Sakata la DP WORLD: Rais Samia asema Serikali itatafuta mbia wa kuiendesha bandari ya Dar, sasa kuchangia robo tatu ya bajeti ya nchi

Sakata la DP WORLD: Rais Samia asema Serikali itatafuta mbia wa kuiendesha bandari ya Dar, sasa kuchangia robo tatu ya bajeti ya nchi

Unaonaje wakabidhi nchi hao matajiri ili nchi iendeshwe na wenye hela wengine tubaki kuwa wafanyakazi wa wenye pesa na urais tumkabidhi tajiri?
Kwai unafikiri nchi zinaendeshwa na watu kama wewe ambao hata kodi hawalipi?

Tumia akili japo kiduchu, mfumo wa Tanzania ni nchi kuendeshwa na wenye pesa. Au huelewi maana ya kulipa kodi?

Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?
 
Lete usha

Lete ushaidi wa uliloandika kama huna chuki binafsi .mwanzo kama nilianza kukuelewa lkn hapa si sawa.changamoto za uendeshaji wa bandari TPA inashindwa kutokana na vitu kadha wa kadha
gharama za ukarabati
tekinologia ya kisasa
ushindani uliopo kwenye bandar za Africa n.k
ebu lete nn kifanyike sio kama unaleta chuki binafsi
Mtu asiyejifunza kutokana na makosa ni MPUMBAVU.
 
Naunga mkono ikiwezekana ifanyike mapema.
wakipata mwekezaji mwenye sifa kama DP ya Dubai / Singapore / Netherlands / South Korea / Japan itakuwa bonus

Mtoa mada unasema huko nyuma zoezi la ubia lilishindikana , ni kweli kwasababu wawekezaji wale hawakuwa na sifa walichaguliwa bila sifa Ndio maana walishindwa
 
a.k.a wahindi wa kariakoo ??!!
 
Nimeona Rais akisema Serikali kutafuta mbia wa kuiendesha bandari ya Dar es Salaam ili kuleta ufanisi na kuongeza mapato.

Ni kweli tunahitaji mbia wa kuiendesha bandari ya Dar? Sisi wenyewe imeshindikana kabisa?

Tumewahi kufanya hivi kwenye reli, shirika la ndege lakini tunajua kilichotukuta.

Hii haiwezi kuja kuiua hii bandari kwa maana tunajuana vizuri sisi hasa linapokuja suala la maslahi.

--
Rais Samia Suluhu amesema maboresho yanafanyika kwenye Bandari ya Dar es Salaam ikiwa ni pamoja na kupata mbia wa kuiendesha, kubadili uongozi na miundombinu ili kuongeza ufanisi.

Amesema robo tatu ya bajeti ya nchi inaweza kutegemea bandari endapo zitafanya kazi inavyotakiwa.

Wakiwaleta wahindi kama walivyofanya TRC itakula kwao! Hata wachina ni hivyohivyo. Wote ni watu wa madili watafilisi bandari.
 
Watu wanapo ona mambo ya kibiashara ayaendi vizuri wanakodisha consultancy firms iliyobobea kwenye area husika of concern kuchunguza na kuwapa mbinu za kusimamia biashara kwa ufanisi.

Sisi tunaleta kampuni iingie ubia wa kuendesha taasisi yenye thamani ya trillion of shillings ambazo zimewekezwa na walipa kodi, huyo mmbia achangii ata cent 5 waje wachote.

Only in Tanzania
 
Wakiwaleta wahindi kama walivyofanya TRC itakula kwao! Hata wachina ni hivyohivyo. Wote ni watu wa madili watafilisi bandari.
Bora ya waarabu kuliko wahindi na wazungu. Tena hawa wahindi mheshimiwa rais aepukanenao mbali hatuwataki.
 
Nchi inavituko sana hii ...bandari ya Dar es Salaam? Mbia? Anyways waache wafanye wanalotaka, inashangaza sana kama hawa watu wana uzalendo na hili taifa.
 
Wewe toa nn kifanyike sio
Unaonaje wakabidhi nchi hao matajiri ili nchi iendeshwe na wenye hela wengine tubaki kuwa wafanyakazi wa wenye pesa na urais tumkabidhi tajiri?
Kejeli zako za kipuuzi ndo nyinyi tunawapa bandari mnashindwa.
 
Watanzania wengi sana wana akili za kitumwa, na mtumwa hata umfanye nini utumwa upo ndani ya damu yake.

Kumiliki kila kitu cha nchi na serikali ndio ikiendeshe ni enzi za utumwa na Ufalme.

Duniani sasa hivi serikali zinabaki kuwa "facilitators", hata ajira zinabaki kuwa kenye private sectors tu kwa wingi. Serikali inabaki na wafanya kazi wachache sana ambao kazi zao zinabaki kuwa acilitators tu na si utendaji wa kina. Feda zinatakiwa mzunguko urudi kwa raia wapate kujiendeleza.

Mama Samia, achana na majuha wenye fikra za kitumwa wachache ambao wanataka kila biashara kubwa iendeshwe na serikali, hao ni wezi na ama wana akilli za kitumwa tu. Bandari zote kubwa duniani sasa hivi haziendeshwi na serikali zao. Sifahamu Tanzania kwanini tumeshelewa sana kwenye hilo?

Mama Samia nakuunga mkono 100% kwenye hili la bandari kupewa mbia aiendeshe.
 
Back
Top Bottom