Sakata la DP WORLD: Rais Samia asema Serikali itatafuta mbia wa kuiendesha bandari ya Dar, sasa kuchangia robo tatu ya bajeti ya nchi

Sakata la DP WORLD: Rais Samia asema Serikali itatafuta mbia wa kuiendesha bandari ya Dar, sasa kuchangia robo tatu ya bajeti ya nchi

Sawa kabisa na hauna headache ya utawala wa bandari. Nitachukua huo mkataba haraka sana. Tena na mishahara na mafao ya wafanyakazi itaboreshwa na wenye kujuwa walifanyalo. Wezi wote wa hapo watatafuta pa kutokea wenyewe.
Hayo mbona hayakufanyika Tanesco, TRL na mwenye ATCL?
 
Hayo yalikuwa madili ya wachahe fulani. Mbona Airtel waliiendesha vizuri walipoinunua?
Kwahiyo hili ni dili la wengi???
Yetu macho, watoto wenu watapiga mateke makaburi yenu.
Mnakula vyote kama fisi hamridhiki mmemaliza ngorongoro mshahamia huko.
Hata watoto wenu watalipa hii gharama.
Karma is really.
 
Hayo yalikuwa madili ya wachahe fulani. Mbona Airtel waliiendesha vizuri walipoinunua?
Ndio nakuuliza kwa nini unasema Airtel na sio ttcl?

Unasema madili ya wachache, hao wachache wenye madili sasa hivi hawapo? Si juzi tu hapo bandari mmesaini mikataba ya wizi
 
Sasa hapo umejichanganya mwenyewe, TTCL ilibinafsishwa kwa MSI waholanzi hawa. Lakini mwisho wa siku TTCL ndio ikafa kabisa, Bora hata walipoacha hao MSI Sasa hivi kidogo Ina uhai.

MSI waliifilisi TTCL na kuiacha na madeni makubwa.

Tukiachana na hao TTCL ambao umewatolea mfano bila.kujua waliowahi kuendeshwa na private.

Kuna Hawa ATCL, Reli na Tanesco, nadhani unajua kilichowakuta nao kwa kufanya hivyo
Tafuta kampuni zenye uwezo wa kufanya biashara tuache kupeana fake companies ziko kampuni wako serious utaratibu uwe wa vigezo hakuna kampuni ikaja kufanya hasara ujuwe mikataba ilikuwa fake. Unaleta kampuni ina record technical finance wako vizuri ili waboreshe huduma za kisasa hakuna kampuni ikaendeshhwa kiserikali ikafanikiwa hakuna tumeuwa mamia ya kampuni na hii SGR wakijifanya kuwapa hawa Railway basi wape miaka miwili tu kwisha, lete watu waendeshe hii ni business ikiwa takataka tu kuzoa hatuwezi mpaka waje kampuni binafsi ndio tutaweza kuendesha kampuni. TTCL ni mfu toka imezaliwa sababu ya ruzuku wanapiga hasara hawajali mishahara si inatoka serikali kuu shida iko wapi.
 
Nimeona Rais akisema Serikali kutafuta mbia wa kuiendesha bandari ya Dar es Salaam ili kuleta ufanisi na kuongeza mapato.

Ni kweli tunahitaji mbia wa kuiendesha bandari ya Dar? Sisi wenyewe imeshindikana kabisa?

Tumewahi kufanya hivi kwenye reli, shirika la ndege lakini tunajua kilichotukuta.

Hii haiwezi kuja kuiua hii bandari kwa maana tunajuana vizuri sisi hasa linapokuja suala la maslahi.

--
Rais Samia Suluhu amesema maboresho yanafanyika kwenye Bandari ya Dar es Salaam ikiwa ni pamoja na kupata mbia wa kuiendesha, kubadili uongozi na miundombinu ili kuongeza ufanisi.

Amesema robo tatu ya bajeti ya nchi inaweza kutegemea bandari endapo zitafanya kazi inavyotakiwa.

View attachment 2153881
Hapo kuna kiongozi mstaafu anaitaka bandari. Tunapiga kweupe
 
Ndio nakuuliza kwa nini unasema Airtel na sio ttcl?

Unasema madili ya wachache, hao wachache wenye madili sasa hivi hawapo? Si juzi tu hapo bandari mmesaini mikataba ya wizi
Kwanza airtel iliibiwa MaGUFULI amekuja ndio serikali ikapata hisa.

Kabla ya hapo serikali haikupata chochote.
 
Katika hili sikubabliani naye kama ni kweli kwasababu huko nyuma, approach hii ilifeli kwa Tanesco na Air Tanzania na Mashirika mengine. Kitu ambacho ningekubaliana naye ni kupata CEO yeyote na kutoka popote duniani asimamie Bandari kama wamatumbi tumeshindwa. Si lazima awe mmatumbi akaishia kuweka wapwa zake na kuharibu kazi.
Hata kama atoke nje ya dunia lazima ataferi hii nchi siasa maji taka..na za kifisadi ndio kipaumbele cha kuongoza nchi...huyo ceo atapigwa matukio sana.

#MaendeleoHayanaChama
 
Ndio nakuuliza kwa nini unasema Airtel na sio ttcl?

Unasema madili ya wachache, hao wachache wenye madili sasa hivi hawapo? Si juzi tu hapo bandari mmesaini mikataba ya wizi
Sasa hivi wapo wengi hapo bandarini, wezi watupu kila idara, siyo wachache. Ndiyo maana naunga mkono atafutwe mbia bandari iendeshwe kibiashara na si kihasara. Au ifaywe ni banadari ndogo tu ya ndani ya nchi utakapokamilika mji kamili wa bandari, Bagamoyo.
 
Kwa nini? Ni kweli sisi tumekubali hatuna kaabisa akili za kuendesha shirika Kama Hilo?

Tunahitaji kwenda na wakati, Pale bado sana. Kauli yakutaka ubia sio kwamba Rais kaamua tu kusema, Kuna kazi kubwa sana imefanyika watu wametembelea bandari kubwa wakaona uendeshaji wake wakapima uwezo wetu wakaona hatutaweza kuwafikia bila ubia na wenye uwezo huo.

Kuna tofauti ya uwezo na akili. Uwezo ni ni akili 100% lakini akili sio uwezo asilimia 100%.
 
Mbia wa nini? kwanini wasitafute CEOs wenye uzoefu mkubwa waliowahi kuendesha bandari kubwa za kueleweka kama Amsterdam, New York etc nina uhakika wapo na wanaweza kunyoosha hiyo bandari kwa mshahara tuu bila ubia
 
Sasa hivi wapo wengi hapo bandarini, wezi watupu kila idara, siyo wachache. Ndiyo maana naunga mkono atafutwe mbia bandari iendeshwe kibiashara na si kihasara. Au ifaywe ni banadari ndogo tu ya ndani ya nchi utakapokamilika mji kamili wa bandari, Bagamoyo.

siku nyingine usiseme kuna wizi bila ushahidi hizo ni hear say
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Kwahiyo hili ni dili la wengi???
Yetu macho, watoto wenu watapiga mateke makaburi yenu.
Mnakula vyote kama fisi hamridhiki mmemaliza ngorongoro mshahamia huko.
Hata watoto wenu watalipa hii gharama.
Karma is really.
Eehh kweli kabisa, tukapeleka na Airport ya Kimataifa Chato, sasa wanatua mbayuwayu tu. Tukawaibia na majumba na magari yao matajiri. Tukawatolea bastola kuwatisha mawaziri hadharani waliposema ukweli. Tukafumua utawala wa bandari na kuweka "The" gang ndiyo waiendeshe. Usiyasahau yote hayo.
 
Msoda kashindwa tunatafuta Mbia sasa

Mimi sindo nakwambia

Akili mtu wangu
 
Bandari kuwekwa chini ya mbia ni kuhatarisha usalama wa nchi mbali uchumi wake.
Hii inaenda kuwa lango la kupitisha mizigo ya magendo, madawa haramu, uingiaji wa silaha haramu pamoja na mambo mengine kama hayo.
 
Back
Top Bottom