Tanzania siyo nchi ya kidini.
Sheria za nchi ndizo sheria kuu kuliko sheria za dini.
Hata hayo madhehebu yamesajiliwa chini ya sheria za Tanzania.
Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971 ndiyo sheria kuu ya masuala ya ndoa Tanzania, ambayo pamoja na mambo mengine mengi, inayapa madhebebu ya dini uwakala wa kufungisha ndoa.
Hizo Canon Law, na Islamic law zina utaratibu wake wa kipekee katika matumizi lakini matumizi yake hayatakiwi kupingana na sheria za nchi.
Mahakama ikivunja ndoa kwa mujibu wa sheria, Kanisa wala msikiti hawapaswi na hawawezi kuingunaisha ndoa husika.
Na kama watagoma kufungisha ndoa nyingine, basi Mkuu wa Wilaya anaweza kufungisha ndoa kwa watu walioachana kisheria.
Kimsingi jukumu la awali la kufungisha ndoa ni la serikali na siyo la dini.
Hizi dini zimepewa uwakala tu na serikali kwa sababu ndizo taasisi zilizo karibu na watu zaidi.