watano huko akiwa bado alijifungua siku sio nyingi.

Natoka rai kwa makundi mbalimbali wasaidie haki ya mtanzania huyo
OCD Songe nnianze kwa kumpa pole kama tukio ni la kweli, JF ni zaidi ya serikaĺi..
 
Unajua kuna vitu vinaumiza sana mama wa mtoto wako unampeleka wakambake washikaji ili iweje sasa??. Kweli tatizo la afya ya akili bongo walitizame kwa makini kuna vichaa tunaishi nao.Serikali ianze kampeni ya watu kupima afya za akili zetu.
 
Sasa hapo wakina mwamposa wameingiaje? wao ndo wanatuma watu wabake au wahusika wa vyombo vya dola kukaa kimya. myonge nmyongeni haki yake mpatie. hapa lawama ni kwa wahusika wanaosaababisha kupindishwa kwa sheria.
Anamaanisha jamii iombewe na hao wanaojiita manabii maana ukatili umezidi. Mtaani ukatili wa kutosha na polisi nao nimakatili maana wanaacha wahalifu watambe mitaani
 
Habari zenu wanajukwaa. Nimatumaini yangu kwamba mmeamka salama salmin
Moja kwa moja kwenye mada ni kwamba lipo sakata linalofanana na la binti wa Yombo ambapo limetokea wilayani Kilindi mkoani Tanga. Ni zaidi ya wiki kama tatu hivi tangu tukio hilo lifanyike lakini rushwa ndio inatembea.

Tukio hilo limetokea jirani na mji wa Songe Kijiji kiitwacho Kwamwande ambapo binti huyo aliitwa na jamaa aliyekuwa amezaa nae kwamba eti akachukue matumizi.

Baada ya msichana huyo kufika kumbe walijiandaa vijana nane kumuingilia dada huyo ambae alikuwa amejifungua hata siku arobaini hajamaliza.

Inasemekana vijana waliofanikiwa kumuingilia walikuwa watano. Ingawa baadhi walikamatwa na polisi pia walipewa dhamana kwa sharti la kila mmoja kutoa laki tano. Kilichopo ni ukimya usiokuwa na majibu.
Rushwa imetumika kumkosesha binti huyu haki yake.

OCD Songe achunguzwe kwa kulikalia kimya suala hili na kutowafuatilia wabakaji wengine Ili kumpatia haki msichana huyo.

Hata baada ya kutoka hospitalini msichana huyo aliendelea kupata tabu maumivu makali ya kubakwa na watu watano huko akiwa bado alijifungua siku sio nyingi.

Natoka rai kwa makundi mbalimbali wasaidie haki ya mtanzania huyo
Ukinisaidia kuniunganisha na walalamikaji itakuwa vema sana. Wakati huo, kwa taarifa hii, ngoja tuwasiliane na huko Tanga.
 
Unajua kuna vitu vinaumiza sana mama wa mtoto wako unampeleka wakambake washikaji ili iweje sasa??. Kweli tatizo la afya ya akili bongo walitizame kwa makini kuna vichaa tunaishi nao.Serikali ianze kampeni ya watu kupima afya za akili zetu.
Afya ya akili imetawala. Hata hao unayosema wafanye ufuatiliaji wenyewe baadhi afya ya akili ni dhoofulihali. Kama yule aliyekua RPC aliyesema dada wa Yombo alikua anajiuza. Hakua sawa yule mama
 
Ukinisaidia kuniunganisha na walalamikaji itakuwa vema sana. Wakati huo, kwa taarifa hii, ngoja tuwasiliane na huko Tanga.
Ahsante sana mama. Ninaamini utafanya ufuatiliaji na utatoa mrejesho jukwaani kama serikali
Binti alishafanyiwa mpaka matibabu lakini hakuna kesi inayoendelea wabakaji haijulikani watachukuliwa hatua au vipi.
Ustawi wa jamii wamelala fofofo
TAKUKURU waingie wanuse watakuambia harufu iliyopo hapo Songe
Ondoeni huyo OCD na hilo dawati lake. Wamekula laki tano kwa kila mbakaji waliyemkamata Ili watoe dhamana

Hii ni aibu mama. Narudia kukutakia ufuatiliaji mwema na utoe mrejesho
 
Back
Top Bottom