Sakata la DP WORLD: Rais Samia asema Serikali itatafuta mbia wa kuiendesha bandari ya Dar, sasa kuchangia robo tatu ya bajeti ya nchi

Sakata la DP WORLD: Rais Samia asema Serikali itatafuta mbia wa kuiendesha bandari ya Dar, sasa kuchangia robo tatu ya bajeti ya nchi

Nadhani hapa kuna harufu ya ufisadi.

Hivi kuna Evaluation and monitoring report ya ufanisi wa TICTS toka awe mbia wa kuendesha bandari.

Ni lipi alifanikiwa ambalo TPA wangeshindwa kulifanya.

Ni imani potofu kwamba kila shirika akipatikana mbia basi litafanyakazi kwa ufanisi.
Mkuu , upande wa TICTS wanafanya kazi very professional sio kama huku kwa wazaramo TPA. Swala la mapato ndio wanatakiwa waangalie kwa ukaribu zaidi mifumo ya TICTS imekaa vizuri kuliko TPA . Wabadilishe tu mifumo yao ya malipo inaleta lope hole za watu kupiga pesa. Ndio maana wanapaita shamba la bibi upande wa TPA ila upande wa TICTS mzee hauwezi kufanya magumashi ukafanikiwa .
 
Aiseee! Kuna siku tutatafuta mbia wa kuiendesha serikali maana tumeshashindwa kuiendesha bandari.

Ili bandari ifanye vizuri zaidi inatupasa kuachana na siasa kwenye uendeshaji wake Menejimenti ya Bandari iwekewe malengo na wasiingiliwe na serikali.

Kuwe na mkataba baina ya serikali na menejimentj ya TPA, iwapo watashindwa kufikia malengo yaliyowekwa kwa kila robo mwaka basi kibarua kinaota nyasi na iwapo kuna jinai sheria ichukue mkondo wake.

Nadhani tuanzie hapo.

Vv
Hata Mimi nimejiuliza malengo inayowekewa menejimenti ya bandari ni yapi na ya aina gani na kwa kipindi gani?

Maswali haya na mengine ndiyo ya kupima utendaji wa bandari.

Kama utendaji umepimwa ukaonekana ni hafifu, basi ni jambo jema kuja na malengo mapya na mkakati wa kuyafanikisha. Inawezekana njia ya kumtumia mbia ikawa na tija na ufanisi zaidi katika kufikia malengo yanayokusudiwa. Mbia anaweza kutumika kujenga strategic capability ya kutupa competitive advantage zaidi sokoni dhidi ya bandari shindani kwenye soko la nchi tunazozihudumia.
 
Ni bora kumweka consultant kwenye bandari kuliko kumuweka mwekezaji. Huyu consultant atajua penye upotevu, uwizi na udanganyifu. Pia tutoe mikono ya wanasiasa pale bandarini.
 
Hapana hapana hapana....sikubaliani na mama kwenye hili....hapanaaaaaaa
 
Akili yangu ya kichaga inaniambia badala ya kulia lia, nitafute sehemu ya kuchomeka mrija na mm ninyonye
Haipaswi kuwa hivi, tunatamani Maendeleo tunayoyoana huko nje. Lakini hayakuja hivihivi bila watu kuacha hivyo vitu.
 
Mama tunamshauri aache mara moja huo mpango. Asichokijua hao akina Makamba na Riziwani na akina Mwigulu ni wezi na wajanja wajanja wanatafuta namna ya kukusanya hela za kuhonga chaguzi zijazo. Wazo ni zuri sana ila ajue viongozi wanaomzunguka ni wezi, bora aimarishe ufanisi wa bandari. Mabadiliko ya kutafuta muendeshaji yafanyike kizazi kinachokuja cha waadilifu na siyo
hawa akina Nape
 
Aanze na kutafuta mbia wa kuendesha unguja akifanikiwa huko,ndo tuongee mbia wa kuongoza bandari.Maana huku ni kutuzalau na kutuona watanzania atujaamka
 
Tatizo letu waafrika hatupendi kuumiza vichwa na kupata solution kwa kutumia resource zetu tunakimbilia cheap na easy solutions.Tukitaka kuanzisha mradi the easiest kwetu ni kutafuta Loans and gants na hatuwazi tuzalushe na kuuza nini tupate fedha ya mradi.Light kama Serikali zetu zingekua zinajikita sana kwenye internal solutions tusingekua tunapata wabia uchwara na wala tusingekua tunahangaika kutafuta fedha kwa kujitwisha lawama .Tukiexport sana tunapata fedha ya kigeni ukipata fedha nyingi za kigeni unaweza kuimport technolojia inayoweza kukufanya ujiendeshe mwenyewe.We have to be solid,creative visionary.Human resource bado haitumiki vizuri Africa
 
Mama tunamshauri aache mara moja huo mpango. Asichokijua hao akina Makamba na Riziwani na akina Mwigulu ni wezi na wajanja wajanja wanatafuta namna ya kukusanya hela za kuhonga chaguzi zijazo. Wazo ni zuri sana ila ajue viongozi wanaomzunguka ni wezi, bora aimarishe ufanisi wa bandari. Mabadiliko ya kutafuta muendeshaji yafanyike kizazi kinachokuja cha waadilifu na siyo
hawa akina Nape
Hauna sababu ya kushambulia personalities za watu jadili hoja
 
Nimeona Rais akisema Serikali kutafuta mbia wa kuiendesha bandari ya Dar es Salaam ili kuleta ufanisi na kuongeza mapato.

Ni kweli tunahitaji mbia wa kuiendesha bandari ya Dar? Sisi wenyewe imeshindikana kabisa?

Tumewahi kufanya hivi kwenye reli, shirika la ndege lakini tunajua kilichotukuta.

Hii haiwezi kuja kuiua hii bandari kwa maana tunajuana vizuri sisi hasa linapokuja suala la maslahi.

--
Rais Samia Suluhu amesema maboresho yanafanyika kwenye Bandari ya Dar es Salaam ikiwa ni pamoja na kupata mbia wa kuiendesha, kubadili uongozi na miundombinu ili kuongeza ufanisi.

Amesema robo tatu ya bajeti ya nchi inaweza kutegemea bandari endapo zitafanya kazi inavyotakiwa.

View attachment 2153881
Tatizo kubwa la TPA na mashirika mengi ya umma ni uteuzi wa kisiasa na kuingiliwa kisiasa ktk utendaji wa kazi. Je tunajua vigezo vya uteuzi wa watendaji wakuu na board? Hawa watendaji wanashindanishwa kabla ya kuteuliwa? Wana mamlaka kiasi gani kabla ya kuingiliwa na wizara mama? Kama mbia akija akatangaza nafasi za utendaji ili zishindaniwe, hataingiliwa na wizara mama, kwa nini utendaji usiwe mzuri? Ubia au ubinafsishaji siyo suluhisho pekee.
 
Back
Top Bottom