Sakata la DP WORLD: Rais Samia asema Serikali itatafuta mbia wa kuiendesha bandari ya Dar, sasa kuchangia robo tatu ya bajeti ya nchi

Nimekuelewa, kumbe inawezekana hata Bandarini.
 
Wewe hujawahi kumpinga Rais wa sasa
 
Kwa mustakabali huu kwanini bandari yote wasipewe ticts?

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Ewe mwanamke wa Nchi Hiyo bandari hapo ndio roho ya Tanzania unataka kuitoa au kuigawa?
Mbona nmb na nbc zilikuwa zinahemea mashine mpaka walipopewa wawekezaji ndio zikaanza kufanya vizuri tena?

Tuache uoga km bandari ikiwa na mbia inafanya vizuri zaidi basi wapewe.

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Tulisha-ibinafsha bandari ikawa vurugu tupu na hapakuwa na tija yeyote kwenye uninafsishaji ule.Sasa tunarudi tena huko huko,jamani nani katuloga?Kitu gani kinatufanya tuamini kwamba things will be different this time around.

Mimi huwa nashangaa sana,kwani hao wabia si watu kama sisi?Kwa nini wao waweze sisi tusiweze?What is wrong with us.Nadhani ipo haja ya kujitafakari.
 
inaweza kuwa sawa na sio sawa pia..

Watanzania wengi wetu ni wajinga sana, toka nimepata akili hii bandari kila siku ni matatizo tu na failures kuanzia enzi za Mwinyi mpaka Samia bado pale bandarini ni shida tu.....

Watanzania ni wepesi sana kulaumu viongozi wa Serikali huku hao hao ndio watendaji wajinga kula virushwa vidogodogo, uvivu kazini, kutojiongeza, nk...
 
Bandari ya Bagamoyo mkataba uko kwenye mapitio, Bandari ya Mtwara kuna makubaliano na Dangote sijui kufanyaje, sasa ni kwenye bandari ya taifa anapewa mkoloni, huko Ngorongoro sijui anakuja nani.

Swali ni je, mwekezaji wa Bagamoyo na bandari ya Dar atakuwa Mtanzania? au kuna mtu atatoka huko Oman au Dubai na briefcase aingie na proposal yake hapo NMB akope kodi zetu na aanze kuvuna? Kama anatoka nje ya Tanzania basi ni kwamba tangu mkoloni aondoke hatujawahi kuwa na akili ya kujitegemea hadi kuendesha uchumi wetu wenyewe tunahitaji mtu atushikie miguu.
 
Reactions: Ame
Tatizo kubwa lipo katika mamlaka za uteuzi. Hawataki kujiongeza na wameshindwa kutafuta kwa dhati Watanzania wenye sifa stahiki na uthubutu wa kuleta mageuzi chanya.

Udhahifu huu mkubwa pengine unatokana na maslahi yaliyojificha ya kisiasa na kiuchumi. Maslahi yanayopelekea kundi fulani kufaidika kutokana uozo uliopo. Na pengine maguezi ya dhati yakifanyika yatapelekea kuwepo kwa "fear of unknown" kwa kundi hili.

Serikali bila hata haja ya kutafuta mbia mpya, inaweza kufanya kile ambacho kilipelekea kuanzishwa kwa TRA mwaka 1996. Uendeshaji wa Bandari ya DSM uundiwe sheria sheria yake ya kujisimamia na kujiendesha kimapato.

Sheria hii iifanye TPA kuwa "semi autonomous" kiuendeshaji, na ipangiwe malengo ya kimkakati ya kukusanya mapato. Mkurugenzi Mtendaji apewe KPIs katika maeneo ambayo yataainishwa, ili akiboronga aondolewe mara moja. Hizo KPIs zake atazi "cascade" wasaidizi wake, na kwenda chini kwa kila mfanyakazi.

Kila mfanyazi itampasa kupimwa utendaji wake wa kazi na ufanisi wake kwa mwaka kupitia "targets" atakazowekea kupitia hizo KPIs. Yule asiyefikia "targets" ashushwe cheo ili apishe mwingine mwenye kuweza kuleta matokeo chanya.

Tukirudi katika mamlaka za uteuzi, ziwe na uwazi katika kutangaza, kushindanisha na hatimaye kuchagua wale wenye sifa za kuliongoza shirika hili nyeti. Hili suala la kuleta majina yale yale, ama yenye mahusiano ya karibu ama maslali na watawala, ndilo kaburi lenyewe la uendeshaji wa bandari zetu.


Sent from my Nokia 2.3 using JamiiForums mobile app
 
Hatari sana, hadi Bandari anapewa muwekezaji
Hakuna kisichoendeshwa kwa uwekezaji.

Badala ya nchi kutumia kuwekeza kwenye bandari ambayo kila kinachowekezwa hakitunzwi, ni bora vipi? Waendelee kuwekeza kwa kuwapa wasiozalisha faida au uwape wawekezaji wawekeze mitaji yao, waendeshe kivyao, watu wako wapate ajira na wewe hazina unaletewa faida tu?

Hata juha atakuba kuwa ni bora apewe mwekezaji mbia.
 
Wee kweli keng.ee yaaani unaunga mkono huu ujinga
 
Ifike pahala tuanze kupima ubongo wa kila anayetamani kuwa kiongozi ikiwa anakidhi kusimamia nchi na rasilimali zetu!!!
 
Acha tuendelee na kili za kiutopolo topolo kama hizi, kizazi cha watumwa ni watumwa tu, akili za kitumwa profile failure haiwezi kuwa smart never tena ndio iwe elimu unga ungamwana tuendeelee kuvaa leso puani huku tukiuliza na kutafuta mtoa ushuzi. Aibu ya karne. Ugalasa nao unaubora
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…