DOKEZO Sakata la binti wa Yombo lilishatokea kama hilo Kilindi -Tanga

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Ahsante sana mama. Ninaamini utafanya ufuatiliaji na utatoa mrejesho jukwaani kama serikali
Binti alishafanyiwa mpaka matibabu lakini hakuna kesi inayoendelea wabakaji haijulikani watachukuliwa hatua au vipi.
Ustawi wa jamii wamelala fofofo
TAKUKURU waingie wanuse watakuambia harufu iliyopo hapo Songe
Ondoeni huyo OCD na hilo dawati lake. Wamekula laki tano kwa kila mbakaji waliyemkamata Ili watoe dhamana

Hii ni aibu mama. Narudia kukutakia ufuatiliaji mwema na utoe mrejesho
[emoji7][emoji7]

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Akina Mwamposa na wenzake badala wakemee haya mapepo kwenye madhabahu yao wao kila siku ni matamasha. Leo ya kuwasha mishumaa, kesho tochi za simu mara sijui komboa nyota. Vitu vya ujingaujinga tu mradi wapige hela. Haya mapepo ya ukatili yaliyoibuka ndo ya kudili nayo kama huo uwezo wanao
Manabii wa zama hizi wanawaogopa sana watawala, wanajua kuikosoa Serikali ni kuomba kupokonywa leseni za biashara zao.
 
Yataibuka mengi kwasababu mambomengi yanayohusu ngongo kimtaamtaa yanafichwa sana
Mambo hayo yako katika jamii zetu kubwa ni kwetu wananchi tuache kiitwacho MUHALI....tunafichana na kufichiana maovu kwa kuoneana aibu na hata kuogopana....yako kuanzia miji ya Pwani hadi ya bara.

Serikali yetu sikivu na adhimu inapambana sana na haya mambo kwa nguvu kubwa sana.Ni vyema tukaisaidia kwa "KUFICHUANA".

#Tanzania kwanza[emoji7]

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Manabii wa zama hizi wanawaogopa sana watawala, wanajua kuikosoa Serikali ni kuomba kupokonywa leseni za biashara zao.
Kazi ya manabii si kuikosoa SERIKALI....

Mbona unawatwisha majukumu yasiyo yao kihalisia zaidi ya KIHISIA....

Kwa hulka hizi ndio maana tunapata mawakili wa TLS wenye mitazamo hiyo isiyo na usahihi hata chembe.....

#Never give wisdom to unworthy as it is unjust to the knowledgeable [emoji7]

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Habari zenu wanajukwaa. Nimatumaini yangu kwamba mmeamka salama salmin
Moja kwa moja kwenye mada ni kwamba lipo sakata linalofanana na la binti wa Yombo ambapo limetokea wilayani Kilindi mkoani Tanga. Ni zaidi ya wiki kama tatu hivi tangu tukio hilo lifanyike lakini rushwa ndio inatembea.

Tukio hilo limetokea jirani na mji wa Songe Kijiji kiitwacho Kwamwande ambapo binti huyo aliitwa na jamaa aliyekuwa amezaa nae kwamba eti akachukue matumizi.

Baada ya msichana huyo kufika kumbe walijiandaa vijana nane kumuingilia dada huyo ambae alikuwa amejifungua hata siku arobaini hajamaliza.

Inasemekana vijana waliofanikiwa kumuingilia walikuwa watano. Ingawa baadhi walikamatwa na polisi pia walipewa dhamana kwa sharti la kila mmoja kutoa laki tano. Kilichopo ni ukimya usiokuwa na majibu.
Rushwa imetumika kumkosesha binti huyu haki yake.

OCD Songe achunguzwe kwa kulikalia kimya suala hili na kutowafuatilia wabakaji wengine Ili kumpatia haki msichana huyo.

Hata baada ya kutoka hospitalini msichana huyo aliendelea kupata tabu maumivu makali ya kubakwa na watu watano huko akiwa bado alijifungua siku sio nyingi.

Natoa rai kwa makundi mbalimbali wasaidie haki ya mtanzania huyo
Hivi ni uwendawazimu au ni nini!
 
Kazi ya manabii si kuikosoa SERIKALI....

Mbona unawatwisha majukumu yasiyo yao kihalisia zaidi ya KIHISIA....

Kwa hulka hizi ndio maana tunapata mawakili wa TLS wenye mitazamo hiyo isiyo na usahihi hata chembe.....

#Never give wisdom to unworthy as it is unjust to the knowledgeable [emoji7]

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Manabii wanaogopa!! Huwezi kuwa nabii ukashindwa kukosoa maovu katika jamii unayoishi.

Asante Kanisa Katoriki kwa kuliona tatizo la ubakaji na utekaji na kupotea kwa watu kuwa sugu na kulisemea.

Wengine wanakusanya fungu la kumi kwanza.
 
Si msikiti wala kanisa linaloweza kukosoa serikali kwa ukosoaji wa viashiria vya UHAINI likaendelea kukosoa...popote pale duniani....

Mfano kule SAUDI ARABIA...wale masheikh wakiikosoa serikali ya huko basi ujue kuwa kutakuwa na BALAA....

Tujifunze.....

Serikali zinatoka mbinguni kwa BWANA....

#JMT milele dumu[emoji7]

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Ahsante sana mama. Ninaamini utafanya ufuatiliaji na utatoa mrejesho jukwaani kama serikali
Binti alishafanyiwa mpaka matibabu lakini hakuna kesi inayoendelea wabakaji haijulikani watachukuliwa hatua au vipi.
Ustawi wa jamii wamelala fofofo
TAKUKURU waingie wanuse watakuambia harufu iliyopo hapo Songe
Ondoeni huyo OCD na hilo dawati lake. Wamekula laki tano kwa kila mbakaji waliyemkamata Ili watoe dhamana

Hii ni aibu mama. Narudia kukutakia ufuatiliaji mwema na utoe mrejesho
Mhe Mkuu wa Mkoa amepokea anafuatilia. Tutapata mrejesho
 
Akina Mwamposa na wenzake badala wakemee haya mapepo kwenye madhabahu yao wao kila siku ni matamasha. Leo ya kuwasha mishumaa, kesho tochi za simu mara sijui komboa nyota. Vitu vya ujingaujinga tu mradi wapige hela. Haya mapepo ya ukatili yaliyoibuka ndo ya kudili nayo kama huo uwezo wanao
Mwamposa ni andunje la sisiemu!
 
Back
Top Bottom