NDOA YA KIKRISTO HAIVUNJIKI. HAKUNA SAHIHI HAPO.
Wengi wanatafiri vibaya maneno aliyoyasema Yesu, ukweli uko hivi.
Mwanamke akiposwa, tayari anadhaniwa kuwa ni mke wa mtu hata kama bado binti hajaagwa kwao. Yusufu aliambiwa asimuache Mariam mkewe, wakati Yusufu anaambiwa hayo Biblia inasema Yusufu alikuwa ameshamposa Mariam tu.
Wayahudi walikuwa na desturi ya kwamba, ukishamposa mwanamke, mwanamke anapaswa asiguswe (kutokufanya mapenzi) kwa miezi 9 ili kubaini kama ana mimba au laah.
Sasa ndani ya hii miezi 9, endapo mwanamke akatembea na mwanaume yoyote au pengine ana mimba changa tafsiri yake ni kwamba mwanamke alifanya uasherati.
Uasherati ni kitendo cha mtu kufanya ngono nje ya ndoa, Uzinzi ni mtu kufanya tendo la ngono kwa asiye mkewe au mumewe.
Sasa Yesu alisema, mtu asimuache mkewe isipokuwa kwa habari ya uasherati, hapo ina maana kwamba, ni sahihi kumuacha mkeo endapo kama umemposa kisha akafanya uashareti ila kama tayari umemposa na wewe ukaenda kulala nae (ndoa kamili inatimizwa hapo ktk tendo) moja kwa moja hiyo ni ndoa kamili maana mmeungana tayari hadi kimwili badala ya kuungana kinafsi na kiroho baada ya familia mbili kupokeana, HAIWEZEKANI TENA KUACHANA.
Sasa hapo wale mitume 12 wakamwambia Yesu kama ni hivyo haipaswi mtu kuoa.
Kwahiyo Mkuu watu wanapaswa kuelewa kwamba NDOA YA KIKRISTO HAIVUNJIKI KWA NAMNA YEYOTE ILE ENDAPO KAMA WATU HAO WAWILI MWANAUME ALITOA MAHALI, NA AKAENDA KULALA NA HUYO MWANAMKE KTK TENDO.